Kumbe sare za traffic mtaji, sare za ffu mkosi?!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe sare za traffic mtaji, sare za ffu mkosi?!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by domokaya, Nov 10, 2011.

 1. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,155
  Likes Received: 1,277
  Trophy Points: 280
  Askari wa usalama barabarani wamepewa madaraka makubwa kuliko uwezo wa ufikiri wao na elimu yao. Askari usalama barabarani ana mamlaka ya kukusimamisha, kukupa makosa na pia kukuadhibu. Hawa vijana wetu waliowe ngi form four ile ya mwisho na wengine wanatumia majina ya ndugu zao kweli wana uwezo wa kutoa maamuzi ya kisheria? Pia hawa wana uwezo na ustahamilivu endapo anayemtuhumu atamuambia kuwa hakubaliani na anachokiamua? Uzoefu unaonesha kuwa dereva asiyetaka kutoa rushwa lakini yupo tayari kulipa faini badala ya kuwa na kosa moja alilokamatiwa anarundikiwa makosa mengine ambayo hayana kichwa wala miguu.

  Nimekutana na dereva mmoja anabishana na Dada trafic police kituo cha police Buguruni. Traffic amempa kosa la kutosimama alipomuelekeza badala yake jamaa kasimama hatua kumi mbele. Dereva anadai alipomuelekeza hapakuwa panafaa kupaki. Askari wa Usalama anadai ni lazima kusimama papo hapo pindi askri anapokuamuru kufanya hivyo. Katika majibizano baina ya mwanadada huyo usalama na kijana huyo, kijana akasema hata akimpa makosa mangapi atalipa kuliko kumpa rushwa na atahakikisha rushwa aliyompa siku za nyuma itamtokea puani. Akaapa kuhakikisha anamtia mkosi mpaka apewe sare za FFU na anyanga'nywe mtaji alio nao sasa, sare za Traffic. Ndipo nilipotambua kuwa sare za FFU mkosi na zile za Traffic Mtaji.


  Mpaka sasa kuna malalamiko kadhaa ya askari wa usalama barabarani kusababisha ajali kwa maamuzi yao yasiyokuwa na weledi. Kuna umuhimu wa kubadili namna askari wetu wa usalama wa barabarani kushughulikia wakosaji na wavunjaji wa sheria. Utaratibu uliopo sasa unawafanya askari hawa kuwa wafanyabiashara wa makosa ya barabarani badala ya kuwa wanausalama barabarani.

   
Loading...