Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,332
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.
Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.
Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.
Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya
Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari
Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.
Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.
Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.
RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.
Paskali
Kuna kitu Uongo ktk taarifa hizo. Hainijii akilini zimepita siku kazaa ndio mseme, Ina maana madokta walikuwa wanachunguza maiti ndipo wajue ugonjwa uliomuua¡!!!!!!!!!