Kumbe ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni sehemu mbili za sherehe moja!

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
Ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kumbe ni sehemu ya kwanza na ya pili ya sherehe moja.

Maonesho ya fataki kwenye ufunguzi wa michezo hiyo yalionesha mchoro wa msonobari unaowakaribisha wageni, na maonesho ya fataki kwenye ufugaji wa michezo hiyo yalionesha mchoro wa mti wa mvinje unaoagana na wageni.

Kwenye ufunguzi wa michezo hiyo kwaya ya watoto walifanya maonesho wakivaa mavazi yenye mchoro wa chuimilia ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China. Na kwenye ufungaji wa michezo hiyo, watoto hao walifanya maonesho wakivaa mavazi yenye mchoro wa samaki ili kutoa matumaini mema kwa watu wote.

Ufunguzi wa michezo hiyo, sehemu ya kuhesabu kurudi chini ilionesha vipindi 24 vya jua na kukumbatia ujio wa majira ya Spring. Kwenye ufungaji wa michezo hiyo, wanyama 12 kwenye mzunguko wa mwaka mpya wa jadi wa China walionekana.

Chembechembe za theluji zilioneshwa kwenye ufunguzi huku taa zikioneshwa kwenye ufungaji.

Kwenye ufunguzi wageni kutoka sehemu mbalimbali walialikwa kufurahia kwa pamoja mwezi, na kwenye ufungaji binadamu wote wanasonga mbele kuelekea mustakabali wa pamoja kama familia.

274589925_4682103305234279_6665942832389962679_n.jpg

274671054_4682103291900947_2164100239587880532_n.jpg

274484011_4682103325234277_5475620472297640177_n.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom