Kumbe mwenge unakimbizwa na huwa unatengewa bajeti na haujawahi tungiwa sheria!!

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Wakihutubia mkutano kwa pamoja Tundu Lisu,John Mnyika, na Godbless Lema (Singida mjini jana), walisema kuwalazimisha watu kuchangia mwenge ni dhuruma iliyopitiliza kwani mwenge kila mwaka unawekewa bajeti yake.

Vilevile, Tundu lissu amesema tangu uanze kukimbizwa baada ya Tanganyika kupata Uhuru haujawahi kutungiwa sheria yoyote ile.

Kwa hiyo Tundu lissu akasema mwananchi ukichangia ni mapenzi yako tu kwani usipochanga utakuwa hujavunja sheria yoyote ile.

Akaongeza,fungu linalotengwa kwa ajili ya kukimbiza mwenge ni kodi za wananchi hata msipochanga utakimbizwa tu.

Alipopanda Lema,likapita gari linatangaza kuwepo kwa mwenge leo Singida mjini, lema akasema kwa nguvu HATUJI,akafafanua,mwenge unatumia milioni kama Sita kwa kufungua mradi wa milioni mbili kama ya TASAF.

Mwenge ulianzishwa ili palipo na dhuruma pawe na Amani, lakini mwenge miaka hamsini unakimbizwa na dhuruma imezidi tena kupitia hata mwenge wenyewe, alisema Mnyika. Mwisho wa kunukuuu.
 
Labda maana kizazi cha leo ni ngumu kujua mwenge huu, labda CCM wanajua hili.
 
IIngekuwa tuna Vipaumbele vya Taifa plus TUNU za Taifa kwa Watanzania... Ujumbe wa Mbio za Mwenge pengine zingekuwa na mashiko kwani Wanafunzi wangekuwa wanalishwa uzalendo ambayo ni muhimu sana kwa uhai wa Taifa letu... Sasa hivi Maudhui sijui nini? maana kila kitu ni hovyo.... Mabepari waliokuwa wanalia sasa hivi wanasherehekea! Misamaha ya kodi inawahusu wao! wananchi wanakilimbitwa mbele nyuma ... maisha yanazidi kuwa magumu wakikolezea na wizi mkubwa TANESCO ...
 
Hivi kweli baada ya miaka 50 ya Uhuru bado tu tunaendeleza propaganda za Kikomunist................ CCM wakubali tu yaishe kama Azimio la Arusha. Propaganda kama hizo zishpitwa na wakati. Hata Cuba na North Korea hawafanyi hivyo. Watafute mbinu nyingine za kuwaunganisha Wananchi na kuleta Umoja lakini siyo kupitia Mwenge!!
 
Hivi kweli baada ya miaka 50 ya Uhuru bado tu tunaendeleza propaganda za Kikomunist................ CCM wakubali tu yaishe kama Azimio la Arusha. Propaganda kama hizo zishpitwa na wakati. Hata Cuba na North Korea hawafanyi hivyo. Watafute mbinu nyingine za kuwaunganisha Wananchi na kuleta Umoja lakini siyo kupitia Mwenge!!

Kweli kabisa mkuu. ningekuwa raisi wa nchi hii, pesa ya mwenge ningepeleka hospitali ikanunue vifaa vya kujifungulia akina mama.
 
Watendaji wote nchini chini ya wakuu wa wilaya,huwekewa lengo la kukusanya fedha za mwenge ncgi nzima, kumbe bajeti huwa inatengwa na serikali sasa:
1. Fungu la bajeti huwa linaenda wapi?
2. Zile ambazo huwa zinachangishwa kwa wafanyabiashara nazo huenda wapi?
Aisee wizi huu,hata shetani anatushangaa sana!
 
Huu mwenge umesaidia sana kuleta majanga haya:
  1. Kuharibu mazingira kwa moshi wake na wa magari yake
  2. Kueneza UKIMWI
  3. Kuzalisha watoto wengi wa nje ya ndoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom