Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799
mfungwa haruna gombellar akionesha nondozzz zake za sheria shahada ya kwanza baada ya kutunukiwa leo. makamu mkuuu wa chuo kikuu huria profesa tory mbwete amesema kwamba tukio hili la kihistoria liliwezekana baada ya chuo kuwekeana mkataba na wizara husika ili kumruhusu mwanafunzi wao abukue. mkuu wa jeshi la magereza afande nanyaro amesema hakukuwa na tatizo kwa gombeller kujisomea kwani kama ni msongamano magerezani upo kwenye sehemu za kulala tu, lakini mchana wafungwa huwa na nafasi kibao za kufanya shughuli kama hiyo ya kujisomea. gombellar ameweka historia kuwa mbongo wa kwanza kutwaa nondo akiwa kifungoni. maelezo ya kesi yake haikutolewa na afande nanyaro amesema hilo halikuwa swala kwa leo na pia ni siri ya mfungwa.
http://www.issamichuzi.blogspot.com/