Kumbe upasuaji katika Hospitali za Serikali sharti malipo kwanza?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo nimepigiwa simu na rafiki yangu ambaye tangu jana alimpeleka mgonjwa wake na hiyo jana aligharamikia ununuzi wa madawa kwa mgonjwa wake huku akiambiwa kuwa madawa husika hayapo kwenye stock.

Leo mgonjwa huyo huyo anahitaji upasuaji na sharti alilopewa ni kulipia kwanza Tshs.240,000 na kupewa risiti ndipo upasuaji uanze kufanyika. Mimi ninajiuliza

(1) Kama huna hizo Tshs.240,000 ina maana unakufa hivi hivi bila msaada wa Serikali?.

(2) Kwenye hospitali za Serikali mbona hiyo gharama ni juu sana?

(3) Kwa nini madawa yanakosa mpaka wahusika wanaenda kwenye maduka ya binafsi ili hali tunaelezwa kuwa awamu ya tano Sekta ya Afya imeongezewa bajeti mpaka 250 billioni?.

Mimi naona kuna tatizo kwenye Sekta ya Afya.
 
Ndugu yangu gharama ya huduma inatokana na upatikanaji wa vifaa tiba na madawa.
Katika kuwezesha hayo tunahimizwa kuwa na bima za afya
 
Hatari sana na hivi uchumi unayumba serikali itazidisha tozo za malipo ya huduma, kodi na faini ndogo ndogo kuweza kuendesha nchi kwa miaka mitano mingine.
 
Back
Top Bottom