Kumbe ni Chato local airport na si international kama wanasiasa wanavyotuaminisha

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Baada ya kufuatilia kwa kina ninakagundua kuna upotishaji mkubwa wa lengo la kumchonganisha rais na wananchi wasio na uelewa,
Uwanja wa Chato ni local airport, ambao pamoja na vipimo vya makadirio utakuwa kama Ile wa bukoba, na haufiki viwango vya mwanza au KIA au JKNIA ,
Ila wanasiasa wameshupalia jambo ili na kuwapotosha wananchi juu ya uwanja uo kwamba ni international airport,

Sababu zinazoonesha kwamba haitakuwa international airport ni kulingana na takwimu za makadirio walizotoa , ukiangalia takwimu hizi ni sawa na za uwanja wa bukoba, moshi na mtwara,

Length surface/urefu wake
Ni Mita 1,385 ambazo ni futi 4,544

Wasafiri kwa mwaka wanaotegemewa 25,943
Aircraft movements/kutua na kuondoka kwa ndege 1,946
Cargo (kg) / mizigo ni 6,851
Chanzo ni TAA TCAA


Uthibitisho wa pili kwamba CHATO haitakuwa international airport ni

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".
Lakini bado utakuwa category ya local airports



Tenda kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa CHATO local airport ilikuwa hivi

Uwanja unajengwa mkoani Geita Namba ya tenda ni 93696
Mwisho wa maombi ya tenda 3rd Sep 2017.

Maelezo ya Tenda

United Republic of TanzaniaSummary

Construction of New Chato Airport in Geita Region

TOT Ref No7993696

DOCUMENT REF. NO.Click Here To Register

CompetitionNCB

Financier Self Financed

Deadline3rd Sep 2017

Maelekezo hayo juu yanaonesha kwamba taratibu zote zimefuatwa,


Umuhimu wa kujenga uwanja huu ni kulingana na uhutaji wa huduma hii maeneo hayo
Wanachato wamekuwa wahanga wa kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata viwanja vya ndege kuliko maeneo mengine,

Wana chato na Geita wengi hutumia sana sana viwanja vya Bukoba na Mwanza ambavyo umbali wake kutoka CHATO ni kama ilivyoainishwa

131 km mpaka Mwanza Airport (MWZ / HTMW)

145 km mpaka Bukoba Airport (BKZ / HTBU)

Licha ya hivyo ufuatao ni umbali wa kutoka CHATO kwenda viwanja mbali mbali vya kimataifa, ambavyo viko karibu yake

131 km mpaka Mwanza Airport

196 km mpaka Kigali International Airport

282 km mpaka Bujumbura International Airport

308 km mpaka Entebbe International Airport

Pia tuangazie umbali wa CHATO na viwanja vinginevyo vya kawaida nchini na nje ya nchi

145 km mpaka Bukoba Airport

301 km mpaka Goma Airport

318 km mpaka Kamembe Airport


viwanja vingine karibu na Chato, Tanzania

196 km mpaka Kigali International Airport

221 km mpaka Shinyanga / Ibadakuli Airport

225 km mpaka Butare Airport

259 km mpaka Musoma Airport

265 km mpaka Mbarara Airport

269 km mpaka Ruhengeri Airport

282 km mpaka Bujumbura International Airport

296 km mpaka Tabora Airport

298 km mpaka Gisenyi Airport

301 km to Goma International Airport

Sababu hizo zinatosha kabisa kuwapa CHATO sifa ya kuwa na local airport,
Maana katika viwanja vyote hakuna kiwanja kilicho ndani ya km 120
Kama ambavyo inapaswa kuwa ,kuanzisha kiwanja cha ndege unaweza kuweka popote Ile wataalamu wa uchumi wanashauri angalau viwanja vya kimataifa viwe na tofauti wa umbali wa km 120 ,lakin pamoja na hiyo bado CHATO so international airport ni local airport,


Hivyo basi tufunge mjadala wa CHATO local airport tuangalie mambo mengine,

Britanicca cc Pascal Mayalla Shark cocochanel Mzito Kabwela
 
Baada ya kufuatilia kwa kina ninakagundua kuna upotishaji mkubwa wa lengo la kumchonganisha rais na wananchi wasio na uelewa,
Uwanja wa CHATO ni local international airport, ambao pamoja na vipimo vya makadirio utakuwa kama Ile wa bukoba, na haufiki viwango vya mwanza au KIA au JKNIA .......,

[/USER]
Local International airport ndio nini Britanicca?
 
Haya msemaji subiria maswali ,kwanini isiwe Geita penye population kubwa,ni mkoa,pana wawekezaji,ni katikati Kwa vijiji vingi.Ni swali tu lenye nia ya kujua na si ushabiki.
Labda huko ulipopataja pako ndani ya 120km kutoka eapoti ya karibu. (Naamini watasema hivyo)
 
Back
Top Bottom