Kumbe spika Anne Makinda upeo wake ni mdogo sana kwa nafasi aliyonayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe spika Anne Makinda upeo wake ni mdogo sana kwa nafasi aliyonayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Jun 12, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa ibara ya 63(2) ya katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania bunge ndicho chombo kikuu chenye madaraka ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi. Kwa mantiki hiyo, chombo hicho kama taasisi na mojawapo wa muhimili wa dola kinapashwa kiwe na mwenendo ambao haautiliwi mashaka na wananchi kinao wawakilisha. Katika siku za hivi karibuni zimetolewa shutuma nzito dhidi ya bunge hilo, tena kutoka kwa wabunge wenyewe, zinazobainisha kwamba wabunge wa bunge hilo wanalipwa mara mbili (na wakati mwingine zaidi) kwa kazi ile ile. Kwa mtizamo wa haraka haraka, inaonekana bunge letu limekula njama na serikali ili kuwaibia wananchi. Kwa kufanya hivyo bunge hilo limefungua mlango kwa wizi mkubwa zaidi. Kwani naambiwa ya kwamba hata watendaji wanapofanya vikao vyao vya ndani ambavyo ni sehemu ya kazi yao wana lipana posho. Siyo hiyo tu, hata mawaziri wanaofikia kwenye nyumba za serikali wanapokuwa huko Dodoma kwaajili ya bunge hulipwa posho ya kujikimu. Kuna wengine wamekwenda mbali zaidi na kudai kwamba hata viongozi wa kitaifa hulipwa posho ya kujikimu wanapokuwa ziarani huko mikoani, wakati wanafikia ikulu ndogo ambapo kila kitu hulipiwa. Kwa kuzingatia uzito wa suala hili haikutegemewa hata kidogo, kwa spika wa bunge linalotuhumiwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kutokana na mgongano wa maslahi kutoa majibu mepesi kwa tatizo hilo zito. Hii imenifanya niamini ya kuwa spika huyo hataweza kuimudu vizuri nafasi aliyonayo kwakuwa upeo wake wakutafakari mambo ni mdogo sana.
   
 2. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu habari ndo hiyo
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wewe hujagundua kwa nini wabunge wa CCM wapo radhi kuuana kwa ajili ya ubunge, sababu ni posho kibao ambazo mbunge yoyote akimaliza kipindi chake ni kama vile alikuwa ameajiriwa na IMF! Hivi unafikiri mbunge angekuwa analipwa kama askari polisi wangekuwa wanang'ang'ania kwenda kule?
  Ni mpaka haapo tutakapokomesha tatizo la siasa kuwa ajira yenye kulipa kuliko kitu kingine chochote ndipo nchi hii itakaposonga mbele kwani wanafiki wote watakuwa wamejitenga.
   
 4. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi leo ndo unajua? Yule ni limonti wanaoliongoza bunge wapo tena bos wao leo yupo Nigeria kwa TB Joshua fuatilia kuanzia dk hii utamuona anaitwa Edward Ngowai Lowasa ni Mbunge wa Mbulu! Huyo ndo spika halisi wa bunge la tz na ndiye aliyemtoa muasi wa ccm Sita kipenzi cha watz na adui wa ccm!!
   
 5. ngamiamzee

  ngamiamzee JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jibu umepata. 101 mbona hata mtoto wa chekechea anajua
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kwanza jimbo lake kwamwachia nani?
  au naye anakula posho ya uspika na ubunge kwa kikao hicho hicho
  utakuna mawaziri nao wanalipwa posho ya uwaziri na ubunge
  bongo shamba la bibi
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu lakini hili si ni tatizo la kamati ya mahesabu ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Chadema, ndiye anayekua kwenye nafasi nzuri sana ya kulitatua kuliko Spika, ambaye ni lazima apelekewe ripioti na Mwenyekiti wa hiii kamati au?

  Es!
   
 8. M

  MPG JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni janga SUNGU KAMA UKIMWI,wanatumia makamasi kufikiri badala ya akili.ANGUKO LAO NIMETIMIA
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu tatizo langu siyo la mbunge mmoja mmoja,bali bunge kama muhimili unaopashwa kuisimamia serikali; Kuna kila dalili ya kwamba bunge letu limelambishwa sukari na hii ndiyo maana linapiga dana dana linapokuja suala la kuisimamia serikali; ngoja huone kuanzia kesho, mbunge atasimama na kukosoa kila kitu, lakini mwishoni anaunga hotuba ya bajeti mia kwa mia! Juzi nilimsikia mh. Mrema akisema kwakuwa posho hiyo aliikuta ikilipwa, ataendelea kuipokea ingawaje anajua kuwa anawaibia watanzania kwa kulipwa mara mbili kwa kazi hiyo hiyo, Mtu anajiuliza ikiwa mtu kama Mrema ambaye anazunguka nchi nzima kusaka wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri naye anashiriki kuibia umma, atawezaje kuwawajibisha wezi wa umma kwenye halmashauri!
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani kwa CCM hakuna wabunge kuna kundi tu la watafuna pesa za wananchi na kiongozi wao
   
 11. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Halafu wachache waliojitokeza kuwa na ujasiri wa kukomesha 'utamaduni huu mchafu' wameanza kubandikwa majina ya 'kijitafutia umaarufu'. Kuna ubaya gani kama 'kujitafutia umaarufu' huo utawaongezea neema wananchi - angaa watoto wao wakalie madawati wakiwa shuleni!!! Tunawaomba wapiganaji kama Zitto na wenzake wasiogope vijembe vya wahuni. Sasa hivi huo usemi wanauneza kama moto wa kichaka eti 'wanajitafutia umaarufu.'
   
 12. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wa Tz sasa hivi wanaakili sana hizo lugha chafu za kusema wanaokataa sitting allowance wanatafuta umaarufu zina eleweka vizuri huko huko CCM na vibaraka wao huko kwingine wana choche moto zaidi bora wa nyamaze.......utamwambiaje mtu anatafuta kitu ambacho tayari anacho kama sio ujuha ninini?
   
 13. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,453
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Ubunge ni mtaji kwa Shamba la bibi,unategemea hao watapitisha katiba huru na haki ni Ndoto kwani Wabunge wa CCM wanajitoshereza kutunga katiba yao na wakaipitisha labda arudi gavana !
   
 14. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Moto uliowashwa na Zitto hauna budi uendelezwe ili kubainisha mianya yote inayotumiwa na wakubwa kuwaibia watanzania. Hii ni pamoja na kufanya mishahara na marupurupu wanayolipwa viongozi na watendaji wakuu serikalini kuwa siri kali. Hivi kama bunge letu siyo "rubber stamp," mbona linapitisha mambo mengi yakiwa kwenye gunia?
   
 15. A

  Ama Amaa Member

  #15
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Lowasa sio mbunge wa Mbulu
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyo mama hana uwezo na tusitarajie mafanikio yoyote katika muda atakaokuwa madarakani
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,448
  Trophy Points: 280
  Langu ni angalizo tuu, M/Kiti wa Kamati za Hesabu za Serikali, PAC ni Mzee wa Mapesa, John Memosa Cheyo-UDP. LAAC ni Lyatonga wa TLP na Chadema kupitia Zitto wameishika POAC.
   
Loading...