mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,036
Kitendo cha Uturuki kuamua kuanza kupokea makombora ya s-400 ya Urusi, kimemfanya Marekani akiri hadharani hofu yake kuwa silaha za Urusi zikiwa karibu na zile ndege zake za F-35 ambazo Uturuki pia alishazilipia, kutasababisha udhaifu wa zile ndege kugundulika!!!! Sasa najiuliza kwa nini asingesema tutagundua udhaifu wa zile S-400 Russian anti-missile defence system. Hii inaonyesha Marekani hajiamini kabisa kwa silaha zake, na ameamua kutokuziachia ziende Uturuki kwa hofu siri ya udhaifu wake itagundulika. Hii imedhihirisha kuwa Marekani anafahamu kuwa ndege zake zina udhaifu mkubwa na anawauzia "marafiki" zake kwa bei kubwa sana hiku akijua ni kama toy fulani vile!!! Marekani ni vitisho tu lakini mbele ya silaha za mbabe wa ukweli analia lia mpaka anatia huruma. Msikilize anaposema hapa BBC: The officials said they did not want the F-35 jets to be near S-400 systems because they feared Russian technicians would be able to access the F-35's vulnerabilities.
Mimi ningedhani Marekani angefurahia mshirika wa NATO kuwa na silaha za Urusi ili iwe rahisi kwake kuchunguza udhaifu wake>.
Mimi ningedhani Marekani angefurahia mshirika wa NATO kuwa na silaha za Urusi ili iwe rahisi kwake kuchunguza udhaifu wake>.