Michael Scofield
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 1,225
- 471
Nilimepata msichana wa kazi kama wiki mbili zilizoisha, nikawa namuomba mawasiliano ya kwao ili niwajue ndugu zake hata kama litatokea tatizo lolote tufahamishane.
Binti akawa ananichengachenga, Nilivyombana sana akaniambia kuwa ametoroka kwao wanataka kumfanyia tohara, kusema kweli nikachoka pamoja na Serikali kupiga kelele kote kumbe mambo haya bado yapo?
Binti anaishi wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, na akaniambia ya kuwa hata watendaji wa kijiji na kata wanayafahamu haya lakini wanayafumbia macho, na akadai maeneo yote ya huko bado wana mila hii, na wanaolazimisha haya ni kinamama na mashangazi.
Nilimshauri kuwa atoe taharifa katika kituo cha polisi, binti akasema anaogopa kuwashitaki wazazi wake, pia atakosana nao Sasa wadau naomba ushauri tumsaidiaje huyu dada na wengineo wanaofanyiwa ukatili kama huu?