Kumbe NHC ni CCM?

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Leo katika habari ITV nimemuona bwana mmoja akizungumzia mikakati ya shirika la nyumba la taifa NHC, nilishangaa aliposema shirika lake linafanya hayo linayoyafanya ili kutekeleza ilani ya CCM, kana kwamba hiyo haitoshi akasema eti hawataki ifikapo 2015, wawe ni kati ya watakaokuwa wamesababisha serikali iliyoko madarakani ishindwe kufikia malengo yake. Hapo ndo nikaanza kujiuliza hilo swali hapo juu.
 
Si ni shirika la umma na CCM ndio chama tawala. Ndio maana inatekeleza ilani ya chama tawala. Hata kama chama kingine kingekua madarakani wao wangetekeleza ilani ya hicho chama. Ndio maana akasema hivyo.
 
Si ni shirika la umma na CCM ndio chama tawala. Ndio maana inatekeleza ilani ya chama tawala. Hata kama chama kingine kingekua madarakani wao wangetekeleza ilani ya hicho chama. Ndio maana akasema hivyo.

Kazi yake ni kuhakikisha shirika linafanya kazi ki biashara ili likue na kuongeza tija and eyeing for 2015 elections bana, correct me if am wrong.
 
Ina maana ulikuwa haujui????????????????????????????????? Wale magamba siyo mchezo Best.
 
Shirika lolote la umma duniani linatelekeza ilani za chama tawala
 
Shirika lolote la umma duniani linatelekeza ilani za chama tawala
Kimaadili ya kitaaluma (professional ethics) viongozi wa idara za serikali na mashirika ya umma wao ni watendaji (technocrats). Hata kama wanatekeleza ahadi/ilani/sera za chama kilicho madarakani hawapaswi kutoa matamshi ya kisiasa. Wao wanapaswa kutumia taaluma zao kufanya yale ambayo wanaamini yataleta matokeo yanayotarajiwa kitaaluma. Ni matokeo hayo ambayo wanasiasa wanayatumia kujigamba kisiasa. Kwa hiyo huyo mtu wa NHC hakupaswa kutoa matamshi ya kukiunga mkono CCM. Lakini waTZ wengi hasa wenye umri uliosonga wana mgando wa mawazo au ufinyu wa uelewa wa demokrasia ya kweli. Kwa mtazamo wao CCM ikitoka madarakani hakutakuwa na serikali.
 
NHC siyo CCM hata kidogo, ila kwa sasa inaendeshwa kwa kufuata sera na iran ya chama tawala ambacho ni CCM
 
Maswali mengine tuwe tunafikiri kabla ya kuuliza. Taasisi yeyote ya umma hulazimika kutekeleza sera za chama kilichopo madarakani,na wakurugenzi na viongozi wote wa mashirika na taasisi za umma huelezwa hilo na wizara zao husika mapema katika miongozo na ma dokezo mbalimbali wanayopewa. Wala halihitaji elimu ya chuo kikuu kujua hilo!. Ndio maana ili utekeleze sera zako, hata ziwe nzuri vipi,cha kwanza jitahd unyakue madaraka ya nchi!.
 
Huyu nehemiah mchechu nadhani anapokwenda hapajui!he is still young!anahitaji kufanya kazi na sio kutwambia mambo ya manifesto ya chama!soo after election kinachofuata ni kazi!habari zake hata yeye sio nzuri tangu akiwa citi-scbl-cba t ltd na sasa nhc!awe mpole sana na afanye kazi, kama kuna mtu anamjua humu jamvini ampe salam, binafsi nimefanya nae kazi naye ni gamba la kutupwa!!!!!!
 
Hata akiwa chama gani,kama anaweza ku accomplish one among primary objective ya shirika analoliongoza-KUKUSANYA MADENI TOKA KWA WADAIWA SUGU-analiongoza shirika vizuri. Secondary objective baada ya kupata mapato ya shirika yaliyokuwa mikononi mwa watu, itakuwa ni kujenga nyumba mpya na kukarabati zilizopo. Tatizo mchapa kazi yeyote akitokea nchi hii huwa kuna tabia ya wale walioumizwa na uchapakazi wake kum discourage na kumpakazia ili kumpunguza nguvu!. Hatutofika tukiwa na tabia hizi. Acheni!.
 
Back
Top Bottom