Kumbe tatizo la cuf ni vyeo tu.

Shapecha

Member
Oct 21, 2010
45
1
Nadhani mliangalia mdahalo wa jana na mliona kwa kiasi gani HR alivyodhihirisha wazi kuwa anahitaji bado kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani. Mlimuona anavyoongea kwa jazba yeye rafu aliziona za CDM tu ila rafu za CCM hakuziona kabisaa kisa wamepewa umakamu wa kwanza wa rais huko kwa Visiwa.

Based on that mdahalo nimegundua tatizo la CUF ni vyeo na wala hakuna kitu kingine. Zanzibar wamepewa umakamu wa rais na mawaziri kadhaa wametulia kimyaa na kukubali kuimplement ilani ya CCM. Huku bara wale ambao ni wabunge na hawana vyeo nao wanataka vyeo sasa, wanataka favour ya CCM itengue kanuni za bunge kwa uwingi wao bungeni ili zitambue kambi zaidi ya moja za upinzani ipo wapi hiyo?

Hamad now anazifikiria zile 100 M alikua anazilamba kama kiongozi wa kambi ya upinzani, Analikumbuka lile STK alilokua analitumia now kapewa mbowe sasa kwa hali ya kawaida lazima achanganyikiwe, sasa anakuja na kisirani cha kuwaumiza CDM ili washindwe kufanya kazi.

Lakini jaribio lake litashindwa kwani bunge la 9 idadi ya wabunge wa upinzani wote ilikua 48, lakini mwaka huu chadema pekee ina wabunge 48 kumbe CDM wanaweza wakawa strong kama bunge lililopita na hawa wapinzania wengine wakajiunga na CCM.

Wapinzani wa kweli wanajulikana ndiyo maana CCM siku hizi haihangaiki na CUF ipo busy na CDM muda wote wakitafuta means ya kuingamiza ambayo moja wapo ni kuiweka CUF karibu na Vyama vingine vya upinzani kama NCCR, TLP na UDP.

HR kiasili ni CCM damu aliingia CUF akitegeme wangelishinda urais wa ZNZ na yeye kulamba vyeo ndani ya serikali ile lakini haikua hivyo wamefight sana wakaona graph inazidi kushuka wakaona dawa ni kujirudi kwa CCM but kwa mgongo wa serikali ya mseto. Now maalim anatembea na Ving'ora humsikii tena akibwatuka.

HR inabidi ajue kuwa cheo ni zamana, Wajipange upya waajenge chama ili kama itawezekana 2015 wapate wabunge wengi zaidi ya wa CDM. Wenzao waliwekeza tangia enzi za Operation sangara thats why now wamevuna kwa kiwango cha kuridhisha. Wareview Operation zinduka yao ilikua na mapungufu gani then wayaboreshe watafanikiwa huenda ila siyo kuwa na Jazba na kupayuka hovyo hovyo.

Ni mtizamo tu!
 
Back
Top Bottom