Kumbe Mji wa Dar inawezekana ukawa ni mzuri

Android 00

JF-Expert Member
May 23, 2013
774
221
Kuanzia jana usiku mmoja tuu baada ya uvunjaji na uondoshaji wa vibanda vya biashara ndogondogo zenye kuleta watu wa aina tofauti mjini wengi wao wakiwa ni majambazi ambao wanaochunguza maduka yanayofanya biashara,wateja jana usiku viliteketezwa na mji umekuwa safi na wenye mandhari ya kuvutia

Nilikua najaribu kujiuliza kila siku Serikali iko likizo? Wanaofanya biashara na walipaji wa kodi wako kwenye usumbufu mkubwa ambao wanaupata kutoka kwenye hawa wasiokuwa rasmi.

Hawa wanaweka meza mbele ya duka kubwa la mfanyabiasha wakielezwa kuondosha wanasema hi sehemu ni barabarani kwaiyo wanaweza kuendelea kufanya biashara na serikali imewaruhusu kwakua mwakani ni uchaguzi wakiwa watasumbuliwa hawatoipigia kura CCM

Maduka wanalipa kodi, leseni, usafi,walinzi, wao wanafanya biashara bila ya kulipia chochote na cha zaidi ni ambacho kinasikitisha ni hichi cha kushirikiana na majambazi

Serikali yetu tunaamini kama watakusudia hawatoshindwa,tuisapmt kwa udhibiti huu na ule wa bodaboda ambao ni wa njia rahis ya kkufanya ujambazi.

Tunaiomba serikali Operesheni hii iwe endelevu sisi wananchi tunahitaji kuishi na kutembea kwa amani.
Hongera Mkuu wa Mkoa wa Dar
Meya wa Mji Dar
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar
 
Hiyo ni sawa, lakini lazima serikali nayo iwajibike kwa hao wenye vibanda kwa kutafutiwa maeneo mbadala. Na kama hawalipi kodi serikali iweke utaratibu walipe kodi. Kuondolewa maeneo yasiyotakiwa kufanya biashara isiwanyime uhalali wao au haki yao ya kujitafutia kwa kigezo cha kuweka mji safi. Pia, ukiangalia kigezo cha kwamb wanashirikiaba na majambazi kwa kuangalia tukio moja au matukio mawili ni kuwakosea mamia ya raia wema.
 
Habari yako haijatimia, hujasema wapi bomoabomoa hiyo imefanyika ili tuweze kuchangia kikamilifu.
 
Bomoabomoa imeanza jana usiku sa9 maeneo ya msimbaz,uhuru hii barabara kubwa ambayo ilikua tayari imeshatekwa na hizi biashara ndogondogo
 
Watendaji wa serikali wahusika wa kusimamia usafi na mpangilio wa jiji huwa wanalala usingizi mpaka hawa machinga wanaweka biashara zao sehemu zisizotakiwa na baadae wanakuwa kama wamezinduka na kuwabugudhi machinga. Hivi kwanini wasiwe wanapatrol na kama wakikuta mtu ameweka biashara yake eneo lisiloruhusiwa atolewe mara moja badala ya kusubiri wamesha ji-establish na kuwatia hasara kama wanavyofanya sasa!!! Ifikie muda tuache kufanya kazi kisiasa zaidi.
 
Unajua Nchi hii ina tabia ya kulea mambo. Kama watu wanatafuta sehemu ya kufanya biashara, mbona machinga Complex imebaki pagale tu wakati watu wanazagaa na biashara barabarani? Kweli tunataka mji usiwe kama ghulio, unakosa hata pa kukanyaga, msongamano, wizi, uchafu sababu ya kutokuwa na udhibiti wa kufanya biashara. Ukiwa na sheria dhaifu, vijana wetu hawawezi kuwa wabunifu, watakachofikilia ni kupanga soksi barabarani, maisha yanaenda lakini kama sheria ni kali watafikiria nje ya box, kama kuunda ushirika, kilimo n.k, sanaa na michezo n.k badala ya kila mtu kung'ang'ania kuupanga bidhaa barabarani.
 
Hilo wanalofanya ni 1 tu yapo mengi sana yanaofanya mji kuwa mchafu na kuwa kichaka cha wahalifu. Ni lazima serikali ya jiji la Dsm lifanye zaidi ya hilo pamoja na kuchukua hatua kali zaidi ya watu wenye maduka wanao panga bidhaa zao nje na gari zinazo paki ktk sehemu za watembea kwa miguu kinacho shangaza vaadhi ya sehemu hizo zinatozwa ushuru
 
Kuanzia jana usiku mmoja tuu baada ya uvunjaji na uondoshaji wa vibanda vya biashara ndogondogo zenye kuleta watu wa aina tofauti mjini wengi wao wakiwa ni majambazi ambao wanaochunguza maduka yanayofanya biashara,wateja jana usiku viliteketezwa na mji umekuwa safi na wenye mandhari ya kuvutia

Nilikua najaribu kujiuliza kila siku Serikali iko likizo? Wanaofanya biashara na walipaji wa kodi wako kwenye usumbufu mkubwa ambao wanaupata kutoka kwenye hawa wasiokuwa rasmi.

Hawa wanaweka meza mbele ya duka kubwa la mfanyabiasha wakielezwa kuondosha wanasema hi sehemu ni barabarani kwaiyo wanaweza kuendelea kufanya biashara na serikali imewaruhusu kwakua mwakani ni uchaguzi wakiwa watasumbuliwa hawatoipigia kura CCM

Maduka wanalipa kodi, leseni, usafi,walinzi, wao wanafanya biashara bila ya kulipia chochote na cha zaidi ni ambacho kinasikitisha ni hichi cha kushirikiana na majambazi

Serikali yetu tunaamini kama watakusudia hawatoshindwa,tuisapmt kwa udhibiti huu na ule wa bodaboda ambao ni wa njia rahis ya kkufanya ujambazi.

Tunaiomba serikali Operesheni hii iwe endelevu sisi wananchi tunahitaji kuishi na kutembea kwa amani.
Hongera Mkuu wa Mkoa wa Dar
Meya wa Mji Dar
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar

Tupiamo vipicha basi nasi tufaudu...!
 
Ni weli mji umekuwa safi, unapitika, hawa wamachinga ndio source kubwa ya uarifu kama ongezeko la uchafu unaotokana na Mazo kama nyanya, vitunguu, ndizi n.k, source ya Ujambazi kwani ni watafiti wazuri wa kutoa ripoti kwa waharifu, ni source ya ukwepaji kodi kwani wachina na wafanyabiashara wenye magodown wanawatumia sana kwa kuwakopesha yaani mali kauli na baada ya kuuza urejesha fedha bila makato yoyote. Ni wahujumu uchumi kwani wengi ndio ubandua mifuniko ya maji ya taka, kichaka cha wezi wa vifaa vya magari, ndio wadhalilishaji wakubwa wa kina mama, ni kichaka cha vijana wadogo ombaomba.
 
Safi sana..!!!, nashauri wafungue akaunti za tigo pesa, m-pesa, na airtel money ili wana-dar tuchangie gharama za kufanya operesheni endelevu ya kuvunja vibanda. Tutachangia kwa hali na mali na jiji letu litapendeza.., hakuna anaependa hii chaos hata kidogo. nasema VUNJAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!
 
Sawa lakini tutaendelea kuwepo no matter what, mmetutia hasara lakini tuta-bounce back, hamna jeuri ya kutunyima riziki na hamtakaa muwe nayo nyie manyan'gau na serikali yenu iliyooza. Huko mitaani kulikojaa uchafu usiozolewa wafanyabiashara ndio wanahusika!? Mngefanya mchana basi nyie si mmejipanga!?
 
Back
Top Bottom