Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
KATIBU wa CCM wa Wilaya ya Tarime, Livingstone Lusinde, amelalamikia viongozi wa chama hicho wilaya ya Chamwino, Dodoma kumruhusu mbunge wa Mtera, John Malecela 'kukampeni' kabla ya wakati.
Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake, kuwa viongozi wa wilaya walionesha dhahiri kumpendelea Malecela kwa kumruhusu kufanya mkutano Dodoma Mjini.
Lusinde alifikia hatua hiyo baada ya kudai kushambuliwa na viongozi wa wilaya ya Chamwino, baada ya kutangaza nia yake ya kugombea Mtera Machi 7 mwaka huu, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alidai kuwa yeye na Malecela walikubaliana mwaka 2005 wakati Lusinde akiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) na kuamua kipindi hicho alipohamia CCM.
"Mimi na Malecela tulikubaliana kuachiana nigombee ubunge wa Mtera ... nashangaa mara ya kutangaza nia yangu hiyo, nashambuliwa na viongozi wa wilaya, ninamtaka Mzee Malecela apinge kama hatukukubaliana mwaka 2005," alisema Lusinde.
Lusinde alikoti katiba ya chama cha mapinduzi ukurasa wa 21 kifungu kidogo cha katiba cha 7 ambacho kinasema ni marufuku jumuiya yoyote inayoongozwa na chama cha mapinduzi kumjenga ama kumbomoa mgombea yeyete mgombea mwingine.
Alidai ni haki ya kikatiba kutangaza nia ya kugombea na kusema yupo tayari kuacha au kufukuzwa na hata kusimamishwa kazi ya ukatibu wa CCM Tarime kama ni makosa yeye kugombea jimbo hilo.
Gazeti hili lilipowasiliana na Mwenyekiti wa Wilaya ya Chamwino Dodoma kuhusu kumruhusu Malecela kukampeni kabla ya muda na viongozi kumshambulia Katibu huyo mara baada ya kutangaza nia yake kugombea Mtera, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Chamwino, Charles Uranga alikiri kufanyika mkutano Dodoma lakini haukuwa wa kumpigia kampeni Malecela.
Uranga alisema mkutano huo, ulikuwa wa kutoa tamko la kuzuia kampeni na kuhusu habari zilizotolewa na gazeti moja la kila siku alidai kuwa lilikosea.
Alidai kuwa gazeti hilo lilimkariri Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chamwino, Patrick Nyambuya, akidaiwa kushawishi Umoja wa Vijana wa CCM wa Wilaya hiyo, kumpigia debe Malecela atetee kiti cha ubunge Mtera jambo ambalo si kweli na kulitaka gazeti hilo likanushe habari hiyo.
Uranga alisema Katiba ya CCM inakataza kumuunga mkono mgombea mmoja na kwamba wagombea wote wanapewa demokrasia sawa wakati ukifika.