Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,393
Kifungu cha sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 kinaruhusu mke kukopa vitu ambavyo mumewe atakuja kuvilipa ilimradi tu vitu hivyo viwe ni muhimu kwa maisha ya familia. Hali inaweza kuwa tofauti kama mke akikopa dhahabu, manukato na nguo za kujipamba au pia kama angekopa vitu vya thamani kubwa kuliko ambavyo mumewe anaweza kuvilipa au vitu vingine ambavyo sio muhimu kwa ajili ya maisha yake na ya familia. Sheria hii inawabana zaidi wale wanaume wanaosafiri kwa muda mrefu huku wakiwa hawajaacha fedha za matumizi zinazokidhi mahitaji ya hapo nyumbani kwa kipindi chote watakachokuwa wako safarini. Au wale wanaotelekeza familia zao kwa muda mrefu bila kujulikana walipo na pale wanaporejea na kukutana na deni baada ya wake zao kukopa, wanakuwa hawana budi kulilipa, kwani sheria inawabana.
Hata hivyo kifungu hicho kimetoa tetezi mbalimbali ambazo mume anaweza kuzitumia ili kumuepusha na wajibu wa kulipa deni hilo. Mume anaweza kuepuka kulipa deni kama tu angekuwa ameshaachana na na mkewe au akiweza kuthibitisha kuwa mkewe anaishi maisha ya waziwazi ya uzinzi. Mfano, kama mume akithibitisha kuwa mkewe anatembea na huyo mwenye duka alipokopa na mtaa mzima unafahamu juu ya hilo, basi hatowajibika kulipa deni hilo. Pia kama akithibitisha kwamba alimpatia mkewe fedha za kutosha kukidhi mahitaji kwa kipindi chote alichokuwa amesafiri au kulikuwa na bidhaa za kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake au kama bidhaa zilizochukuliwa ni nyingi kuzidi uwezo wake wa kulipa, na hapa kiasi cha bidhaa kinaweza kuthibitishwa kwa rekodi aliyokuwa anaiweka mmiliki wa duka kwa bidhaa alizokuwa anamkopesha huyo mke mkopaji.
Sheria hii ni muhimu sana kwa sababu, inalinda familia kutoka kwa mume asiyetaka kutimiza majukumu yake ya kifamilia. Lakini mapungufu katika sheria hii ni kuwa imelalia upande mmoja kwa sababu, haimpi mwanaume uwezo wa kukopa pale mwanamke anapokataa kutimiza majukumu yake ya kifamilia. Labda itaonekana ni jambo la kuchekesha kidogo kwa wasomaji wa JF, lakini sheria hii hii ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 katika kifungu cha 63 (b) inampa haki mwanaume kulelewa na mkewe (maintenance) pale anapokuwa hana uwezo wa kuitunza familia kutokana na mapungufu kimwili, kiakili, au inapothibitika kuwa afya yake ni ya mgogoro na inapothibitika kuwa mkewe ana uwezo wa kutunza familia hiyo. Sasa inakuwaje pale mwanamke huyo anapokwepa wajibu wake huo?
Naomba Mods wasiipeleke hii thread kule jukwaa la sheria kwa sababu inawahusu wanandoa na ndio maana nikaiweka hapa MMU kwa faida ya wengi.