Kumbe Maalim Seif Sharif HAMAD yupo kazini..Nilidhani kalala baada ya kupata sahani ya wali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Maalim Seif Sharif HAMAD yupo kazini..Nilidhani kalala baada ya kupata sahani ya wali.

Discussion in 'Jamii Photos' started by Nicksixyo, Nov 25, 2011.

 1. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameanza utekelezaji wa mpango wake wa kutembelea barza za mazungumzo kwa lengo la kuwa karibu zaidi na wananchi.

  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ameanza ziara hiyo katika barza ya Radio One Darajabovu Zanzibar na kuzungumza na wananchi juu ya mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo yao na taifa kwa jumla.

  Amesema ameanza ziara hiyo katika Barza hiyo kwa kuelewa historia yake katika historia za siasa za upinzani Zanzibar, “Nimeamua nianzie barza zangu hapa Radio One kwa kuelewa historia na na umuhimu wa barza hii katika ulingo wa siasa zetu”, alisema Maalim Seif.

  Ziara hiyo inatoa changamoto kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ambao wamekuwa wakilalakiwa kwa kukimbia majimboni mwao na hatimaye kuwa mbali na wananchi, jambo ambalo linawafanya wapiga kura wao kutoamini kile kinachotokea baada ya viongozi hao kuchaguliwa.

  Mara kwa mara Maalim Seif amekuwa akiwahimiza viongozi wa majimbo kufanya bajeti ya muda ili kutenga muda kwa ajili ya kutembelea barza za mazungumzo na kushiriki shughuli za kijamii zikiwemo mazishi na harusi.

  Katika mazungumzo hayo Maalim Seif alielezea juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuwakwamua na ukali wa maisha, licha ya kuonekana hali kuwa tofauti na hivyo kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa mbali mbali hasa vyakula.

  Amesema serikali inatambua hali inayowakabili wananchi lakini inafanya juhudi kuona kuwa matatizo ya wananchi yanapatiwa ufumbuzi muafaka katika kipindi kifupi kijacho, “kipindi cha mwaka mmoja uliopita serikali ilikuwa inajipanga kuangalia namna ya kukabiliana na matatizo haya, lakini nna matumaini kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo hali itakuwa tofauti kabisa Insha-Allah”, alisema Maalim Seif.

  Amesema serikali inafanya juhudi za kuwaalika wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar sambamba na kuimarisha huduma za kilimo na uvuvi kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi.


  source: Maalim Seif atembelea barza za mazungumzo - Wavuti 7767148.jpg
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  hazina uwakilishi wa jinsia au makundi! Ama wao hawana ajenda za kuwakilisha?
   
 3. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Anajitambulisha kwa Barza na vikundi vingine vidogovidogo ili kuongeza utambulikaji wa chama chao miongoni mwa wananchi...Ndio fikra zake za kujenga chama.
   
 4. F

  Falconer JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Maalim Seif ni mwana siasa na Tanzania wanajua kuwa baada ya Mwalimu Julius, Maalim ndie mwana siasa bobeya. Tazameni namna anavokwenda na watawala. Hana vishindo bali anatumia akili.
   
Loading...