Kumbe ni kweli bila siasa uwezi kutoka kimaisha mbona hawa walikimbilia siasa ile hali niwasomi wa juu

Umemsahau Professor Jay.Nae si Professor, kaamua kukimbilia mbugani na professional yake.
 
Pesa haziwezi kukupa furaha ya maisha. Watu tunasoma na kufanya vitu kwa passion. Passion yangu siyo kulaghai wananchi kwa kuwapa matumaini ili ushirikiane nao katika harakati za kutafuta maendeleo halafu unaishia kuwaacha njia panda.
 
Malengo makuu ya elimu ni matatu
1.kusaidia jamii yako.
2.kuendeleza somo ulilosomea
3.kujisaidia mwenyewe binafsi.

Sasa kwa wasomi wetu wanapenda zaidi kujisaidia wao wenyewe katika kujikwamua katika umaskin,ten bahati mbaya zaidi ile elimu yao hawaitumii kabisa katika mambo yao hata siasa.Angalau wachungaji na mapadre waliosoma elimu ya kawaida wanawasaidia wahumini wao kwa kuchanganya iman na elimu ya kawaida.

Katika kuendeleza masomo waliosomea ndo kabisaa huko hakuna kitu wanachofanya.Inshu ya kuisaidia jamii ni 30% na 70%ni kujisaidia wao wenyewe.

Wasomi tubadilishe mitazamo yetu lasivyo tutabaki kuwa nyuma milele huku tukilaumu kuwa weusi wanabaguliwa wakati ulaya na America wanablack wengi ni maprof.na wahadhiri kibao.
 
Back
Top Bottom