KUMBE MAMBO HAYA yanawezekana

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
mfungwa haruna gombellar akionesha nondozzz zake za sheria shahada ya kwanza baada ya kutunukiwa leo. makamu mkuuu wa chuo kikuu huria profesa tory mbwete amesema kwamba tukio hili la kihistoria liliwezekana baada ya chuo kuwekeana mkataba na wizara husika ili kumruhusu mwanafunzi wao abukue. mkuu wa jeshi la magereza afande nanyaro amesema hakukuwa na tatizo kwa gombeller kujisomea kwani kama ni msongamano magerezani upo kwenye sehemu za kulala tu, lakini mchana wafungwa huwa na nafasi kibao za kufanya shughuli kama hiyo ya kujisomea. gombellar ameweka historia kuwa mbongo wa kwanza kutwaa nondo akiwa kifungoni. maelezo ya kesi yake haikutolewa na afande nanyaro amesema hilo halikuwa swala kwa leo na pia ni siri ya mfungwa.

http://www.issamichuzi.blogspot.com/
 
je hapa serikali ya CCM itapewa hongera zake inayostahili ??

Binafsi naipa serikali hongera kwa hilo !

lakini hiyo haimaniishi wasioweza kujilipia shule muanze uharifu halafu mkapate elimu bure jela !
 
jamani kuna hii thread hapa, nzuri tu. kama mtakuwa na muda naombeni tuipitie hii pia !

Shukrani !
 
Nimeiona hii kitu, kwa kweli ni very moving sikutegemea kuwa bongo kuna kitu kama hii, kwa kweli ni safi sana ingawa ni vyema kama ingesemwa huyu Mfungwa alifanya nini hasa kilichompelekea kufungwa miaka 50,

Mimi nilifikiri ni US tu na majuu ndio wafungwa hupata nafasi kama hizi, unajua jamaa ana mke na watoto, kwa kweli inatia huruma sana, lakini mwenye dataz atuwekee mfungwa alichofanya!

Halafu bado pia tunamkumbuka Babu Seya, majuzi niliongea na mtoto wa kike wa Chinyama Chiyanza, maana mpaka leo bado huwa ninaifuatlia hiyo kesi, huwa ninaamini kuwa kuna siku ninaweza kumsaidia mkuu na watoto wake na kifungo cha maisha kama kweli walivyowahi kuniambia kuwa hawakufanya ile kitu, huyu mtoto wa Chiyanza, anasema kuwa baada ya baba yao kufariki, wao wakiwa wadogo sana walichukuliwa na kulelewa na Nguza mpaka sasa ni watu wazima na watoto wao, kama ni kweli anasema basi angewaanza wao kwanza, ingawa pia kuna story nyingi sana kuhusiana na ishu hiyo, lakini tunamuomba Mungu, awasaidie Babu Seya, na watoto wake maana yeye na familia yake ndio sorry tena,

Lakini hii story ni very moving, ya mfungwa kupata Degree akiwa jela ya bongo!
 
je hapa serikali ya CCM itapewa hongera zake inayostahili ??

Binafsi naipa serikali hongera kwa hilo !

lakini hiyo haimaniishi wasioweza kujilipia shule muanze uharifu halafu mkapate elimu bure jela !

....hata ukijenga nyumba na kuoa utashukuru CCM,jina lingine ni unazi uliokomaa
 
Jambo la kupongezwa kwa mfungwa mwenyewe kuwa na moyo wa kupiga book
 
Back
Top Bottom