Kumbe penny anatembea na kigogo wa ccm?

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
230
237
Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya Naseeb Abdull 'Diamond' na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Penny! Swahilitz inakupa full details

Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba fedha anazo.

Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo huyo kula vya watu

367b0ca45d1a11e38dc912e5acb4b5c7_8.jpg


"Amini kwamba katika kipindi chote cha mahusiano yao, Diamond hajawahi kusalimiana na mama yake Penny hata siku moja, hata kaka zake Penny hawataki kabisa kumsikia Diamond na mara kibao wamekuwa wakimsema sana Penny kuhusu Diamond" kimesema chanzo chetu

Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya kuishi na Diamond

"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye aliyemshinikiza kwenda kuzika"

"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?
"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho

dia1.jpg

Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa akiishi na Wema.

"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.

"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"
Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!" kilisema chanzo hicho

"Kimsingi huyo kigogo niliyewatajia ndiye anahudumia Penny , fanyeni utafiti mtagundua" kilimaliza chanzo hicho.


source: Mtandoa wa Vijana.


 
Kweli kwa mtazmo huu, Diamond ni king'asti tu maana hata kwa Wema nako alikuwa akisaidiwa na kigogo wa ikulu, huku kwa Penny nako Kigogo wa CCM.

Hata huko kwa Wema watamsaidia tu kutunza,

Anahitaji kukua na kuwa mwanaume, sio kupigapiga vipicha tu..... Mwanamke anahitaji matunzo, na akafundwe jinsi ya kuhandle mwanamke
 
Ha ha ha kigogo wa ccm aweza kuwa Savimbi

Yeye mwenyewe si kaimba Kuchapiwa siri ya ndani? He he he ! Labda alikwisha jua wazee wa " kidumu chama T...." Wanajipumzisha mitaa ya kwake. Chezea kijani na njano wewe!
 
Back
Top Bottom