Kumbe mwanamke huwa anaboreka akipendwa sana?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Nimeshangaa sana hili, Jana katika kupiga story za hapa na pale na rafiki yangu mmoja hivi wa kike akanambia yeye alishawahii kumuacha mwanaume kisa huyo mwanaume alimpenda sana kitu ambacho mwanadada alikuwa akiboreka sana.

Ikabidi nimuulize like ni wewe tuu ambaye huwa unaboreka ukipendwa sana au wote! akanambia asilimia 90% ya wanawake wote hapa Duniani huwa wanaboreka sana wakipendwa sana na mwanaume!

Ikabidi nimuulize kwanini wanaboreka kupendwa sana wakati ndio kitu kizuri kwenye mahusiano? Akanambia mwanaume kumpenda sana mwanamke haikatazwii ila mwanaume hatakiwi kuonesha kama amempenda sana huyo mwanamke, mwanamke hatakiwi kujiona kama kapendwa sana, anasema ukimtengenezea mazingira mwanamke wako kuonesha kuwa anaweza kuachwa muda wowote na saa yoyote ile itampa nidhamu mwanamke na kukuheshimu sana! Ila ukionesha bila yeye huwezi kuishi basi kinachofuata ni mwanaume utadeki hadi nyumba.

Akaendelea kusema, mwanaume kumtumia SMS mpenzi wako muda wote like uko wapi unafanya nini,kwanini hujaaga na vitu kama hivyo anadai wanawake wengi wanaboreka ila huwa hawawezi kusema reaction yake wataonesha siku wakipata mwanaume ambae 3/4 haoneshi Care 1/4 anaonesha Care Atang’ang’aniwa huyo mwanaume na hao ndio huwa michepuko.

Anadaii hakutakuwa na maendeleo kwenye hayo mahusiano kwasababu mwanaume akionesha kupenda sana atashindwa kufanya vitu vya kuleta maendeleo akihofia kuachwa na mpenzi wake, like anaogopa kwenda kupanga biashara na mwanamke akihofia mke wake kununa na mwisho wa siku kuachika! Hizi points kadhaa niliweza kudaka jana! Nikaona sio mbaya kushare nanyi hapa

Nyie kwa uzoefu wenu vipi? Tubaki nayo moyoni tuu si ndio?
 
Back
Top Bottom