Kumbe mapailot wengi hawawezi kuendesha ndege za kisasa na inawezekana hii ilichangia ajali ya ndege ya Ethiopia!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ndege za leo zimetengenezwa kwa namna ambayo ni ya kisasa sana kwa kutumia mfumo wa kumpyuta (automation) kiasi cha kwamba inazidi kudhihirika kwamba hili sasa linakuwa tatizo kwa ma-pilot wengi na hata kusababisha ndege kuanguka.

Kimsingi, kwa ndege za siku hizi pilot huwa ana kazi kidogo sana, zaidi kazi yake ni kukaa na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa kwa kuangalia geji zilizopo kwenye chumba ha marubani. Kazi ya pilot inakuja wakati wa kutua na kupaa, kwa dakika chache sana. Wakati wa kupaa, akishaacha ardhi basi anaiweka ndege kwenye auto-pilot kiasi kwamba ndege inajiendesha yenyewe. Ndege tayari inakuwa na program ya wapi inaenda, na direction ya kufuata, hata wapi itakata kona. Kimsingi kuna ndege zinaendeshwa kwa kutumia key board kama ya computer, unachofanya unaingiza data na ndege inafuata, hata kitu kama kukata kona itakapofika mahali fulani. Sehemu chache sana, kwa mfano kukwepa mawingu ya dhoruba, pilot anaweza kuiendesha kabla ya kuirudisha tena kwenye auto-pilot.

Matokeao ni kwamba ma-pilot wengi wamekuwa wanashindwa la kufanya pale ndege inapopatata tatizo au mfumo wa auto-pilot unakuwa na hitilafu. Ni kwamba kuendesha ndege kwa mfumo wa komputer kunawafanya ma-pilot wasiwe na uwezo wa kuendesha ndege au kutojua la kufanya kukitokea tatizo angani.Sasa hili linaonekana kuwa limechangia kuanguka ndege ya Ethiopian Airways ya Boeing 737 Max. Ni wazi kwamba mfumo wa computa wa hizi ndege za Boeing 737-Max una matatizo, lakini kwa pilot makini tatizo la mfumo huu sio la kuangusha ndege.

Mapiloti kadhaa wameripoti kwamba walipata tatizo kama la ndege ya Ethiopian Airways muda mfupi baada ya kupaa walipoiweka ndege kwenye mfumo wa auto pilot. Wanasema baada ya kufanya hivyo ndege iligeuka na kuannza kwenda chini. Lakini wao wanasema walipoona hivyo waliiondoa ndege toka mfumo wa auto-pilot na kuiendesha wenyewe na hivyo kuepuka ajali.

Pilot aliyeendesha ndege ya Indonesia ya Boeing 737-Max kabla haijaanguka, alitoa taarifa kwamba na yeye alikumbana na hilo tatizo la ndege kuanza kuelekea chini baada ya kuiweka kwenye auto-pilot. Alipoona hilo tatizo aliirudisha haraka kwenye manual control na kurekebisha muelekeo wa ndege na kuendelea na safari bila tatizo. Alisema aliliripoti hili tatizo.

Sasa kumbe basi, kuna mapilot ambao mfumo wa auto-pilot ukiwa na tatizo wanashindwa kabisa kuiendesha ndege wenyewe. Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, ma-pilot wetu wa Dreamliner, wana uzoefu wa kutosha wa kuendesha hiyo ndege ya kisasa sana kwenye manual control au nao wamejikita zaidi kwenye kutegemea mfumo wake wa computer na auto-pilot?

Maoni ya pilot mmoja mzoefu na mfumo wa automatic wa ndege za kisasa ni kwamba;

Pilots need to practise their flying technique. If they would always fly autopilot, they would lose the skills to fly. Skills that they need when the autopilot does fail. There are phases of flight where it is better or even required to let the autopilot do its job, but landing is one the things pilot are allowed to and need to be capable of doing themselves.

Ethiopian Airlines pilot 'reported flight control problems before crash'

It has emerged pilots on at least two US flights last year filed safety concerns about the aircraft after its nose tilted suddenly down when they engaged the autopilot.

The pilots’ reports were filed in a database compiled by Nasa and do not publicly reveal the airlines or locations.

On one flight, the co-pilot said the nose pitched downwards and the plane began descending at 1,200-1,500ft per minute before the the captain disconnected the autopilot.

Another pilot complained that Boeing had not explained changes to the plane’s automatic functions, describing the flight manual as “inadequate and almost criminally insufficient”.
 
Ndege za leo zimetengenezwa kwa namna ambayo ni ya kisasa sana kwa kutumia mfumo wa kumpyuta (automation) kiasi cha kwamba inazidi kudhihirika kwamba hili sasa linakuwa tatizo kwa ma-pilot wengi na hata kusababisha ndege kuanguka.

Kimsingi, kwa ndege za siku hizi pilot huwa ana kazi kidogo sana, zaidi kazi yake ni kukaa na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa kwa kuangalia geji zilizopo kwenye chumba ha marubani. Kazi ya pilot inakuja wakati wa kutua na kupaa, kwa dakika chache sana. Wakati wa kupaa, akishaacha ardhi basi anaiweka ndege kwenye auto-pilot kiasi kwamba ndege inajiendesha yenyewe. Ndege tayari inakuwa na program ya wapi inaenda, na direction ya kufuata, hata wapi itakata kona. Kimsingi kuna ndege zinaendeshwa kwa kutumia key board kama ya computer, unachofanya unaingiza data na ndege inafuata, hata kitu kama kukata kona itakapofika mahali fulani. Sehemu chache sana, kwa mfano kukwepa mawingu ya dhoruba, pilot anaweza kuiendesha kabla ya kuirudisha tena kwenye auto-pilot.

Matokeao ni kwamba ma-pilot wengi wamekuwa wanashindwa la kufanya pale ndege inapopatata tatizo au mfumo wa auto-pilot unakuwa na hitilafu. Ni kwamba kuendesha ndege kwa mfumo wa komputer kunawafanya ma-pilot wasiwe na uwezo wa kuendesha ndege au kutojua la kufanya kukitokea tatizo angani.Sasa hili linaonekana kuwa limechangia kuanguka ndege ya Ethiopian Airways ya Boeing 737 Max. Ni wazi kwamba mfumo wa computa wa hizi ndege za Boeing 737-Max una matatizo, lakini kwa pilot makini tatizo la mfumo huu sio la kuangusha ndege.

Mapiloti kadhaa wameripoti kwamba walipata tatizo kama la ndege ya Ethiopian Airways muda mfupi baada ya kupaa walipoiweka ndege kwenye mfumo wa auto pilot. Wanasema baada ya kufanya hivyo ndege iligeuka na kuannza kwenda chini. Lakini wao wanasema walipoona hivyo waliiondoa ndege toka mfumo wa auto-pilot na kuiendesha wenyewe na hivyo kuepuka ajali.

Pilot aliyeendesha ndege ya Indonesia ya Boeing 737-Max kabla haijaanguka, alitoa taarifa kwamba na yeye alikumbana na hilo tatizo la ndege kuanza kuelekea chini baada ya kuiweka kwenye auto-pilot. Alipoona hilo tatizo aliirudisha haraka kwenye manual control na kurekebisha muelekeo wa ndege na kuendelea na safari bila tatizo. Alisema aliliripoti hili tatizo.

Sasa kumbe basi, kuna mapilot ambao mfumo wa auto-pilot ukiwa na tatizo wanashindwa kabisa kuiendesha ndege wenyewe. Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, ma-pilot wetu wa Dreamliner, wana uzoefu wa kutosha wa kuendesha hiyo ndege ya kisasa sana kwenye manual control au nao wamejikita zaidi kwenye kutegemea mfumo wake wa computer na auto-pilot?

Ethiopian Airlines pilot 'reported flight control problems before crash'

It has emerged pilots on at least two US flights last year filed safety concerns about the aircraft after its nose tilted suddenly down when they engaged the autopilot.

The pilots’ reports were filed in a database compiled by Nasa and do not publicly reveal the airlines or locations.

On one flight, the co-pilot said the nose pitched downwards and the plane began descending at 1,200-1,500ft per minute before the the captain disconnected the autopilot.

Another pilot complained that Boeing had not explained changes to the plane’s automatic functions, describing the flight manual as “inadequate and almost criminally insufficient”.
Mkuu umeandika kana kwamba umeshaona report ya kilichosababisha ajali.Usiwahukumu pilots kwamba hawakua na uwezo, inawezekana kulikua na hitilafu nyingine.

Siumesikia pia kuwa hata system ya anti- stall kwenye hizi 737 ilikua na mapungufu?
 
Sio ndege zote. 737max imewekewa sensor ambayo ikisense kuwa ndege inaangalia juu zaidi,inajiweka kwenye automatic ili kuweka pua ya ndenge ikae sawa,matokeo yake pua ya ndege inaendelea kuangalia chini,na Pilot anakuwa hana la kufanya wanajikuta wanacrash.
 
Boeing tatizo lao walitaka kuijibi A320 Neo. Ndo wakajikuta wanakuja na B737 max 8,max9.Ambayo ipo very automatised na kuifanya pua iende chini pale ndege inapohisi kuna stalling. Kosa lao hawakuwafundisha mapilot. Wameishia kuwapa manual tu. Maana wanajua kufundisha ni gharama kubwa sana hivyo wakaona watapoteza wateja. Tatizo ushindani wa biashara kati ya Boeing na Airbus ndo unatufikisha hapa.
 
Mm pia Nina wasiwasi na hilo la ma-pailoti kukosa ujuzi wa kutosha kuendesha hizo ndege hasa kwa kua ni toleo jipya.. Ila hiyo autopilot nayo ichunguzwe hapo ndio kwenye shida kubwa.
 
Mkuu umeandika kana kwamba umeshaona report ya kilichosababisha ajali.Usiwahukumu pilots kwamba hawakua na uwezo, inawezekana kulikua na hitilafu nyingine.

Siumesikia pia kuwa hata system ya anti- stall kwenye hizi 737 ilikua na mapungufu?
Bado unarudi pale pale.Hata system ya anti-stall ni sehemu ya automation. NI kwamba ndege ikipungua sana spidi hiyo system inageuza pua kuielekeza chini ili i-gain spidi, lakini hili lnawezekana tayari ndege ikiwa juu sana. Kwa Ethiopian Airways hakukuwa na altitude ya kutosha.

Ona kwamba zaidi ya mapailot wanne wa Boeing 737 Max wamesema walipata tatizo kama lililoangusha ndege ya Ethiopia na Indonesia. Wanasema walipopata hilo tatizo walichofanya ni kuitoa tu ndege kwenye mfumo wa autopilot wakati wa kupaa. Hata pilot wa ile ndege ya Indonesia ambaye aliendeha ndege safari ya kabla haijaanguka alisema alipata tatizo lile lile lakini akaamua kuitoa ndege kwenye autopilot. Kwa hiyo ripoti ya ajali inaweza kusema kweli operating system ya Boeing 737 Max ina tatizo kubwa- lakini suala ni kwamba, kwa nini pilots walishindwa kufanya kile walichofanya wenzao? Hilo halihitaji upelelezi.
 
Sio ndege zote. 737max imewekewa sensor ambayo ikisense kuwa ndege inaangalia juu zaidi,inajiweka kwenye automatic ili kuweka pua ya ndenge ikae sawa,matokeo yake pua ya ndege inaendelea kuangalia chini,na Pilot anakuwa hana la kufanya wanajikuta wanacrash.
Na bahati mbaya kurecover stall in low altitudes ni muujiza.

Na ndicho nilichosema hapo juu kuwa tusiwahukumu pilots ilihali anti-stall system ina failure issues...
 
Bado unarudi pale pale.Hata system ya anti-stall ni sehemu ya automation. NI kwamba ndege ikipungua sana spidi hiyo system inageuza pua kuielekeza chini ili i-gain spidi, lakini hili lnawezekana tayari ndege ikiwa juu sana. Kwa Ethiopian Airways hakukuwa na altitude ya kutosha.

Ona kwamba zaidi ya mapailot wanne wa Boeing 737 Max wamesema walipata tatizo kama lililoangusha ndege ya Ethiopia na Indonesia. Wanasema walipopata hilo tatizo walichofanya ni kuitoa tu ndege kwenye mfumo wa autopilotwakati wa kupaa. Hata pilot wa ile ndege ya Indonesia ambaye aliendeha ndge safari ta kabla haijaanguka alisema alipata tatizo lile lile lakini akaamua kuitoa ndege kwenye autopilot. Kwa hiyo ripoti ya ajali inaweza kusema kweli operating system ya Boeing 737 Max ina tatizo kubwa- lakini suala ni kwamba, kwa nini pilots walishindwa kufanya kile walichofanya wenzao? Hilo halihitaji upelelezi.
Nimekuelewa bro.
Point yangu ni kwamba huenda kuna hitilafu nyingine hivyo tusubirie reports zote mbili(Lion air na Ethiopian airways) walete mrejesho wa kilichotokea.
 
Sio ndege zote. 737max imewekewa sensor ambayo ikisense kuwa ndege inaangalia juu zaidi,inajiweka kwenye automatic ili kuweka pua ya ndenge ikae sawa,matokeo yake pua ya ndege inaendelea kuangalia chini,na Pilot anakuwa hana la kufanya wanajikuta wanacrash.
Umeongea point nzuri sana, nadhani wewe ni pilot! Ina maana kunakuwa na mgongano kati ya anti-stall system na angle of attack ndege ikiwa kwenye autopilot. Nadhani ukirudisha kwenye manual control na kupunguza angle of attack wakati wa kupaa basi you should be fine, anti-stall system haita-kick in na utaendelea kurusha ndege bila tatizo. Sasa inaonekana hapo ndipo kilipokuwa kitendawili kwa hawa mapilot walioangusha 737 Max.

Ila ukweli unabaki kwamba automatic operating system za Boeing 737 Max zina tatizo kubwa.
 
Nimekuelewa bro.
Point yangu ni kwamba huenda kuna hitilafu nyingine hivyo tusubirie reports zote mbili(Lion air na Ethiopian airways) walete mrejesho wa kilichotokea.
Pamoja! Ila si unajua tena haya mambo lazima tutaongea sana kabla ripoti haijatoka.
 
Boeing tatizo lao walitaka kuijibi A320 Neo. Ndo wakajikuta wanakuja na B737 max 8,max9.Ambayo ipo very automatised na kuifanya pua iende chini pale ndege inapohisi kuna stalling. Kosa lao hawakuwafundisha mapilot. Wameishia kuwapa manual tu. Maana wanajua kufundisha ni gharama kubwa sana hivyo wakaona watapoteza wateja. Tatizo ushindani wa biashara kati ya Boeing na Airbus ndo unatufikisha hapa.
Umefanya Wrong assumptions. Anaetakiwa kulipia mafunzo ya pilot wake ni Shirika la ndege husika. Wao ndio wanatakiwa wafanye ivo. Halafu, huruhusiwi kurusha ndege ambayo huna rating yake, kwaio mapilot wote wanaorusha 737 max wamesomea hio ndege. Ishu ni kuwa, kuna possibility Boeing hawakuwafundisha Pilots nini cha kufanya ikitokezea hio scenario ya pua kuelekezwa chini.

It seems there is a missing information kwenye checklist book
 
Mimi ni Aviation enthusiast nmesoma reports kuhusu ndege na ajali zake nkagundua kwamba Ajali ni ajali tu, there is no specific case inayohusu ajali zote.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
hata mapilot wa marekani walilalamika,tatizo ni kuwa hizi ndege zilikuwa zinahitaji software update,sasa mwezi uliopita serikali ya marekani ilifungwa,juu ya mambo ya bajeti na hili suala likapelekea kucheleweshwa kwa boeing kuziupdate hizo ndege
 
Umefanya Wrong assumptions. Anaetakiwa kulipia mafunzo ya pilot wake ni Shirika la ndege husika. Wao ndio wanatakiwa wafanye ivo. Halafu, huruhusiwi kurusha ndege ambayo huna rating yake, kwaio mapilot wote wanaorusha 737 max wamesomea hio ndege. Ishu ni kuwa, kuna possibility Boeing hawakuwafundisha Pilots nini cha kufanya ikitokezea hio scenario ya pua kuelekezwa chini.

It seems there is a missing information kwenye checklist book
Mkuu hebu soma tena comment yako halafu useme inatofauti gani ya mtu uliyem-quote huku unasema kafanya wrong assumptions

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hiyo kumbe hata sisi akina siye tunaweza kuyarusha angani madreamliner kwa msaada wa autopilot.

Nashauri awamu nyingine tukinunua ndege izinduliwe na waziri wa usafirishaji ili kuwaonesha hawa mawakala wa mabeberu kuwa tuko serious na uwekezaji kwenye anga za mbali
 
Back
Top Bottom