Kumbe madaraja{classes] ya leseni mpya za magari ni pesa yako tu! Hata ukitaka yote unapata!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe madaraja{classes] ya leseni mpya za magari ni pesa yako tu! Hata ukitaka yote unapata!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by white wizard, Jul 21, 2011.

 1. w

  white wizard JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Wanasema ukistajabu ya musa utaona ya filauni,juzi nilikwenda trafic makao makuu,kufuatilia leseni yangu ya gari,kila kitu kwa upande wa tra nilikuwa nimemaliza,nimeingia ktk ofisi ya trafiki makao makuu,nikakuta watu wapo kwenye foleni,ya kuingia,cha ajabu wengi ya wale waliokuwa wanatoka ndani ya ofisi hiyo,wanasikitika,kuwa wameambiwa warudi tena tra au kama wana 20,000,wawape ili wapitishe leseni zao ili waende kwa ajili ya malipo tu kule tra.Ilipofika zamu yangu nikaingia akaanza mkwala wa kunionyesha alama kama mia hivi za barabarani ili nimtajie moja baada ya nyingine, hiyo yote ni zengwe tu kuweka mazingira ya kukutoa upepo!!Mi nilikuwa nahitaji class D,ndipo akaniambia toa shilingi 40,000.nikuongezee class B na classA,nikamwambia shida yangu ni D,baadaye akasema mtandao hamna! eti kama una hela ya kutosha utapewa CLASS A HADI ILE YA WINCH!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole mzee, sasa kama wewe ni mzalendo ulichukua hatua gani? Au ndio hii ya kuja kuripoti hapa JF?
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tanzania bana, Kazi ya polisi haitakiwi kuwa utoaji wa leseni hiyo ni kazi ambayo ingeundwa idara ta TDLA - Tanzania Driving Licence Authority: idara hii ingekuwa chini ya wizara ya mambo ya ndani kwenye upande wa technical na wizara ya fedha upande wa makusanyo ya malipo under one door. Kuwapatia madaraka makubwa polisi wenye njaa ni kuu-najisi mfumo mpya kuanzia mwanzo. Tutakuwa tumerudi kwenye square one baada ya utoaji kukamilika.
   
 4. w

  white wizard JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Mimi nilimwambia nataka daraja,nililojaza hapo'D"basi.ndio tatizo la mtandao likaanza.akaniambia nirudi siku nyingine.ndio maana nimetoa angalizo,hapa jf.
   
 5. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa unamaanisha hausupport rushwa au? Duh kama mie nadhani ningeweza kuwa tempted kumuhonga maana foleni na maangaiko yanachosha

  At the end of the day mie kuwa mstaarabu hakuna atakaye nipa cheti cha nidhamu kwa hiyo mambo mbele kwa mbele

  Mie naendesha manual siko ***** na ma auto ambao wengi hawajui kuendesha manual
   
Loading...