Leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu, naibu waziri ameelezea kuhusu matumizi ya uwanja wa ndege wa Chato.
Naibu waziri huyo amedai uwanja huo utakuwa unatumika kusafirisha madini kwani kutoka Mwanza hadi Chato ni zaidi ya kilomita 300 na kusafirisha madini umbali huo ni hatari kwa usalama. Na pia hata wamiliki wa mgodi wa Bulyanhulu wana uwanja wao hivyo ni muhimu serikali nayo kuwa na uwanja wake
Ameongeza kuwa uwanja huo pia utatumika kusafirisha watu na vifaa mbalimbali na hivyo uwanja huo ni kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote ni si wachache.