Kumbe tunahesabu awamu za Serikali bila kuwa na sheria au utaratibu maalum unaotuongoza? Si muhimu sasa kuweka utaratibu rasmi?

SSH amerithi kila kitu kutoka awamu ya 5 kuanzia Baraza la Mawaziri, Bunge, na vyote vinavyounda serikali kisha kufanya marekebisho kidogo baada ya urithi huo.

Nadhani lengo la kuita awamu ya 6 ilikuwa kuweka kwa makusudi mstari unaotenganisha mambo yaliyofanyika na mtangulizi wake pamoja na atakayofanya yeye ili kuji'brand' zaidi.
 
... mkanganyiko zaidi! Kwamba Rais (mmoja) anaweza kutawala kwa awamu mbili? Basi tuna awamu nyingi sana aisee! Kuondoa utata, Samia ni Rais wa 6 wa JMT; upuuzi wa awamu tupa kuleee! Wahuni wa CCM wanautumia kumyumbisha Rais!
Awamu ni mbili tu Mkuu, sasa mkanganyimo unakuja kwenye Ibara ya 37(5) ya Katiba hiyo inakwambia kama raisi akifariki au kujiudhuru Makamu wa raisi akiwa raisi anakuwa ni raisi ndani ya awamu ya aliyefariki/kutolewa/kujihudhuru.

Sasa hapa ndio mkanganyiko wa Samia kuwa raisi ndani ya awamu ya pili ya JPM unapokuja. Ila katiba hiyo hiyo inasema raisi hataruhusiwa kugombea zaidi ya awamu mbili, na kama haitoshi ikasema tena Mtu akiwa raisi (kama ilivyo Samia) akatawala kwa zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha raisi husika basi ataruhusiwa kugombea kwa mara moja tu.

Sasa swali linakuja kwenye Ibara ya 37(5) kwanini inasema huyu aliyechukua nafasi ya raisi aliyefariki kuwa raisi ndani ya awamu ya raisi aliyefarikii? Hii Ibara imekaa vibaya sana na ubaya ikirekebishwa sasa hivi italeta mgogoro wa Samia kutaka kutawala zaidi ya awamu mbili. Ni utata na mtego.
 
Samia ni Raisi wa Sita wa Tanzania anayetawala katika awamu ya tano ya utawala.wa hii nchi awamu kwa tafsiri ya kimantiki ni kipindi cha uongozi wa sarikali (naomba tusitumia tafsiri ya uchanguzi ama kuhesabu namba ya viongozi) kwani Kwa dhana ya uchaguzi Nyerere na Mwinyi hawakuchaguliwa na wananchi hivyo dhana idadi au namba haina mashiko
Hivyo Nyerere ni Raisi wa awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi iliyodumu kwa miaka 21, mwinyi ni Raisi wa awamu ya pili ya uongozi iliyodumu kwa miaka 10 kama ilivyokuwa kwa awamu ya tatu na awamu ya nne Zilizongozwa na Mkapa na Kikwete mpaka kufikia kwa Raisi wa tano aliyeongoza awamu ya Tano ya serikali ya hii nchi

Na hapa ndipo likaja swala la Samia katiba iko wazi kuwa makamu wa Raisi huwa mgombea mwenza hii inamaanisha hushirikiana na mgombea wa nafasi ya uraisi kuunda serikali majukumu yake pamoja na mengine ni kushika nafasi ya raisi anapokuwa hawezi kufanya majukumu yake na hasa kuwa raisi pale raisi anapofariki ....

Naomba nigusie kidogo swala la serikali kuundwa kwa mujibu wa katiba yetu raisi huunda(huunda sio hubadili) baraza la.mawaziri kwa kuanza na waziri mkuu na hii hutokea baada ya uchaguzi mkuu na ikitokea Raisi akalivunja baraza la mawaziri italazimu kuitishwa kwa uchaguzi ......

So far kwa ubora wa uelewa wangu Samia ni Raisi wa Sita Wa Tanzania katika awamu ya Tano ya uongozi wa serikali ya JMT siku akichaguliwana wananchi au akivunja serikali au akifanya.mageuzi na kuunda serikali yake mpya atakuwa raisi wa sita wa Tanzania katika awamu ya sita
Kikwete alivunja baraza la mawaziri kwa kumtoa Lowasa uwaziri Mkuu na haukufanyika uchaguzi hapa umechanganya mambo Mkuu. Ni Bunge likivunjwa ndio tunaingia kwenye uchaguzi Mkuu.

Na ajabu ni kwamba Bunge likitaka kumlazimisha raisi kupitisha sheria yoyote anao uwezo kisheria kuvunja Bunge tukaingia kwenye uchaguzi mkuu.
 
... "Awamu" ni nini? Inakuwa determined vipi? Vigezo? Kama hakuna uataratibu unaoleweka wala vigezo basi kila mmoja (awamu ya 5 vs 6) yuko sahihi ndio hoja ya mleta mada - MKANGANYIKO!
Kwa maoni yangu awamu ni uchaguzi wa rais + rais mpya. Lazima vyote viende kwa pamoja.
 
ukweli ni kwamba samia anaongoza awamu ya tano siyo ya sita. Kungeitishwa uchaguzi mkuu baada ya JPM kufariki ndipo tungesema tuko awamu ya sita. Hata waziri mkuu wake ni yule yule wa awamu ya tano na wala hakutangaza kuvunja baraza lote la mawaziri akaunda jipya. Alikubali kurithi la awamu ya tano akafanya marekebisho madogo tu kuwaondoa asiowapenda hasa wasukuma.

Kusema hii ni awamu ya sita ni janja ya kukwepa failures za kipindi cha JPM akiwa rais na Samia akiwa Makamu.
Hapana Katiba inamtambua si raisi alietokana na uchaguzi pekee Bali hata alieingia kikatiba... Maana ipo wazi kabisa imeleza pale raisi anaposhindwa kufanya majukum yake au kufariki basi anaefwata atatambulika na Katiba kuwa ni raisi... Hii upo ulimwenguni kote awamu ni mtu anaetawala kama raisi na sio muhula wa uchaguzi...
 
Awamu ni mbili tu Mkuu, sasa mkanganyimo unakuja kwenye Ibara ya 37(5) ya Katiba hiyo inakwambia kama raisi akifariki au kujiudhuru Makamu wa raisi akiwa raisi anakuwa ni raisi ndani ya awamu ya aliyefariki/kutolewa/kujihudhuru.

Sasa hapa ndio mkanganyiko wa Samia kuwa raisi ndani ya awamu ya pili ya JPM unapokuja. Ila katiba hiyo hiyo inasema raisi hataruhusiwa kugombea zaidi ya awamu mbili, na kama haitoshi ikasema tena Mtu akiwa raisi (kama ilivyo Samia) akatawala kwa zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha raisi husika basi ataruhusiwa kugombea kwa mara moja tu.

Sasa swali linakuja kwenye Ibara ya 37(5) kwanini inasema huyu aliyechukua nafasi ya raisi aliyefariki kuwa raisi ndani ya awamu ya raisi aliyefarikii? Hii Ibara imekaa vibaya sana na ubaya ikirekebishwa sasa hivi italeta mgogoro wa Samia kutaka kutawala zaidi ya awamu mbili. Ni utata na mtego.
Kiongozi asante sana kwa ufafanuzi murua! Hii Katiba ina matobo mengi sana! Katiba Mpya ni hitaji la dharura sana kwa sasa kwa anayeitakia mema nchi hii!
 
Rais anayepokea kijiti kama imebaki miaka zaidi ya mitatu anahesabiwa ni awamu yake.Ila kama amepokea chini ya miaka miwili anahesabiwa anakamilisha awamu ya mtangulizi wake,Ndiyo maana anaruhusiwa kugombea mara mbili
Mkuu umechanganya jambo hapa, raisi yoyote anayepokea kijiti kwa kufariki/kujiudhuru raisi anakuwa raisi ndani ya awamu ya aliyefariki/kujiudhuru bila kuangalia umebaki muda gani

Ila sasa hii ya miaka mitatu ni kwenye kugombea ili arudi kuwa raisi tena ndio itaangaliwa iyo miaka mitatu.

Katiba Ibara ya 37(5) na Ibara 40(4)
 
Kwa maoni yangu awamu ni uchaguzi wa rais + rais mpya. Lazima vyote viende kwa pamoja.
... naheshimu maoni yako Mkuu kama ambavyo naheshimu maoni ya wengine. Na kwa kuwa kila mmoja anaweza kuwa na maoni yanayokinzana na mwingine then nobody is wrong or right! Hii ni hatari.
 
Kiongozi asante sana kwa ufafanuzi murua! Hii Katiba ina matobo mengi sana! Katiba Mpya ni hitaji la dharura sana kwa sasa kwa anayeitakia mema nchi hii!
Amini nakwambia Mkuu kama Samia akasema anapigania Katiba mpya atapingwa ndani ya CCM hadi na Upinzani sababu itampa uwezo wa kutawala kwa miaka karibu 15 sasa hapo ndio mtihani na hili halionekani kwa sasa ila lipo ni swala la muda tu.

Tumekaa pabaya sana kwenye hili.
 
... wala haina shida; kitawekwa kipengele cha kumzuia kufanya hivyo.
 
Hayo uliyosema sio kweli, Rais anaweza kulivunja baraza la mawaziri wakati wowote na wala hailazimiki ufanyike uchaguzi upya ili rais kuunda upya, Rais anaweza kulivunja na kuliunda upya baraza la mawaziri wakati wowote akiona kuna haja kufanya hivyo.
Kuna member wameshaweka sawa hilo ni Bungesio baraza la mawaziri
 
Samia ni Raisi wa Sita wa Tanzania anayetawala katika awamu ya tano ya utawala.wa hii nchi awamu kwa tafsiri ya kimantiki ni kipindi cha uongozi wa sarikali (naomba tusitumia tafsiri ya uchanguzi ama kuhesabu namba ya viongozi) kwani Kwa dhana ya uchaguzi Nyerere na Mwinyi hawakuchaguliwa na wananchi hivyo dhana idadi au namba haina mashiko
Hivyo Nyerere ni Raisi wa awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi iliyodumu kwa miaka 21, mwinyi ni Raisi wa awamu ya pili ya uongozi iliyodumu kwa miaka 10 kama ilivyokuwa kwa awamu ya tatu na awamu ya nne Zilizongozwa na Mkapa na Kikwete mpaka kufikia kwa Raisi wa tano aliyeongoza awamu ya Tano ya serikali ya hii nchi

Na hapa ndipo likaja swala la Samia katiba iko wazi kuwa makamu wa Raisi huwa mgombea mwenza hii inamaanisha hushirikiana na mgombea wa nafasi ya uraisi kuunda serikali majukumu yake pamoja na mengine ni kushika nafasi ya raisi anapokuwa hawezi kufanya majukumu yake na hasa kuwa raisi pale raisi anapofariki ....

Naomba nigusie kidogo swala la serikali kuundwa kwa mujibu wa katiba yetu raisi huunda(huunda sio hubadili) baraza la.mawaziri kwa kuanza na waziri mkuu na hii hutokea baada ya uchaguzi mkuu na ikitokea Raisi akalivunja baraza la mawaziri italazimu kuitishwa kwa uchaguzi ......

So far kwa ubora wa uelewa wangu Samia ni Raisi wa Sita Wa Tanzania katika awamu ya Tano ya uongozi wa serikali ya JMT siku akichaguliwana wananchi au akivunja serikali au akifanya.mageuzi na kuunda serikali yake mpya atakuwa raisi wa sita wa Tanzania katika awamu ya sita

Wewe hakika umekariri na kudhani wengine wana tatizo la ''kukalili''.
Hakuna kipengere chochote katika katiba ya JMT inayo eleza hayo ya awamu mnayo hangaika nayo katiba imeongelea urais na namna rais anavyo weza kukamilisha, kuacha au kuachishwa madaraka yake ya urais , kuapishwa kwa rais, pamoja na mamlaka ya urais basi, hayo ya awamu endeleeni nayo nyie mnao jadili mambo ya kusadikika
 
Mkuu umechanganya jambo hapa, raisi yoyote anayepokea kijiti kwa kufariki/kujiudhuru raisi anakuwa raisi ndani ya awamu ya aliyefariki/kujiudhuru bila kuangalia umebaki muda gani

Ila sasa hii ya miaka mitatu ni kwenye kugombea ili arudi kuwa raisi tena ndio itaangaliwa iyo miaka mitatu.

Katiba Ibara ya 37(5) na Ibara 40(4)
40 : 4
Screenshot_20211205-193129_Office.jpg
 
Hakuna kipengere chochote katika katiba ya JMT inayo eleza hayo ya awamu mnayo hangaika nayo katiba imeongelea urais na namna rais anavyo weza kuacha madaraka yake na mamlaka ya urais basi hayo ya awamu endeleeni nayo nyie SUKUMA GANG.
Katiba haiwezi kuandika kila kitu kwa ufafanuzi na maelezo unayotaka wewe awamu ni kipindi cha uongozi wa serikali na katiba imeeleza vizuri sana hilo kuanzia mwanzo kwenye uundaji wa serikali hadi hatima yake
 
Ibara ya 40 (4)

SSH amechukua kijiti ikiwa imebaki miaka minne hivyo anastahili kuiita awamu yake ni ya sita kwakuwa hatoruhusiwa kugombea mara mbili.Lakini kama ingekuwa chini ya miaka mitatu angekamilisha kwanza awamu aliyoikuta (5) Alafu angeweza kuendeleza awamu yake.
Screenshot_20211205-193129_Office.jpg
 
Katiba haiwezi kuandika kila kitu kwa ufafanuzi na maelezo unayotaka wewe awamu ni kipindi cha uongozi wa serikali na katiba imeeliza vizuri sana hilo kuanzia mwanzo kwenye uundaji wa serikali hadi hatima yake
Alaaa! Kumbe mengine yanatakiwa kutoka vichwani ee! Kwa jambo muhimu na la msingi kama hili huwezi kisema halipo kikatiba kijana rejea na usome upya katiba ya JMT
 
Ibara ya 40 (4)

SSH amechukua kijiti ikiwa imebaki miaka minne hivyo anastahili kuiita awamu yake ni ya sita kwakuwa hatoruhusiwa kugombea mara mbili.Lakini kama ingekuwa chini ya miaka mitatu angekamilisha kwanza awamu aliyoikuta (5) Alafu angeweza kuendeleza awamu yake.View attachment 2034057
Kuna nyumbu hata katiba hawasomi wanasubiri tu kusikia kundi lao litasema nini ili nao waunge mkono 😅😅😅😅😅😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom