Kumbe Matajiri waliovamia uongozi CCM ni majambazi!

Pole sana ndugu yangu kama hukujua.Wengi tulipoona matajiri wanaingia kwenye siasa tulijua tumekwisha.Tajiri hana ajenda nyingine,ajenda yake ni kuwa tajiri zaidi.Kwahiyo nia kwenye siasa ilikuwa ni kutafuta utajiri.Chochote kilichopo mbele yake yeye ni kukwapua,ndiyo tuliyo yaona na tunayoendelea kuona!Tusipowawekea brakes tumekwisha.

ii Habari baada ya kuisoma nimeona ni vema . Tupige kelele
ili chama cha CCM kiwangalie matajiri wake kwa macho mawili!!

Na siyo tu kukimbilia michango yao mikubwa at the expense of our people being killed!!

Lengo ni kuhamasisha JK na wana CCM wengine kusafisha chama!
Ili konokono watoke! Nia aibu kwa chama kikubwa kama CCM kukubali kupokea majambazi kuwa viongozi wao simply tu kwa TAMAA YA KUCHANGIWA HELA TENA WAKATI WA UCHAGUZI! HILI LISIKALIWE KIMYA WALIJADILI KWENYE KIAKO CHAO CHA JUNI 2006. NIMEANZA KUFARIJIKA KUWA YALIYOSEMWA KUHUSU WABUNGE WALIOGUSHI VYETI WAMEANZA KUFUATILIWA!
LABDA NI WAKATI MUAFAKA HIYO TOPIC IFUFULIWE(ILIKUWA HOT TOPIC BCSTIMES). LEO NIMESIKIA KUWA WATATU TAYARI WAMEHOJIWA NA DCI NA WOTE NI WA CCM.


HABARI KUHUSU TAJIRI JAMBAZI NI HII

Imetolewa mara ya mwisho: 02.06.2006 0947 EAT

•
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya kizimbani akituhumiwa ujambazi

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Mwenyekiti CCM Wilaya atuhumiwa kwa ujambazi 30.05.2006 [Soma]
• Mfanyabiashara wa Arusha kizimbani akidaiwa kutapeli 19.05.2006 [Soma]
• 'War Bus', wenzake wakamatwa Arusha 24.04.2006 [Soma]

*Asomewa mashitaka tisa ya wizi wa magari, silaha
*Ni mfanyabiashara anayemiliki kiwanda cha samaki
*Nako Dar kesi ya Askofu wa Marekani yanguruma

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Bw. Joseph Obeto, amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za ujambazi ikiwamo kukutwa na magari ya wizi, silaha na risasi.

Mwenyekiti huyo alifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, ambapo alisomewa mashitaka tisa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. Kapita Mwaruka, mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka tisa yakiwamo ya kukutwa na magari ya wizi na kughushi hati za magari.

Pia mashitaka mengine aliyosomewa ni kukutwa na risasi kubwa tofauti na bastola aliyokutwa nayo, hivyo kuashiria risasi hizo zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi mengine.

Bw. Obeto ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki magari na kampuni ya KOTRA, alijisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Musoma mwanzoni mwa wiki hii, baada ya Polisi kumtafuta.

Naye Grace Michael, anaripoti kuwa shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya kujipatia zaidi ya dola za Marekani milioni mbili kwa udanganyifu kupitia jina la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Jimmy Julius (45) ameieleza mahakama jinsi watoto yatima na wajane walivyokesha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakisubiri msaada kutoka Marekani.

Ushahidi huo ulitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Bi. Euphemia Mingi. Mshitakiwa katika kesi hiyo ni Askofu wa Kanisa moja la Marekani, Bw. Peter Mutafungwa.

Ilidaiwa kuwa wajane, watoto yatima waliokuwa uwanja wa ndege siku hiyo walikuwa wakisubiri msaada wa tani 360 za chakula, viatu, dawa na dola za Marekani 2,250,000 kutoka kwa mshitakiwa huyo.

Bw. Julius ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Jamii linajishughulisha na kutoa misaada kwa watoto yatima, wajane na wasiojiweza, alidai waliahidiwa kupewa msaada na shirika la Children Pastors International, lililoko Marekani kupitia Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Alidai kuwa baada ya kuambiwa kuna msaada huo walipewa maelekezo na Bi. Angela Chaila ambaye ni Mwandaaji Mipango wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, kuwa wanatakiwa kutafuta kibali cha msamaha wa kodi ili msaada huo uweze kuletwa nchini.

Bw. Julius alidai mahakamani, kuwa walifanikiwa kupata kibali hicho ambacho walipewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya kutuma kibali hicho, Bw. Mutafungwa alidai kimechelewa, hivyo aliwataka wakate tiketi ya ndege kwenda Marekani na kurudi, ili aweze kuleta msaada huo.

Baada ya kupata ujumbe huo, waliamua kwenda kuchukua mkopo katika Benki ya Akiba wa sh. milioni moja na kuwachangisha wajane na watoto yatima sh. 600,050 ambazo walizitumia kwa kukata tiketi ya Bw. Mutafungwa, ambaye alitakiwa kuwasili nchini Septemba 30, mwaka juzi ambapo aliahidi kuwa atalipa gharama hizo baada ya kufika Dar es Salaam.

Alidai kuwa siku hiyo ilipofika, yeye na vikundi mbalimbali vya utamaduni, watoto yatima, wapiga picha na wajane, walikwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Bw. Mutafungwa, ambaye aliwasili saa 6 usiku, na baada ya kumpokea, alisomewa risala na kuchezewa ngoma na waliambulia kukumbatiwa, na hakuwa na kitu chochote alichokuja nacho kama alivyokuwa ameahidi.

Bw. Julius alidai baada ya kumpeleka kwenye nyumba waliyokuwa wamemwandalia, walimwacha apumzike na aliwaomba kuwa fedha hizo angezilipa Oktoba 2, mwaka juzi, lakini hakuweza kufanya hivyo, aliendelea kuwazungusha bila kuwapa misaada kama alivyotakiwa.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka utakuwa na shahidi mwingine.
Tuma kwa Rafiki Nakala inayochapika
 
Habari za Mathayo Musoma ni za kutisha sana .Lakini ni CCM bwana nani wa kusema ?
 
Back
Top Bottom