Kumbe mume ni Buzi tu!

OMGHAKA

Member
Aug 15, 2011
97
23
Nilikuwa na kazi maalum ofisini kwetu nikapata fursa ya kufanya "utafiti" ambao nilikusanya data zifuatazo:
Ofisi yetu ina wafanyakazi wanawake 42, na wanaume 72
Wanawake walioolewa ni 31, wasio katika ndoa ni 11
Wanaume walio ktk ndoa ni 62 wasio ktk ndoa ni 10 (wote madereva)
Kati ya wanaume 62 waliooa, 49 wameandika wake zao kama "next of kin", 1 ameandika dada yake, 1 ameandika kaka yake na 11 wameandika watoto wao.
Kati ya wanawake 31 walio ktk ndoa, 1 ameandika mumewe kama "next of kin", 3 wameandika dada zao na 27 wameandika watoto wao.
Conclusion: 97% ya wanawake walio katika ndoa huchukulia waume zao kuwa ni mabuzi tu!!
 
Hii kali, lakini ndivyo ilivyo kwani angalia kama umeoa na mke wako anafanya kazi, umewahi sikia kuwa mwezi huu mwanamke atatoa angalau chakula tu. Hata kama anamshahara na anausafiri wa kwenda kazi mume ndio atamjazia mafuta katika gari hilo.
 
Hivi vi-thread ndiyo tunaviitaga havina mashiko. Yaani mtu amekosa wa kupiga naye stori kwahiyo anaona kupost vitu visivyoeleweka ili muda uende.
 
Hahahaah very interesting, wanawake wakishakuwa na watoto nahisi wana wa value zaidi watoto kuliko mmewe. lkn hapo hapo yeye atataka wewe umrithishe kila kitu . Mwanamke ekiwa na nyumba atawaandika wazazi wake na si wewe mmeo!
 
Very interesting! Ngoja na mimi nitaanza kuchungulia files za watu nione na mimi hapa kwetu itakuwaje!
 
mhhhhhhhh! wenyewe watatujibu, tusubiri tuone. Ila kama umeongea ukweli hivi. 'They feel more secure to have their property under the names of their bloody relatives'. Phew!, nadhani nimekosea"
 
Hii kali, lakini ndivyo ilivyo kwani angalia kama umeoa na mke wako anafanya kazi, umewahi sikia kuwa mwezi huu mwanamke atatoa angalau chakula tu. Hata kama anamshahara na anausafiri wa kwenda kazi mume ndio atamjazia mafuta katika gari hilo.

Wewe kijana tafadhali heshimu mama zako na dada zako. Wanaume wangapi wanazo kazi nzuri na hawawaulizi wake zao kwa mahitaji muhimu, na wanaona afadhali wakanufaishe nyumba ndogo ambako huko ndiko wanakoitwa mabuzi? Wanapalilia mikoko wakati minazi inakufa kwa nyasi (unaujua msemo huu?).

Mshahara wa mama ambao ni mdogo ndiyo unaosukuma mwezi.

Nilikuwa na kazi maalum ofisini kwetu nikapata fursa ya kufanya "utafiti" ambao nilikusanya data zifuatazo:
Ofisi yetu ina wafanyakazi wanawake 42, na wanaume 72
Wanawake walioolewa ni 31, wasio katika ndoa ni 11
Wanaume walio ktk ndoa ni 62 wasio ktk ndoa ni 10 (wote madereva)
Kati ya wanaume 62 waliooa, 49 wameandika wake zao kama "next of kin", 1 ameandika dada yake, 1 ameandika kaka yake na 11 wameandika watoto wao.
Kati ya wanawake 31 walio ktk ndoa, 1 ameandika mumewe kama "next of kin", 3 wameandika dada zao na 27 wameandika watoto wao.
Conclusion: 97% ya wanawake walio katika ndoa huchukulia waume zao kuwa ni mabuzi tu!!
mmmh mwajiri akikugundua huna kazi, unaanza kutoa siri za watumishi ???? wewe ni mtu hatari, unaweza kudhani ni kitu kidogo kutoa taarifa hizi lakini zikiwafikia walengwa unaweza kuleta mtafakaruku katika familia, be careful
 
Back
Top Bottom