Kumbe uchawi upo! Soma hii toka kwenye blog ya mwanamke nyumba

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,309
8,369
Kuna dada mmoja yeye ni mwalimu na mchumba wake ni mfanyakazi katika bank moja hapa mjini, wapenzi hawa wamekuwa katika uhusiano kama miaka kumi sasa na ndipo wa kamuua kuoana mwaka huu ambayo harusi yao ilikuwa jumamosi ya juzi.

wakati wote wa uhusianao wao, mwanamke yeye anasema hakuwahi hata siku moja kutoka nje ya uhusiano wao, lakini kumbe yule kaka alikuwa na mwanamke wa mje ambaye mpaka jumamosi anaoa walikuwa wameshakuwa pamoja kwa miaka minne!!!!huyu dada anasema wala hakuwahi kujua maana mwanaume hakuwa na dalili zozote ambazo zinaweza kumuonyesha ya kwamba alikuwa anatoka nje, wala hakuwahi kubadilika katika mapenzi hata siku moja na hata kama wakigombana yani hakubadilika alikuwa vile vile kama alivyoanza naye mwanzao kwahiyo hata siku moja huyu dada hakujuwa kama huyu kaka alikuwa na mwanamke nje.

sasa kumbe huyu kaka alivyoanza kupanga mipango ya kumuoa huyu mchumba wake wa miaka mingi akamuarifu yule kimada wake kwamba mimi nataka kuoa, kwahiyo nitakuwa busy katika kupanga harusi ukiona siwezi kuwa na wewe muda mwingine ujuwe mipango imenibana, huku kimada akamueleza huyu jamaa ya kwamba hutaoa, kama huwezi kunioa mimi basi hutamuoa huyo mchumba wako labda hunijui. akawa anamwambia kwanini ampotezee muda halafu amuache kwenye mataa, huyu kaka akamueleza sinilikwambia mwanzo kwamba nina mchuma na ukanielewa sasa unabadilika nini lakini nasikia huku kimada akaweka msisitizo ya kwamba kama haolewi yeye basi hata huyo dada mwengine hataolewa.

yule kaka anasema alivyoona vile akaamua kuendelea kupanga mipango yake ya harusi huku hakumwambia kitu chochote yule mchumba wake, na yule dada kumbukeni hajui lolote kama mwanaume ana mtu pembeni, basi kwa vile yule kaka hakutaka matatizo hakwenda tena kumuona yule kimada zaidi ya kumpigia tu simu huku kila akiongea naye bado anasisitiza hataoa kama hamuoi yeye.

alhamisi iliyopita ndio ilikuwa send off ya huyu dada, asubuhi alikuwa mzima kabisa, akaenda salon kupambwa bado alikuwa mzima, mara alivyomaliza kupambwa akasema jamani najisikia vibaya, mara akaanguka, wakamkimbiza hospital, kufika akapimwa kila kitu hana anachoumwa, mara yule dada akaanza kulala mika anaumwa miguu, miguu ikwa miguu mpaka akashindwa kutembea (jamani inauma!!!) akawa analia anasema akisimama miguu inamuisha nguvu kwahiyo mpaka amuegemee mtu ndio akokotwe kutembea.

kumbuka hii ni siku yake ya send off sherehe haikuweza kusimamishwa maana watu walikuwa wameshaanza kufika ukumbini, masikini ikabidi apelekwe hivyohivyo akagoma kuingia ukumbini akawa analia kwa uchungu maana kila mtu alikuwa analia sasa maana hamna anayejuwa liliotokea ghafla tu wakati mtu alikuwa mzima, basi taarifa ikapelekwa ukumbini wakaadithiwa kilichotokea salon mpaka hapo alipo bibi harusi maaba watu walitokwa na machozi ya huruma lakini mc aliwashauri bibi harusi atakapoingia wajitahidi kuchangamka na kufurahia ili asijisikie vibaya.

baada ya kumbembeleza sana bibi harusi mtarajiwa akakubali kuingia ukumbini, akishikiliwa na matron na mama yake mzazi aliingia huku watu wakishangilia, wakicheza ili kumchangamsha, basi sherehe ikaendelea lakini yule dada aliketi tu kila kitu chengine akafanya matron, kama kupeleka keki kwa wakwe na wazazi wake na mengineyo. kwa kweli watu walijitahidi sana kuchangamsha hii sherehe wakati wa chakula ulipofika ilibidi bwana harusi mtarajiwa ndio aende mbele kumchukuwa mke wake wakali na sio kama utaratibu wa kawaida wa bibi harusi kumtafuta mumewe wakale.

basi wakamaliza kula wakati wa zawadi yule dada akaketi kwenye kiti kupokea zawadi zake, na yeye mwishoni akasema anazawadi ya kumpa mumewe mtarajiwa, ndipo akapewa kipaza sauti na kuongea kwa kweli hapa ndio kila mtu mwenye moyo usio wa chuma alipotoa chozi, yule dada akamshukuru sana mumewe na kumwambia anampenda na kumuomba msamaha kwa ghali iliyotokea kwani wote walitaka kufurahia sana siku yao lakini janga hilo likatokea na juu ya yote akamwambia anaujauzito, jamani watu walipiga vigelegele huku machozi yakiwatoka watu walilia jamani hata wanaume machozi yaliwatoka.

yule kaka akaenda kumkumbatia mkewe mtarajiwa akilia machozi kama
 
uchawi upo ndugu yangu, suluhisho la huyo dada ni Mungu tu mana hakuna awezaye kushndana na Mungu, na kwa wanaume jamani mpango wa kando tuachane nao mnawaletea shida wake zenu, watoto wenu, girlfriend zene, na wachumba zenu, dada wa atu amepata adhabu ya buree.
 
Mtu analalamika anaumwa watu wanampeleka ukumbini kufanya nini?Baada ya bi harusi kuonyesha udhaifu saloon ilitakiwa watu waelekeze nguvu kwenye kumsaidia matibabu na si vinginevyo.
 
Hujuhi wabongo kwa kupenda sherehe; watu wako radhi waendelee kula/kunywa hata kama bi harusi yuko ICU.

ndugu nimesoma hbr yako,inatia huruma sana, mpelekeni kanisani,ktk kanisa lolote la kiroho,hasa tag,eagt,kakobe,na mwingira kama upo dar,nashauri waende na huyo jamaa,na amweleze nchungaji stor yote,atapona,aamini hivyo,,jina la Yesu linaponya.
 
Kwa wapagani kitu kinachowahangaisha zaidi ni ulozi au uchawi. Kwa walokole uchawi hauna mamlaka kabisa.
 
Hujuhi wabongo kwa kupenda sherehe; watu wako radhi waendelee kula/kunywa hata kama bi harusi yuko ICU.
Dah kwa kweli hapa hakuna ustaarabu uliotendeka....wamemlazimisha bi harusi aingie ukumbini ili wapige menu.....sema bwana harusi nae kachemsha kulikuwa hakuna haja ya kuconfess mbele ya hadhara yote hiyo labda kama ni bongo movie ingependeza.
 
Hope muhusika au jamaa zake wa karibu watapita JF; Mimi hata siwafahamu nimeikuta hii habari kwenye blogu ya mwanamke nyumba ika ni touch.

ndugu nimesoma hbr yako,inatia huruma sana, mpelekeni kanisani,ktk kanisa lolote la kiroho,hasa tag,eagt,kakobe,na mwingira kama upo dar,nashauri waende na huyo jamaa,na amweleze nchungaji stor yote,atapona,aamini hivyo,,jina la Yesu linaponya.
 
Back
Top Bottom