Kumbe vyeti feki ni kupunguza wafanyakazi serikali haina pesa, vingine mbwembwe

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
Na Dr Christopher Cyrilo

Fikra zingine zinatanabaisha kuwa serikali imetumia kigezo cha vyeti kama ajenda ya kupunguza wafanyakazi, huku vyeti feki imekuwa kisingizio tu. Yaani kwamba, serikali imeona inatumia pesa nyingi kulipa mishahara, kwa hiyo kama ingewapunguza kwa kufuata utaratibu wa 'redundance' pia ingetakiwa kuwalipa, ndipo kukaibuka zoezi la vyeti feki.
Hoja hiyo inaweza kuwa na nguvu kwa sababu kuu nne.

1. Wanaoitwa viongozi wa kisiasa hawajakaguliwa. Kwa sababu nafasi zao zipo moja moja haingewezekana kupunguzwa. Mkuu wa mkoa au wilaya lazima awepo. Haiwezekani mkoa au wilaya isiwe na mkuu. Kwa hiyo hakukuwa na haja ya kuwakagua hawa ilihali ni lazima wawepo. Haingewezekana kupunguza wakuu wa wilaya. Lakini Daktari, nesi, Mwalimu, na wengineo wakifukuzwa watabaki wachache wataendelea.

2. Sababu ya pili ya kukoleza hoja ya kwamba lengo la serikali ni kupunguza wafanyakazi na sio kurudisha heshima ya elimu ni kama inafanana na ya kwanza. Polisi na jeshi la wananchi hawajaguswa kenye zoezi hilo. Na huko ndio tunaambiwa kumefurika wafoji vyeti. Yaani kuna uwezekano kwamba, kati ya polisi kumi, kumi na moja kati yao wamefoji vyeti, nadhani inaeleweka hiyo. Kisingizio kilichotolewa kwa wanasiasa wateule wa Rais cha kwamba wanahitaji kujua kusoma, kuandika na kuhesabu hakina nafasi kwa jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Kwanini hawajakaguliwa? Jibu litakuwa serikali haioni haja ya kuwapunguza, ikiwa hoja tajwa ina ukweli. Hawa wanaisaidia serikali kutawala.

3. Kutumia vyeti vya kidato cha nne pekee kama kigezo cha kufoji vyeti vya elimu. Fikra zinakubaliana kwamba kufoji cheti cha elimu ni kosa kisheria na linahitaji adhabu. Na kama hivyo ndivyo, maana yake hakuna anayetakiwa kuachwa; awe mwanajeshi, askari polisi au mkuu wa wilaya au mkoa. Lakini kwanini hawa hawajaguswa? Ndipo fikra zinapojengeka kwamba, ilitakiwa idadi kubwa ya watu wa kuwapunguza na hivyo ikabidi kutumia vyeti vya kidato cha nne, ili kuwapata wengi bila kuwagusa watumishi wa majeshi.
Serikali ingeweza kutumia vyeti vya kitaaluma (professional certificates). Kwa mfano, daktari aliyesoma chuo kikuu cha Muhimbili, cheti chake cha chuo kikuu cha Muhimbili ndio kikaguliwe. Kukagua cheti cha kidato cha nne kwa mtu aliyemaliza masomo ya udaktari chuo kikuu kigumu kama Muhimbil, lengo ni kutafuta uhalifu na sio kutafuta watumishi wasio na vigezo. Kwa sababu huyu mtu ni daktari, amefuzu masomo ya chuo kikuu na cheti chake cha chuo kikuu ni halali. Kumfukuza kazi hakuna lengo lingine zaidi ya kupunguza wafanyakazi, kwa sababu kazi ya kutibu 1 anaimudu vema. Vivo hivyo kwa walimu, makarani, wahasibu, wauguzi, wanasheria na wengine. Ingekuwa lengo ni kupungua wafanyakazi wasio na vigezo wangekagua vyeti vya kitaaluma, sio vya kidato cha nne. Kwa hiyo lengo hasa ni kupunguza watumishi. Labda kwa sababu ya ukata wa fedha.

4. Sababu ya nne ni kuwa, baada ya serikali kutangaza majina ya watumishi walioghushi vyeti na kuwataka wajifukuzishe kazi wenyewe. Serikali haijaajiri watumishi wa kuziba nafasi zao. Katika mazingira kama haya, nani haoni kuwa lengo la serikali lilikuwa kupunguza watumishi.
Any way! Sababu inaweza kuwafanya sahihi, je! Dhumuni ni sahihi?
Kwanini serikali haiwakagui viongozi wa kisiasa? Kwani wao wakifoji vyeti ni sawa?
Kwanini majeshi yasikaguliwe? Wao wakifoji ni sawa?
Kwanini serikali haitangazi ajira kuziba nafasi zilizoachwa wazi? Sio kwamba imetoa redundance kwa kisingizo cha vyeti feki ili walengwa wasilipwe?

Najiwazia tu mjinga mimi.
 
Je hizo nafasi za kazi za replacement zikizotangazwa watawalipa nini?
 
Hayo yote yamesababishwa na dhuluma aliyofanyiwa Seif na ccm visiwani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 pamoja na sheria kandamizi kwa vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom