Kumbe St. Augustine University of Tanzania (SAUT) ni moto wa kuotea mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe St. Augustine University of Tanzania (SAUT) ni moto wa kuotea mbali

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by samirnasri, Jun 29, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Siku za nyuma nilidhani chuo kikuu cha mtakatifu Augustine (SAUT) kilichopo mkoani Mwanza hakina uwezo wa kuzalisha vijana na wasomi wenye kuweza kulisaidia taifa katika kusukuma gurudumu la maendeleo, Nilidhani ni vyuo vikuu vya umma kama vile UDSM ndio vinaweza kudhalisha viongozi bora wa taifa hili lakini sasa hivi nimeamini kuwa SAUT nacho ni moto wa kuotea mbali katika kuandaa viongozi pengine na watumishi watakao sukuma gurudumu la maendeleo mbele.

  Mpaka sasa chuo cha mtakatifu Augustine (SAUT) kimezalisha wabunge watatu machachali walioingia bungeni kupitia vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu uliopita. Wabunge hao ni Ezekiah Wenje, Moses Machali, na Felix Mkosamali.

  Mbali na hao mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Heche pia ni mhitima wa SAUT. jana nilisikiliza michango ya Moses Machali na Wenje katika kujadili bajeti ya waziri mkuu kwa kweli nilivutiwa na jinsi vijana wale walivyokuwa wamejipanga wakati wakitoa hoja zao.

  Wabunge hao walitoa michango yao huku ikiambatana na nukuu "quotations" kutoka kwa wasomi mbalimbali. Hatua hii imenifanya sasa niamini kuwa kumbe SAUT ni moja ya vyuo makini vionavyozalisha viongozi na wataalamu makini katika taifa hili.  [HR][/HR]
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mkosamali hivi sasa yuko SAUT akimalizia mitihani yake ya mwisho. Ni mwanafunzi wa kitivo cha sheria mwaka wa nne.
   
 3. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Vyuo vikuu vya umma vina changamoto kubwa manake walimu wazuri wengi wanakimbilia vyuo binafsi, lakini hili linasababishwa na serikali kutokuwajali watumishi wake..
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,948
  Trophy Points: 280
  UDOM...wanajisifia mtaani tu
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Duh!hivi saut wamefanya research ngap vile?
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  kivipi mkuu?
   
 7. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nimeipenda hii! Kizazi cha viongozi makini ambao ndio tumaini letu ktk Dunia hii ya Utandawazi.
   
 8. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nadhani kuna issue ya 'mtu' na 'chuo'. hao uliowataja hata kama wangesoma chuo gani still wangepafom tu.
   
 9. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  zilizofanywa na hao wanaoandika proposal kila siku kuomba pesa toka nje zimetufikisha wapi or zimetusaidia nini kuondokana na umasikini/matatizo yetu? what???
   
 10. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bado wana safari ndefu, ukilinganisha na UDSM. Si muda muafaka wa kujisifia. Waongeze juhudi zaidi watafika tu.
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wanajitahidi ukisikiliza kipindi cha Star TV cha tuongee asubuhi mara nyingi wanaalika vijana kutoka pale unaona uwezo wao wa kujieleza kama vijana ni wa hali ya juu waendelee kujenga vijana safari yao ndefu
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa, SAUT inatoa wahitimu walioiva vizuri katika fani mbalimbali na wako maeneo mengi tofauti tofauti, hao wabunge kama ulivyowataja ni mifano michache tu ya product nzuri ya SAUT.

  Kazi nzuri SAUT, keep it up.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hili nililitegemea kuliona, na hii ndio kasumba ya baadhi ya UDSM "die hard" kwao digrii ya kweli inapatikana UDSM tu na nsi vinginevyo, tehe tehe tehee!!
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,889
  Likes Received: 2,346
  Trophy Points: 280
  hapa sasa mnawatafuta vijana wa UD. wanakuja muda si mrefu.
   
 15. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hakuna aliyekilinganisha SAUT na UDSM maana UDSM inafikisha miaka 50 hivi karibuni tangu ianzishwe lakini SAUT nadhani umri wake hauzidi miaka 15. UDSM bado kina historia ya kipekee hapa nchini na barani afrika kwa ujumla, lakini wanachokifanya wahitimu hawa wa SAUT ishara nzuri kwamba tutarajie kupata viongozi na wasomi wazuri kutoka katika vyuo vya binafsi pia.
   
 16. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,971
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  SAUT = ROMAN CATHOLIC Why Upinzani tu?
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na mtoa mada kama anakitangaza chuo, lakini chuo kutoa wawakilishi bungeni sio sifa ya kutoa viongozi wazuri, hakuna kipimo cha kupima hilo, maji marefu ni mbunge kasoma chuo gani? au pale mjengoni kuna wabunge wangapi waliomaliza UDSM na hawana michango yeyote ya maana???
   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  prof. baregu anafundisha chuo gani jamani?
   
 19. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  ​Ndo vyuo vilivyopo sasa bongo ulitaka watu wakasome Taliban..................................
   
 20. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ni vyuo gani ambavyo unadhani havizalishi viongozi wa baadae? Kama unavijua vitaje tujaribu kushawishi vifutwe kwani vinatengeneza bomu baya sana
   
Loading...