KUMBE SILAHA ZA MAREKANI HAZINA UJANJA KWA ZILE ZA URUSI.

Hiyo Drone ya Marekani iliyotunguliwa na Iran hutumia technologia ya stealth na ni ya gharama sana. Marekani hawakuamini kama Iran ingeweza kuiona na kuitungua, lakini ilidondoshwa na kombora la bei rahisi tu lakini la teknologia kali.
Hiyo ndege isiyo na rubani (Drone) unayosema ni kwaajili ya Surveillance. Haina silaha zozote na ni Non-Stealthy.
 
Ile drone yao waliipamba kama hivi unavyo zipamba ndege zao. ..Lakini walipigwa Bomba 1 tu chali. .hahaa Mpaka sasa hivi wapo kwenye maabara zao wana jikuna vichwa hawaamini walichokiona. ..wanadhani kuwa kilicho tokea ni njozi tu 'labda ipo siku itatokea wakaamka kwenye huo usingizi mzito
Hahaha! Si kwamba nazipamba. Hiyo Drone na hizi ndege nyingine za kivita ni tofauti kuanzia kimuundo, kazi zake na uwezo wake pia.
 
VITA NI TECHNOLOGY, TECHNOLOGY N UCHUMI. BAJETI YA MAREKANI BILA HATA VITA NI MARA 4 YA BAJETI YA URUSI. KWA LUGHA NYINGINE MAREKANI INAMUDU GARAMA ZA VITA MARA 4 YA URUSI. KUPIGA KOMBORA MOJA TU NI MILLIONS OF DOLLARS, PIA KUZUIA KOMBORA MOJA NI MILLIONS OF DOLLARS. PIA MAREKANI INA USHAWISHI MKUBWA DUNIANI KULIKO URUSI. PIA MAREKANI HAJAFUNGUA HAZINA YA SILAHA, HIZO S500 ANA KAMA HIZO MUDA, KAWEKA STOO.
unaweza ukawa na uchimi mkubwa na vita ukapigwa vile vile
 
Basi tu uwa wanajitoa akili ila wanajua sana kuwa ela sio muhimu sana kwenye mambo ya kivita.mpaka leo hii mungano wa nchi za kiarabu zikiongozwa na Saudi arabia na sapoti ya nchi za EU,zimeshindwa kufika Sanaa(mji mkuu wa Yemen) kuwatoa waasi wa houthis.
Kila siku wanashambulia tu na ndege za kivita ila wakija ardhini wanachezea za uso.mwisho wa siku nchi imezidi kugawika tu mpaka Al-qaida nao kwa sasa wanadhibiti 36% ya Yemen.
Sasa EU na mungano wa nchi za kiarabu si wana uchumi mkubwa lakini huu ni mwaka wa 4 mpaka leo awajafika Sanaa,sasa hii kazi mpe mtu mmoja wa kuitwa Mrusi alafu mpe tu mwaka 1 uwone atakuwa wapi
unaweza ukawa na uchimi mkubwa na vita ukapigwa vile vile
 
Kitendo cha Uturuki kuamua kuanza kupokea makombora ya s-400 ya Urusi, kimemfanya Marekani akiri hadharani hofu yake kuwa silaha za Urusi zikiwa karibu na zile ndege zake za F-35 ambazo Uturuki pia alishazilipia, kutasababisha udhaifu wa zile ndege kugundulika!!!! Sasa najiuliza kwa nini asingesema tutagundua udhaifu wa zile S-400 Russian anti-missile defence system. Hii inaonyesha Marekani hajiamini kabisa kwa silaha zake, na ameamua kutokuziachia ziende Uturuki kwa hofu siri ya udhaifu wake itagundulika. Hii imedhihirisha kuwa Marekani anafahamu kuwa ndege zake zina udhaifu mkubwa na anawauzia "marafiki" zake kwa bei kubwa sana hiku akijua ni kama toy fulani vile!!! Marekani ni vitisho tu lakini mbele ya silaha za mbabe wa ukweli analia lia mpaka anatia huruma. Msikilize anaposema hapa BBC: The officials said they did not want the F-35 jets to be near S-400 systems because they feared Russian technicians would be able to access the F-35's vulnerabilities.
Mimi ningedhani Marekani angefurahia mshirika wa NATO kuwa na silaha za Urusi ili iwe rahisi kwake kuchunguza udhaifu wake>.
HAHA AMERICA AISEE.. THAT'S WHY WE EXPERIENCE COLD WAR IN 1900'S. EVERYONE IS FRIGHTENED BY THE OTHER BUT AMERICA IS MORE SCARED. IF YOU WON'T BELIEVE ME EXPLORE THE RIVAL EXPERIMENT OF WEAPONS BETWEEN M16 AMERICAN RIFLE AND A-47 RUSSIAN RIFLE AND YOU SHALL BOOST YOUR THOUGHTS ON THIS PROPAGANDAS. IT'S LIKE HOW AMERICA IS MORE CONCERNED AND FRIGHTENED BY 5G FREQUENCY REVOLUTION BY CHINESE.
 
Urusi yuko vizuri kwenye Techinolojia ya Siraha.
Kuanzia Ndege za kivita, Nyambizi, Makombola, Meli za kivita, vifaru, Mitambo ya Ulinzi na kadhalika.

Ukitaja Top 5 ya either Vifaru, Helicopta, ndege, Meli, nyambizi, makombola na mitambo ya Ulinzi basi humukosi Murusi kwenye top 5 tena saa zingine akiwa na na mitambo miwili kwenye top 5

Sawa, uko sahihi kwa upande fulani ila Kiswahili chako kinakera kwa kweli.. ''silaha' na siyo 'siraha'; 'makombora' na siyo 'makombola', 'humkosi' na siyo 'humukosi', 'Mrusi' na siyo 'Murusi', 'teknolojia' na siyo 'techinolojia', 'Urusi iko...' na siyo 'Urusi yuko....'
 
VITA NI TECHNOLOGY, TECHNOLOGY N UCHUMI. BAJETI YA MAREKANI BILA HATA VITA NI MARA 4 YA BAJETI YA URUSI. KWA LUGHA NYINGINE MAREKANI INAMUDU GARAMA ZA VITA MARA 4 YA URUSI. KUPIGA KOMBORA MOJA TU NI MILLIONS OF DOLLARS, PIA KUZUIA KOMBORA MOJA NI MILLIONS OF DOLLARS. PIA MAREKANI INA USHAWISHI MKUBWA DUNIANI KULIKO URUSI. PIA MAREKANI HAJAFUNGUA HAZINA YA SILAHA, HIZO S500 ANA KAMA HIZO MUDA, KAWEKA STOO.
Acha uongo chifu,
 
Syria bado ipo kwenye ramani ya dunia licha ya marekani kufanya mashambulizi mfululizo akiwasaidia waasi wamwondoe Al Assad marakani, lakini mitambo ya kizamani yenye asili ya Urusi iliweza kudhibiti ( intercept) makombora kadhaa ya TomaHawks ya kisasa toka marekani.

Mitambo aina ya S-200, s-125 (sa-6 Goa) ambayo hata Tanzania tunayo ilidhibiti mashambulizi ya makombora ya cruise missiles.

Pia mnaosema kuwa Syria inashambuliwa licha ya kuwepo mifumo ya s-400, iko hivi mitambo ya s-400 Urusi iliipeleka kwa ajili ya kulinda kambi zake tu na sio kuilinda Syria. Urusi anatumia askari wa miguu ( infantry soldiers) na light weapons kuisaidia Syria, till now Al Assad is still in power!

Ukweli ni kwamba duniani Hapa Urusi ndiyo taifa lenye ujuzi wa Hali ya juu kwenye silaha, hata kombora lililotungua drone ya marekani ni version of the USSR missiles.
 
Hahahhaha
Sawa, uko sahihi kwa upande fulani ila Kiswahili chako kinakera kwa kweli.. ''silaha' na siyo 'siraha'; 'makombora' na siyo 'makombola', 'humkosi' na siyo 'humukosi', 'Mrusi' na siyo 'Murusi', 'teknolojia' na siyo 'techinolojia', 'Urusi iko...' na siyo 'Urusi yuko....'
 
Marekani kutaka kujua madhaifu ya S-400?

In Fact tayari kwa asilimia kubwa madhaifu ya S-400 yapo wazi na kuna njia mbalimbali tu za kukabiliana nazo ukiachana na Stealthy Technology ambayo imekuwa ikiipa Urusi wakati mgumu sana kukabiliana nayo.

Kwa upande wa Urusi, kama ni swala la kugundua udhaifu wa hizo ndege kumbuka S-400 zipo kule Syria chini ya Urusi ukiacha zile 'S-300'.

Tayari ndege za F-35 zimeshafanya Operations mbalimbali Syria zikifanywa na Majeshi mbalimbali ya anga kama vile RAF ya Uingereza na Israeli Air Force zikitumika Variants tofauti tofauti za F-35 na Urusi imekuwa ikizifuatilia kwa muda mrefu tu.

Hizo ndege ni ngumu sana kuzichunguza (Detect) na si kwamba hazionekani kabisa kwenye Radar. La hasha.

Kwa kutumia Low-Frequency Radars ambazo Urusi imekuwa ikiwekeza kwazo na kuzifanyia uboreshaji kwa muda sasa, inawezekana kuziona hizo F-35.

Tatizo ni kwamba kuiona tu F-35 ama F-22 kwenye Radar bado haitoshi.

Kuna zoezi la Interception ambapo ili zoezi lifanikiwe kuna michakato mbalimbali ambapo kwa hizo Low-Frequency Systems bado ni mtihani mkubwa sana kwa Modern SAM System yeyote ile kwa sasa.

Hilo ni kutokana na madhaifu yake ikiwemo 'Accuracy' ndogo hivyo ni ngumu kuyaongoza makombora kwa ufanisi kuelekea kwenye Targets husika.

Hapo zitahitajika High-Frequency Radars ili kuweza kuzifuatilia hizo ndege wakati wa kuzishambulia ambapo kwa hizo Radar kuziona tu hizo ndege mtihani unarudi palepale.

Hiyo ni kutokana na uwezo wa hizo ndege na jinsi zilivyoundwa kuziwezesha kuwa na vitu kitaalamu vikijulikana kama Low Radar Cross Sections katika hizo Frequency kubwa.

Isitoshe katika Operations kubwa hizi ndege huambatana pia na mifumo mingine ya kukabiliana na kuharibu mifumo ya ulinzi wa anga. Na hapo ugumu wa kuzishambulia hizo ndege unazidi kuongezeka.

Kuhusu Uturuki kinachohofiwa zaidi ni jinsi gani hiyo mifumo ya S-400 itajumuishwa ili ifanye kazi pamoja kitu ambacho hakitokwenda sambamba na mifumo ya ulinzi wa anga ya NATO iliyopo ambapo Uturuki ni mwanachama wake.

Je Uturuki watawezaje kuiendesha mifumo hiyo Separately bila kuleta matatizo ya kiusalama?

Kumbuka hata Urusi pia imekuwa ikisita kuzikabidhi zile S-300 moja kwa moja kwa mshirika wake, Syria aziendeshe sababu moja ni kuhusiana na maswala kama hayo ya kiusalama ikumbukwe kuwa Syria ilishawahi kuitungua ndege ya Urusi kimakosa na mifumo kama hiyo.
Sjaelewa ata kidogo
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom