Kumbe tunaibiwa kiasi hiki? ufafanuzi tafadhari!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe tunaibiwa kiasi hiki? ufafanuzi tafadhari!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Mar 29, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Nimepitia biblia takatifu kwa umakini nikakutana na mistari ambayo imenifanya kwenda kwa baadhi ya watumishi wa mungu kuomba ufafanuzi na niliwatembelea watumishi wanne 1.alinambia acha kabisa kujifanya unajuajua kwenye kanisa langu 2.hiyo ilikuwa agano lakale hivyo leo halina nguvu. 3 akasema bwana mimwenyewe huwa inanichanganya sana hiyo mistari. 4 huyu alibaki kukenua meno tu. Mistari yenyewe ni kumbukumbu la torati 14:22-30. Msaada wanajamvi najua wapo waolimeza bible humu
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Toa ufafanuzi wewe, tunaibiwa nini? Na nani? Tunaibiwa kitu gani? Ukihitaji msaada kama ulivyotoa post yako, maelezo yako yatosheleze ili anayetaka kukusaidia aelewe azungumuzie kipengele gani.

  Nimesoma mistari uliyoelekeza ina mambo mengi, ni yapi unayalenga?
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Mtumishi wa mungu nilielewa mimi ktk mistari hiyo ni zaka/maongeo ya mbegu zako hutumiwa na muhusika/mtoaji nasimfumo uliozoeleka wakupeleka kanisani!!
   
 4. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Wengine hatuna biblia ebu weka jamvini mistari yenyewe
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huo mstari unasemaje?
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sasa unaanza kuwakwaza ze upako, mwingira , kakobe nk
  Haya mamo ya kuquestion kila kitu hayajakaa sawa
   
 7. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Msiache kutoa maongeo ya mbegu zenu yatokayo shambani mwako mwaka baada ya mwaka halafu nendeni mahali mungu alipopachagua kuweka jina lake na mkiwa mbele yake MTAILA zaka ya nafaka yenu ya divai yenu na ya mafuta na ya wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na kondoo wenu. Fanyeni hivi huku mkijifunza kucha bwana mungu. Nanjia ikiwa ni ndefu, nenda uzibadili ziwe fedha na uende mahali mungu alipokarisha jina lake MZITUMIE hizo fedha chochote roho yenu itakachotamani kama nyama yang'ombe,nyama ya kondoo, divai au kileo mle huku mkimuenzi mungu wenu. usimwa kijakazi wala mtumwa wako kwakuwa hana urithi!! Waweza kusoma vizuri mistari hiyo kwani nimeandika vipengele muhimu tu
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Huyo aliyekwambia kanisa langu amejidisqualify mwenyewe katika kazi ya utumishi wa mungu,kwani lengo letu la kumuomba mungu ni kupata baraka zake pamoja na msamaha wa dhambi,sasa kama yeye anasema kanisa ni lake ina maana anaweza kusamehe dhambi za watu au kutoa baraka?
   
 9. Mch.A.Mwasapile

  Mch.A.Mwasapile Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi mwenyewe ni Mchungaji lakn andiko hilo limenipiga chenga ya maudhi
   
 10. M

  Mandi JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kua makini sana katika kiswahili neno tafadhari hakuna hadi muda huu bado tunatumia neno tafadhali ok!kuwa makini na lugha yawatu,home work.jifunze maneno yafuatayo sema haluwa,mpira,mara,...yanatosha kwa kwaleo.unapo leta mada jf hakikisha ni yenye kufahamika.kwaheri
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  aliyeandika hiyo mistari mwenyewe ukimwuliza akufafanulie atatoa macho tu..
   
 12. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Yericko,
  Hakuna anayekuibia ndugu yangu ni wasiwasi wako tu. Isome vizuri Biblia utagundua kuwa kutoa fungu la kumi kanisani ni sahihi kabisa. Maana ni agizo la MUNGU kwa watu wake kwa ajili ya makuhani (Wachungaji).

  Hesabu 18:21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utimishi wautumikao, maana, nihuo utumishi wa hema ya kukutania.

  Hapa kumbuka wana wa Lawi ndo walikuwa ukoo wa Makuhani.

  Waebrania 7:1-5 Kwa maana Melikizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
  2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, na tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
  3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
  4 Basi angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yenu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.
  5 Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo na sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.


  Malaki 3:7-12 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gain?
  8 Je! Mwanadamu atamuibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gain? Mmeniibia zaka na dhabihu.

  9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.

  10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

  11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukusha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.

  12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana watakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi


  Kwahiyo ndugu yangu tia bidii katika kutoa fungu lako la kumi shetani asikudanganye kisha ukavuna laana.
   
 13. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  haya sasa umeyachokoza majawabu ndo hayoooo!
   
Loading...