Kumbe viongozi wa dini wameamriwa kuwaombea wafalme na wenye mamlaka

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,211
5,936

1 TIMOTHEO 2​

Mafundisho kuhusu sala
1Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, 4ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
 
Ndivyo ilivyo , ukiwa kiongozi Wa dini kazi yako ni kuwaombea Wafalme lakini pia kuombea nchi ili MUNGU asamehe uovu, lakini pia wameamriwa kutii mamlaka, hivyo basi Mkuu Wa nchi akikosea wanatakiwa kumfuata na kumwambia makosa take ili arekebishe na sio kupingana nao hadharani.
 
Kuwaombea ndio, l akini si kuwaombea tu. Unawaombea waongozwe na Mungu katika kutenda haki na kweli ya Mungu kwa wanao waongoza. Mungu anategemea kiongozi akishamsimika na akampa mamlaka ya kutawala awe anasimamia mambo ya kimwili na kiroho. Na haya mambo yako pande mbili giza na Nuru.

Kwa msingi huo ndio utaona ukisoma 1Yohana 4:1-6 Mungu anaongea na watu wake si washetani walio chini ya hizi mamlaka za kidunia.

1. Msiamini kila roho, bali mzijaribu mjue zinatoka kwa Mungu ama kwa shetani. Hii maana yake kweli mamlaka zote zimewekwa na Mungu lakini zina uhuru kufanya mapenzi ya Mungu ama kukengeuka kufanya ya shetani. Zile zilizo kwenda na kujisimika kwa shetani ndio hao manabii wengi wa uongo duniani. Tunaenda na dunia tumeacha tumtangulize Mungu kwanza.

2. Jinsi ya kumjua Roho wa Mungu. Yesu Kristo amekuja katika mwili wa uwanadamu kutoka kwa Mungu. Ukiri huo, ukiona kuna ukakasi kusema Bwana Yesu Asifiwe fikiri mara mbili. Sio bwana asifiwe, mabwana wako wengi, hata shetani ni bwana kwa wafuasi wake. Roho isiyo kiri hili kuwa Yesu katoka kwa Mungu hiyo imetoka kwa shetani na ndiyo inayoitwa roho ya mpinga Kristo ambayo tulisikia inakuja na sasa iko duniani ikifanya kazi. Na mida hii tunaona tu inavyo jidhihirisha.

3. Bali watoto wa Mungu wanaotoka kwa Mungu wameishinda hii roho ya mpinga Kristo kwa sababu Mungu aliye ndani yao ni Mkuu kuliko aliye katika ulimwengu huu ambaye ni shetani akisaidiwa na mawakala wake yaani mpinga Kristo na yule nabii wa uongo( aka utatu wa shetani). Hawa watatu na wafuasi wao wanazungumza ya ulimwengu huu na wa ulimwengu huu na ulimwengu unawasikiliza.
 
1 TIMOTHEO 2​

Mafundisho kuhusu sala
1Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, 4ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
Vipi kama aliyemuweka madarakani huyo kiongozi siyo Mungu bali kawekwa na upande wa pili kupitia mikono ya kikundi fulani cha watu?.Hayo maombi yatafanya kazi?.Maana nilijualo ni kweli kila 'mamlaka' imewekwa na Mungu lakini 'wenye mamlaka' hata shetani hupenyeza wa kwake.
 
1 TIMOTHEO 2​

Mafundisho kuhusu sala
1Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, 4ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
Maana yake unaijua lakini?
Ni kwamba hiyo mistari ya mwisho inabeba uzito.Hiyo ndio motive ya Mungu,kuwe na amani ili ibada kwake ifanyike,watu wahubiriwe kumjua,tuishi kwa amani,na kuwa raia wema.Hiyo ndio sababu mfalme anaombewa yeye na ufalme wake.So kama anakiuka sababu za yeye kuombewa,you know what it means..hizo sala zinageuka kuwa tatizo kwake.Sisi tutasali kubariki ila Mungu atahakikisha aliyeko madarakani ni yule anayestahili sala zetu na baraka zake!
 
Tatizo dini haziruhusu kutumia akili umewahi kujiuliza kwa nini uenezaji wa dini ulienda sambamba na juhudi za kuleta ukoloni?
 
Maana yake unaijua lakini?
Ni kwamba hiyo mistari ya mwisho inabeba uzito.Hiyo ndio motive ya Mungu,kuwe na amani ili ibada kwake ifanyike,watu wahubiriwe kumjua.Hiyo ndio sababu mfalme anaombewa yeye na ufalme wake.So kama anakiuka sababu za yeye kuombewa,you know what it means..hizo sala zinageuka kuwa tatizo kwake.Sisi tutasali kubariki ila Mungu atahakikisha aliyeko madarakani ni yule anayestahili sala zetu na baraka zake!
Kazi kweli kweli.Shetani nae hayupo nyuma kuweka watu wake madarakani.
 
Tatizo dini haziruhusu kutumia akili umewahi kujiuliza kwa nini uenezaji wa dini ulienda sambamba na juhudi za kuleta ukoloni?
Ukiona dini inafunga utashi wako aisee nakushauri kaa na hiyo dini mbali sana.Yaani Mungu akupe utashi halafu eti kirahisi tu mtu na dini yake aje kufunga kufikiri kwako.
 
Kazi kweli kweli.Shetani nae hayupo nyuma kuweka watu wake madarakani.
Taifa likiwa na waomba Mungu wa kweli,hiyo satanic network haipati nafasi,na kama tayari ina nafasi itaanguka.
Ndio maana kunapotokea mfalme mkorofi mwenye kuumiza sana watu,wakimkumbuka Mungu na kulia sana,lazima taifa linaingia kwenye mambo ambayo hayajafikiriwa wala kupangiliwa,sababu Mungu anakuwa kazini kuokoa watu.
Nadhani hata sisi tupo katika stage hiyo.Vilio ni vingi na wakorofi wamepewa nafasi waonyeshe ukorofi wao vizuri ili wakipigwa kofi liwe kofi kweli kweli na yoyote asiwatetee.Ionekane ni haki kwa yatakayowakuta.
Kuna mkono unanyanyuliwa huko juu,tunaoona jicho la tatu tumeanza kufumba macho huku roho zikidunda.Shuhudia the next two years,utanikumbuka.
 
Kila mtu kwenye dini anayoiamini aoni mapungufu yake
Mimi ni Mkristo nisiye na dhehebu na nipo huru kumuhoji Mungu chochote wakati wowote na huwa ananijibu hadi naridhika.Hakuna wa kufunga kufikiri na kuhoji ndani yangu.Nimegundua dini na ukristo ni ardhi na mbingu.
 
Taifa likiwa na waomba Mungu wa kweli,hiyo satanic network haipati nafasi,na kama tayari ina nafasi itaanguka.
Ndio maana kunapotokea mfalme mkorofi mwenye kuumiza sana watu,wakimkumbuka Mungu na kulia sana,lazima taifa linaingia kwenye mambo ambayo hayajafikiriwa wala kupangiliwa,sababu Mungu anakuwa kazini kuokoa watu.
Nadhani hata sisi tupo katika stage hiyo.Vilio ni vingi na wakorofi wamepewa nafasi waonyeshe ukorofi wao vizuri ili wakipigwa kofi liwe kofi kweli kweli na yoyote asiwatetee.Ionekane ni haki kwa yatakayowakuta.
Kuna mkono unanyanyuliwa huko juu,tunaoona jicho la tatu tumeanza kufumba macho huku roho zikidunda.Shuhudia the next two years,utanikumbuka.
Uko sahihi wala sipingani na wewe lakini njia zetu za kupata viongozi zinamfavour zaidi shetani kupenyeza watu wake kuliko Mungu hivyo tunajikuta tunaishi maisha ya mbwa kuukimbiza mkia wake kila awamu.
 
1 TIMOTHEO 2​

Mafundisho kuhusu sala
1Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 3Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, 4ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.
Husikiagi kwa Gwajima akiwaombea? Mbona hufanya hivyo Mara kwa mara.
Ndivyo ilivyo , ukiwa kiongozi Wa dini kazi yako ni kuwaombea Wafalme lakini pia kuombea nchi ili MUNGU asamehe uovu, lakini pia wameamriwa kutii mamlaka, hivyo basi Mkuu Wa nchi akikosea wanatakiwa kumfuata na kumwambia makosa take ili arekebishe na sio kupingana nao hadharani.
Kwa andiko lipi linakataza kuwaonya hadharani? Ulisoma habari za Eliya na mfalme Ahabu?
Je husoma habari za Yeremia na mfalme wa Israeli?
,Alimuonya na alipokataa kutii maneno ya nabii majanga yalimwandama.
 
Bottom line ni kuwaombea viongozi wanaotoa haki wapate baraka na wale waovu waache nyendo zao mbaya.
Dini ya kweli ni ya kutetea haki.
Kiongozi wa dini anayeungana na wanasiasa wasiotoa haki hafai na wala siyo wakili wa Mungu.
 
Uko sahihi wala sipingani na wewe lakini njia zetu za kupata viongozi zinamfavour zaidi shetani kupenyeza watu wake kuliko Mungu hivyo tunajikuta tunaishi maisha ya mbwa kuukimbiza mkia wake kila awamu.
Rafiki,kila kitu kwa wakati wake.
The history of this nation is written by those who fulfil their heavenly purpose,not the evil men who are busy trying to replace them.
Huwezi kureplce betri kwa jiwe halafu saa iendelee kuzunguka.
Pale kila mwema wa taifa hili atakaposimama katika zamu yake,then hao unaowahofia hawatakuwa na la kufanya.
Na tayari mimi naziona dalili.
Now ndimi za watu wetu wengi zinahoji mambo ambayo hayakuhojiwa huko nyuma,na wale mashetani wameanza kuicheza ngoma ambayo hawajui mdundo wake unatokea wapi.
Usihofu,usiumie,just relax,watch and learn..enjoy the coming show!
Mambo makubwa huanza taratibu.Na mwenye mali yake huichukua taratibu hadharani bila hofu,lakini ni mwizi mwenye haraka za kunyata na kuiba kitu haraka bila kuonekana!Sijui umenielewa mkuu?!
 
Rafiki,kila kitu kwa wakati wake.
The history of this nation is written by those who fulfil their heavenly purpose,not the evil men who are busy trying to replace them.
Huwezi kureplce betri kwa jiwe halafu saa iendelee kuzunguka.
Pale kila mwema wa taifa hili atakaposimama katika zamu yake,then hao unaowahofia hawatakuwa na la kufanya.
Na tayari mimi naziona dalili.
Now ndimi za watu wetu wengi zinahoji mambo ambayo hayakuhojiwa huko nyuma,na wale mashetani wameanza kuicheza ngoma ambayo hawajui mdundo wake unatokea wapi.
Usihofu,usiumie,just relax,watch and learn..enjoy the coming show!
Mambo makubwa huanza taratibu.Na mwenye mali yake huichukua taratibu bila hofu,lakini ni mwizi mwenye haraka za kunyata na kuiba kitu haraka bila kuonekana!Sijui umenielewa mkuu?!
Hao wema wako sensitive kujua kwamba wanatakiwa wasimame kwenye zamu zao kwa kiwango gani?.
 
Hao wema wako sensitive kujua kwamba wanatakiwa wasimame kwenye zamu zao kwa kiwango gani?.
Jiulize sana swali hili wewe mwenyewe maana kwa uandishi wako inaonekana ni mmoja wa hao wema wanaoitakia mema nchi hii.

Mimi binafsi ukiniuliza ntakujibu tuu tupo tunauzunguka ukuta wa Yeriko hapa,tumeambiwa mwakani ndio malaika wanapuliza trumpet.😊
 
Back
Top Bottom