Mallaba
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 2,554
- 48
Nilikuwa Jijini Mwanza kwa siku kadhaa na niliyojionea sio siri ni mazito sana hata kusema,maana mengine nilikuwa ninasikia tu humu ooh wizi wa kura,ooh uchakachuaji,na mda mwingine nilijua tu kuwa huu umehakuwa ni wimbo wa Taifa,lakini nilivyojionea na kutazama kuna kila hali ya kuonyesha kuwa wizi umefanyika maeneo yote si wabunge,maraisi au udiwani.
Jimbo la Nyamagana matokeo yalijulikana mapema tu kuwa Waziri ameshindwa hivyo matokeo yakakatazwa kutangazwa kutoka kwa mkuu wetu,hata hivyo wananchi waliendelea kuandamana kuomba matokeo yatangazwe hadi Kikwete akaenda Mwanza na kilichofanyika ilikuwa ni kumuomba Wenje akili kushindwa ili aandaliwe nafasi maalum yeyote serikalini lakini yeye alikataa,hapo ndio wananchi walipoanza vurugu za kuchoma ofisi ya CCM na magari ya vigogo (mashangingi) na kufunga barabara zote zinazoelekea jimboni huko na kila mtu aliyepita pale mwenye VX kama asipoonyesha alama ya Chadema aiambiwa aidha gari ichomwe au atoke aiache gari palepale.
jAMANI HALI ILIKUWA NI MBAYA basi ndio mwisho matokeo wakayatangaza baada ya kuona SUTI YA UMMA haivumiliki tena.
Mambo hayo pia yametokea Jimbo la Magu ,maana ukweli ni kwamba Chadema kupitia mgombea wake NGONGOSEKE alimshinda Limbu ,ila taarifa zilipomfikia Mkwere akasema haiwezekani ,yaani Chadema wamechukua Nyamagana na Ilemela(majimbo yote mhimu sana ya Mwanza) bado tena wachukue na hili la Magu,hapa ni Lazima CCM itangazwe imeshinda .Kwa hiyo maamuzi yanaonekana yalikuwa yanatoka ngazi za juu kabisa,ndio maaana matokeo yalikuwa yanacheleweshwa sana,maana yakiripotiwa kwa NEC ,Nec inayapeleka kwa Mkwere kama aki-approve basi ndio ynatangazwa na kama yakikataliwa basi huyo mgombea anashindwa hata kama awananchi wote walimpigia kura.
Hii inaweza ikatudhihirishia kuwa hata hayo majimbo Chadema waliyochukua bila kuwa na nguvu ya umma basi wala wasingeshinda.Je ni majimbo mangapi yaliyofanyiwa mchezo kama huo?
I think we still have a long journey to go