tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,788
- 4,490
Nakumbuka ni muda mfupi sana toka tufanye Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani na Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano yaano 2015 - 2020.
Tumebakiza muda mfupi sana kumaliza miaka mitano ya awamu ya tano na kufanyika tena kwa uchaguzi mkuu...nakumbuka ule mchakato wa uchukuaji wa fomu za uchaguzi kwa ngazi ya urais pale mgombea wa Chadema alipolisimamisha jiji la Dar kwa dakribani saa 3 mpaka 4 magari hayatembei mitaa yote ya mjini kiasi cha Polisi wa usalama barabarani kuacha mambo yajirekebishe yenyewe.
Toka nimeanza kushiriki katika uchaguzi kwakweli sijawahi kuona mtiti wa watu kama ule na sijui kama itaweza kujirudia tena hali kama ile.
Nakumbuka magezeti yalivyoandika kuhusu ule umati na jinsi Dr Kikwete alivyojibu kuhusu ule umati kuwa ni picha za kutengeneza tu kwa tecknolojia ya kisasa wala hakukuwa na umati mkubwa kama ule na hata mikutano mingine ilikuwa ikionekano mtiti wa watu kwenye magazeti.
Watanzania nawasifu sana kwa kuwa mabalozi wazuri wa amani kwakweli na hakukuwa na matukio yoyote ambayo yalitishia kuvunjika kwa amani wala vifaa vya uchaguzi na watumishi wa Tume ya Uchaguzi.
Ni matumaini yangu hata uchaguzi ujao wa 2020 kutakuwa na amani tele na viongozi watapatikana kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.