Kumbe rais wetu nchi nyingine anagombewa?

kachumbari

Senior Member
Nov 1, 2010
125
8
Angalia hapa!

Final_letter_to_Kikwete-2011-03-04.jpg
 
It doesn't matter anagombaniwa na nani huko nje. Jukumu lake ni kwa wapiga kura wake na historia itamhukumu kwa aliyowafanyia Watanzania na si watu wa nje.
 
Halafu wengine ohhhh, anasafiri sana nje. Mlifikiri anaenda cheza Disco huko?

Huyo ndio JK "action speaks louder than words".
 
Kwa barua hiyo ni nani anayemgombea? Hii barua imetamka wapi kwamba anatakiwa aende kutawala nchi nyingine? Mtu anapokuandikia barua kukupa taarifa fulani na kushukuru kwa ushirikiano wako katika jambo fulani anakugombea? Huoni kwamba hata watu walioandika barua hawajiamini hadi wakasaini watu wanne? Umetumwa kumfagilia? Hizo ni propaganda zisizo na kichwa wala miguu.
 
kwa barua hiyo ni nani anayemgombea? Hii barua imetamka wapi kwamba anatakiwa aende kutawala nchi nyingine? Mtu anapokuandikia barua kushukuru kwa ushirikiano wako katika jambo fulani anakugombea? Umetumwa kumfagilia? Hizo ni propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

maralia haikubaliki..!
 
siku zote mtu mjinga msifie hapo utafurahia ujinga wake,mkwere wanamkebehi nayeye anapata biiichwaaaaa
 
Kwa barua hiyo ni nani anayemgombea? Hii barua imetamka wapi kwamba anatakiwa aende kutawala nchi nyingine? Mtu anapokuandikia barua kukupa taarifa fulani na kushukuru kwa ushirikiano wako katika jambo fulani anakugombea? Huoni kwamba hata watu walioandika barua hawajiamini hadi wakasaini watu wanne? Umetumwa kumfagilia? Hizo ni propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

Hivi ule msemo wa nabii hakubaliki kwao tumeusahau?? Huyo ndiyo JK mazee.
Napita tu fasta lakini wakuu.
 
Nafiri huko anakogombewa wanadhani TZ ni peponi ingekuwa inaruhusiwa wangempa wiki mbili tu awaongoze ndo wangejua JK ni nani.Zingeshuka EPA MEREMETA DEEP GREEN DOWANS RICHMOND za kutosha mkataba wake wa wiki mbili unapoisha angeulizwa kulikoni angekuna kichwa kisha angetabasamu na kujibu ENHEE HATA MI SIJUI.
 
Wanaojua diplomasia, that letter is a diplomatic way ya kumkumbusha nini anachopaswa kufanya na siyo kumsifia!
 
Hivi ule msemo wa nabii hakubaliki kwao tumeusahau?? Huyo ndiyo JK mazee.
Napita tu fasta lakini wakuu.

Ule msemo? Wa kisukuma, kikwere au wa wapi? Acha kudandia mambo usiyoyajua. Maneno mazito hayo; siyo ya kufanyia mchezo na siasa zenu za maji taka.
 
Mataifa ya nje hayawezi kumponda JK hata siku moja. Watamsifia sana coz they know what they get from him. Thats why u c wanampa heshima sana huko majuu, wanafahamu wanachokipata kutoka kwake. They know anahitaji ujiko so wanampa wa kumwaga then wakihitaji wanachotaka hajiulizi mara 2. They say ktk Africa nzima JK ndiye rahisi anayependwa mamtoni kuliko maraisi wengine wote coz si mchoyo.......
 
Ule msemo? Wa kisukuma, kikwere au wa wapi? Acha kudandia mambo usiyoyajua. Maneno mazito hayo; siyo ya kufanyia mchezo na siasa zenu za maji taka.

Mdudu,
Usiwe na jazba, punguza munkari,, wewe ukisema cha nini wengine wanajiuliza watakipata lini. Utatukana sana, utamaliza vituko lakini ukweli utabaki palepale tu. Huyo ndiyo JK kaka utakufa bure kwa vijiba vya roho.
 
wote mnaotumia hiyo barua kumpigia debe JK ichukueni muipeleke kule malampaka shinyanga ambako watoto hawana hat viatu vya kuendea shule,au lakitatu ambako wananchi wanakufa kwa njaa,au gongo la mboto walikolipukiwa na mabomu kwa uzembe
 
Back
Top Bottom