Kumbe tohara kwa wasichana bado zipo?

Michael Scofield

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
1,225
471
Nilimepata msichana wa kazi kama wiki mbili zilizoisha, nikawa namuomba mawasiliano ya kwao ili niwajue ndugu zake hata kama litatokea tatizo lolote tufahamishane.
Binti akawa ananichengachenga, Nilivyombana sana akaniambia kuwa ametoroka kwao wanataka kumfanyia tohara, kusema kweli nikachoka pamoja na Serikali kupiga kelele kote kumbe mambo haya bado yapo?

Binti anaishi wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, na akaniambia ya kuwa hata watendaji wa kijiji na kata wanayafahamu haya lakini wanayafumbia macho, na akadai maeneo yote ya huko bado wana mila hii, na wanaolazimisha haya ni kinamama na mashangazi.

Nilimshauri kuwa atoe taharifa katika kituo cha polisi, binti akasema anaogopa kuwashitaki wazazi wake, pia atakosana nao Sasa wadau naomba ushauri tumsaidiaje huyu dada na wengineo wanaofanyiwa ukatili kama huu?
 
Nchi hii ni blah blah tu, tatizo kwenye utekelezaji, mikoa ya kati Dodoma, Manyara, Singida, Mara bado mambo hayo yapo tena bila hata kificho wanaendekeza eti ni mila!
 
.
Nilipokuwa Tanzania miaka ya mwishoni mwa 80's na mwanzoni mwa 90's ilikuwa jambo la kawaida sana kule Mwanza, Shinyanga na Mara.

Poleni sana.
 
bado ipo sana tu. kama una dada lete tumfanyie hiyo kitu huku longido umasaini,heroo suvai?
 
Hilo swala lina harufu ya siasa ndani yake. Ni vigumu kulimaliza hilo tatizo.
 
Lakini pia fikiria the other way round maybe yawezekana akawa ana mabaya yake kafanya huko ndo maana kakimbilia mjini, majuzi rafiki yangu moja alinieleza kuwa mfanyakaz wao ambae amekaa nao almost a year katoroka na kuelekea polisi na kusingizia kuwa kaja na dadake sasa wamepotezana na anataka arudi kwao mkoani. Kumbe yote ilikuwa zuga ya kupewa nauli ama usafiri wa bure kumrudisha kwao. Namaanisha msiwasikilize sana maneno wayasemao hao wasaidizi wetu wa kazi za ndani.
 
Mkuu nimejaribu kulifuatilia ikaonekana hii mila imechukua nafasi kwao, na kuna binti mwingine amefukuzwa kwao bahada ya kukataa kufanyiwa hiyo tohara, na mbaya zaidi wanawatafuatia waume, badala ya kuwasomesha.
 
Lakini nadhani kwa sasa linafanyika kwa siri mno..
We masikio hili swala liko kwa uwazi na kama ni kificho basi ni mijini, kuna bahadhi ya makabila kama haujafanyiwa hii kitu bado haujakuwa na ndoa haupati labda uolewe na kabila ambalo si lako.
 
Bwana Abdala mi na wasiwasi kidogo iweje wewe baba mwenye nyumba umdadisi msichana wa kazi kiasi hicho ? hii kazi si ya mama ? just curious.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom