Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
1,222
2,000
Kifo cha Magufuli kimethibitisha pasipo shaka kuwa sisi kama nchi hatuna utaratibu wowote rasimi wa kikatiba, kisheria au usio wa kisheria unaotuongoza katika kuhesabu au kuzitambua awamu za serikali.

Kama utaratibu rasimi huo, basi ni wazi hauleweki na unapaswa kutazamwa upya ili kuondoa huu mkanganyiko unaojitokeza sasa tena ukiwahusisha viongozi wakubwa tu katika nchi yetu.

Hivyo, tunapaswa kuwa na utaratibu unaotamka rasimi kama awamu ya serikali inahesabiwa pale anapoingia Raisi mpya hata ikitokea Raisi aliepo madarakani anafariki na kurithiwa na makama wake au vinginevyo. .

Tujiulize, ikitokea tunapata Raisi mwingine kutokana na sababu zilizoainishwa na katiba yetu, Raisi huyo atakuwa ni wa serikali ya awamu ya tano, ya sita au ya saba?

Kwakuwa hatuna utaratibu unaoeleweka, hata awamu ya Nyerere inaweza isiwe ni awamu ya kwanza kwani zilikuwepo serikali za kikoloni kabla ya Nyerere kuwa Raisi.

Tujifunze kutokana na makosa kwa kuupatia suluhisho huu mkanganyiko uliopo sasa.

Kama ambavyo mikutano ya Bunge na vikao vyake viko well defined, basi na hizi awamu pamoja na chaguzi zake ziwe well defined.
Tukosoe utendaji wa serikali ya Rais aliyeko madarakani. Lakini tuchukue tahadhari, tusimdogoshe, tusimdiminish kwa namna yoyote Rais wa nchi. Bila huyo Rais tungekuwa tunamlaumu nani kututendea tunavyotaka? Tutamtaka nani atuanzishie mchakato wa uandishi wa katiba mpya?
SSH ni Rais wa sita wa Tanzania na serikali yake ni serikali ya awamu ya 6.

Tusitamani hata siku moja Rais wa nchi kuwa mnyonge lkn tumkosoe na tuikosoe serikali yake ba kuitaka iwajibike tunavyotamani sisi wananchi.
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,890
2,000
Nyerere aliyeoongoza Tanzania kwa miaka 21 akiwa na mawaziri wakuu na makamu rais tofauti alitawala kwa awamu ngapi?
kwani kuna akina nyerere wangapi. Uliwahi kusikia nyerere alikuwa rais wa awamu ngapi?
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,890
2,000
Huo ukweli uliambiwa na nani? Kwanza awamu inarefer jina la Rais. Hii kama hutaki namba 6, sema tu awamu ya Mama Samia, basi. Ukiulizwa ni Rais wa ngapi, sema Rais wa 6 wa JMT.
awamu inareflect jina la rais?...poor you. chekechea uliyomaliza haikuwa chuo kikuu. rudi shule
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,890
2,000
Maana yake ni kuwa samia hataruhusiwa kugombea mwaka 2025 maana ndio mwaka wa mwisho kwa awamu ya tano
anaruhusiwa-ni suala la kichama zaidi. ni rais wa muda tu aliyekabidhiwa madaraka amalizie awamu ya tano. akifanya vyema chama chake kitaamua
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,890
2,000
Mfumo wa makamu kupendekezwa na mgombea mkuu unamnyima power makamu kiutendaji
ndiyo sababu ukiangalia makamu ni kama hana kazi sana. ni bora kuwa na pm tu. rais akienda mbele za haki uchaguzi unaitishwa
 
Ninaweza

JF-Expert Member
Dec 14, 2010
11,143
2,000
Define determinants za awamu
1)uchaguzi mpya
2)rais mpya
3) 1na 2
4) si 1 Wala 2
5)zipo determinants nyengine
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,235
2,000
Kama ni awamu moja, basi hoja ya kwamba awamu ni raisi na sio kipindi fulani cha muda wa utawala ina nguvu.
Awamu moja = rais mpya + uchaguzi mpya (idhani mpya). Kimoja kikikosekana awamu haiwezi kuwa mpya.
 
Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
275
1,000
Imeandikwa wapi tuna-refer Jima la Raisi? Na serikali za kikoloni mbona hatuzihesabu na ziiongoza hii nchi?Nadhani mpaka hapa utakuwa umeona umuhimu au logic ya hizi awamu kuwa defined tena baada ya nchi yetu kuwa huru vinginevyo hata awamu ya Nyerere sio awamu ya kwanza bali tutasema serikali ya kikoloni ndio awamu ya kwanza.
Bila shaka umejichanganya mwenyewe! Serikali za wakoloni wetu, yaani Wajerumani na Waingereza walikuwa na utaratibu wao na sisi tumeanza utaratibu wetu mara baada ya nchi kuwa Jamuhuri.

Katiba hii hii mbovu iliyopo imeweka ukomo wa Urais na namna ambavyo Rais mpya anapatikana. Samia amepatikana kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Aidha ukomo wa Urais wa Magufuli umepatikana kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Kwa hiyo hii si awamu ya Magufuli ni awamu ya Samia.

Samia kuendelea kuwa na Waziri Mkuu yule yule ni mapenzi yake mwenyewe. Hata Rais Mwinyi alifanya hivyo kwa kuteua Waziri Mkuu aliyewahi kutumika wakati wa Nyerere.

Kwa kifupi hii ni awamu ya sita!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,235
2,000
Rais halali wa JMT anapatikana kwa njia mbili tu ambazo ni uchaguzi mkuu au (makamu) kuchukua hatamu baada ya rais kufa au kushindwa kuendelea kwa magonjwa. So Samia ni rais kamili na halali hata kama hakujafanyika uchaguzi
Sikusema siyo rais halali! Hapa tunazungumzia juu ya awamu. Fikiri kwa kina kabla hujaandika.
 
DINHO

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
320
1,000
Imeandikwa wapi?
Usikaze ubongo mzee. We unadhani awamu huangalia nini? Kama ni chaguzi basi nyerere ametawala awamu nne. Awamu huashiria RAIS aleyekuwepo madarakani ni wa ngapi. Kwa mfano Tundu Lissu angeshida ingekuwa AWAMU YA NGAPI MKUU??
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,795
2,000
Bila shaka umejichanganya mwenyewe! Serikali za wakoloni wetu, yaani Wajerumani na Waingereza walikuwa na utaratibu wao na sisi tumeanza utaratibu wetu mara baada ya nchi kuwa Jamuhuri.

Katiba hii hii mbovu iliyopo imeweka ukomo wa Urais na namna ambavyo Rais mpya anapatikana. Samia amepatikana kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Aidha ukomo wa Urais wa Magufuli umepatikana kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. Kwa hiyo hii si awamu ya Magufuli ni awamu ya Samia.

Samia kuendelea kuwa na Waziri Mkuu yule yule ni mapenzi yake mwenyewe. Hata Rais Mwinyi alifanya hivyo kwa kuteua Waziri Mkuu aliyewahi kutumika wakati wa Nyerere.

Kwa kifupi hii ni awamu ya sita!
Kwahiyo Polepole haelewi? Ndio mjue yote haya ni kwasababu hakuna mwongoza wa kisheria wahili jambo na ndio maana kila mtu anajiona yuko sahihi kimtazamo.
 
Izia maji

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
275
1,000
Kwahiyo Polepole haelewi? Ndio mjue yote haya ni kwasababu hakuna mwongoza wa kisheria wahili jambo na ndio maana kila mtu anajiona yuko sahihi kimtazamo.
Polepole amechanganyikiwa! Katiba iko wazi kabisa katika ukomo wa Rais na ukomo wa Rais ndiyo mwisho wa awamu, atakayefuata anaanza awamu yake bila kujali aliyemtangulia amekaa muda gani.
 
NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
993
1,000
Kifo cha Magufuli kimethibitisha pasipo shaka kuwa sisi kama nchi hatuna utaratibu wowote rasimi wa kikatiba, kisheria au usio wa kisheria unaotuongoza katika kuhesabu au kuzitambua awamu za serikali.

Kama utaratibu rasimi huo, basi ni wazi hauleweki na unapaswa kutazamwa upya ili kuondoa huu mkanganyiko unaojitokeza sasa tena ukiwahusisha viongozi wakubwa tu katika nchi yetu.

Hivyo, tunapaswa kuwa na utaratibu unaotamka rasimi kama awamu ya serikali inahesabiwa pale anapoingia Raisi mpya hata ikitokea Raisi aliepo madarakani anafariki na kurithiwa na makama wake au vinginevyo. .

Tujiulize, ikitokea tunapata Raisi mwingine kutokana na sababu zilizoainishwa na katiba yetu, Raisi huyo atakuwa ni wa serikali ya awamu ya tano, ya sita au ya saba?

Kwakuwa hatuna utaratibu unaoeleweka, hata awamu ya Nyerere inaweza isiwe ni awamu ya kwanza kwani zilikuwepo serikali za kikoloni kabla ya Nyerere kuwa Raisi.

Tujifunze kutokana na makosa kwa kuupatia suluhisho huu mkanganyiko uliopo sasa.

Kama ambavyo mikutano ya Bunge na vikao vyake viko well defined, basi na hizi awamu pamoja na chaguzi zake ziwe well defined.
It sounds like Polepole vile!
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
1,327
2,000
Siyo kweli kwa sababu ilani ya uchaguzi inayotumika ni ya awamu ya tano
Hakuna ilani ya awamu ya sita.
Inatekelezwa ilani ya CCM hakuna kitu inayoitwa ilani ya awamu ya tano,endeleeni kulia tu lakini ukweli ndio huo.
 
nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,872
2,000
Inatekelezwa ilani ya CCM hakuna kitu inayoitwa ilani ya awamu ya tano,endeleeni kulia tu lakini ukweli ndio huo.
Nilikuwa nafikiri una akili kumbe jinga tu. Nani analia ? Off point. Pumbavu kabisa. Utakuwa ulipigwa na cheti fake wewe.
 
Buyuni Kwetu

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
743
1,000
Ukweli hii ni awamu ya tano ila CCM wenye nchi yao wamelazimisha kuwa awamu ya sita na Rais ambaye si chaguo la wananchi. LET IT BE.
Samia Suluhu ni chaguo la wananchi kwa sababu alikuwa ni mgombea mwenza wa JPM wakati wa kupiga kura. Kwenye karatasi ya kupigia kura picha yake ilikuwepo pamoja na ya JPM kama mgombea mwenza ambaye anakuwa Makamu wa Rais.

Katiba inasema Rais aliyepo madarakani akifariki au akipata sababu yoyote ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, Makamu wa Rais ndiye anakuwa Rais.

Kama hamkutaka Samia awe Rais watu wa CCM walitakiwa WAMKATAE wakati wa uchaguzi wa watu watakaosimamisha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa Rais na wabunge. Kwa kuwapitisha JPM na Samia kama wagombea ina maana ni KUKUBALI Samia kuwa Rais just in case JPM anashindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu yoyote ile.

Kuhusu awamu it doesn't mean anything. Hata Marekani wanaita Rais aliyepo madarakani kwa idadi ya Rais waliokwisha kutawala USA tangu imepata uhuru. Hata kwa Marais waliofia madarakani aliyefuata haukufanyika uchaguzi bali Makamu wa Rais alichukua madaraka na aliitwa Rais wa namba inayofuatia baada ya huyo aliyefariki.

Hivyo hili neno awamu doesn't mean anything. Tanzania tungehesabu tu ni Rais wa ngapi basi!!!
 
Buyuni Kwetu

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
743
1,000
Samia ni Rais wa ngapi?
Na kuna jambo limewahi kukwama au kutokufanikiwa kwa ufanisi kutokana na matumizi ya neno " awamu"?

Samia ni Rais wa awamu ya sita.
Nashangaa watu wanashupalia neno awamu utafikiri litabadilisha kitu chochote katika utendaji. Samia ni Rais wa 6 wa URT period.
 
Buyuni Kwetu

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
743
1,000
... mkanganyiko zaidi! Kwamba Rais (mmoja) anaweza kutawala kwa awamu mbili? Basi tuna awamu nyingi sana aisee! Kuondoa utata, Samia ni Rais wa 6 wa JMT; upuuzi wa awamu tupa kuleee! Wahuni wa CCM wanautumia kumyumbisha Rais!
Afadhali umeelewa sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom