Kumbe Lowassa ni msanii by proffesion

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Kwakuwa EL amesoma mambo ya theatre ARTS Katika ELIMU yake ya chuo kikuu,

Kwakuwa majibu na maelezo ambayo amekuwa akiyatoa ni ya kisanii,

Kwakuwa amedhirisha anaweza kutumia vizuri Elimu yake ya usanii wa jukwani (wengine wanamuita Ndanda Kossovo),

Na kwakuwa habari hii imethibitishwa na classmate wake wa miaka ya 75; JE wananchi wanasubiri nini kupuuza kauli zake za kisanii?

Tuendelee kuomba wakati huu wa kuwaamsha watanzania...
 
Education
kwa mujibu wa wikipedia na wenyewe wameshaipata hii
Lowassa received his Undergraduate degree in Theatre Arts from the University of Dar es Salaam and a Masters Degree in Development Studies from The University of Bath in the United Kingdom.

http://en.wikipedia.org/wiki/Edward_Lowassa
 
Na ashukuru kuwa na urafiki na JK, vinginevyo hata unaibu asingeupata labada angemfanya kuwa mkuu wa mkoa, huko nako sidhani manake hana sifa za uanajeshi
 
ni kweli, ndiyo maana alishindwa kumjibu mwanafunzi wa primary alipomuuliza kama kweli watanzania wote wataweza kupata maisha bora
 
Naona Mwakyembe angefaa kuwa waziri wa Sheria maaba amezama humo sina hamu. lakini labda naye anngepindisha uongo kuwa kweli maana utatu nao una vibweka.
 
sikujua jamaa ana kibali (cheti) cha kufanya usanii !

akiulizwa anaweza kujibu kwani serikali ilimlipia kusoma USANII kisha asiutumie??
 
HAhahaha Lowasa aka Rich man from Monduli (Richmond) yeye kwa kuwa amesomee sanaa yupo kwenye jumba la sanaa (siasa)akipiga porojo sintoshangaaa mwanasaa huyu akiwa ndiye chaguo la chama tawala kuwa mgombea uraisi 2015!!

Propaganda ameishaanza anajaribu kujenga umaarufu kisanii nchini ndo maana kila siku yupo kwenye ziara mikoani kujenga mazingira. kwa mtazamo wangu mpango wake huo unaweza usifanikiwe maana mambo anayo kutana nayo huko yanamshusha hadhi mfano anapotoa majibu ya porojo ama anaposhindwa kujibu swali na mwanafunzi wa kidato cha kwanza anapotunishiwa misuli na baadhi ya wakuu wa wilaya !!!

Hii bwana Rich man from Monduli inamshusha hadhi kuna uwezekano asiweze fikisha adhima yake ya kuwa ukuu wa sirikali!!!
 
poleni wote wanofikiria El ni kiongozi makini,ndio anayechangia umasikini wa nchi hii,anaiba pesa ambayo ingeshajenga barabra za Lindi ,Singida..
mie akigombea tu najichoma moto
 
poleni wote wanofikiria El ni kiongozi makini,ndio anayechangia umasikini wa nchi hii,anaiba pesa ambayo ingeshajenga barabra za Lindi ,Singida..
mie akigombea tu najichoma moto

Usijichome moto! Stand up and fight! But 2015 is too far away, many interesting things may happen! Wewe anza kujiandaa mapema kama yeye alivyoanza kujiandaa.
 
Na ashukuru kuwa na urafiki na JK, vinginevyo hata unaibu asingeupata labada angemfanya kuwa mkuu wa mkoa, huko nako sidhani manake hana sifa za uanajeshi


HIVI haya maoni yenu yanareflect nini kuhusu maendeleo ya Nchi? HIVI ili mtu awe waziri Mkuu anatakiwa awe na elimu gani?
HIVI haya maoni tunayoyatoa hatudhani yanakua more Personal than of a Public interest? Mnanikumbusha maisha ya kitoto, ambapo kundi moja likigombana na mwenzao mmoja basi watamsema hata kwa kununuliwa kwake viatu vipya vizuri.

Mimi nadhani tunaihitaji kuwa more constractive tunavoleta mada zetu mbele ya meza.
 
HIVI haya maoni yenu yanareflect nini kuhusu maendeleo ya Nchi? HIVI ili mtu awe waziri Mkuu anatakiwa awe na elimu gani?

Cha muhimu ni kuwa mtu kuwa na PM anatakiwa awe na akili ya kutosha kuwa kiongozi wa watu anaowaongoza, kama anaowaongoza wote ni mbumbumbu, hata PM akiwa darasa la saba hakuna ubaya. Usanii unaozungumizwa hapa ni ule alioufanya JK unaoonesha kuwa anawafanya watanzania wehu, kusema uchumu unapaa wakati inaonekana kabisa unaanza kudidimia, kuuliza watu wamefanyia nini taifa wakati yeye alichofanya halionekani(labda wewe unaliona) Kwa hiyo watu wamegundua kuwa ni kutokana na kuwa yeye ni artist by profession ndiyo maana anafanya anayofanya. I hope he did not take it personal.
 
Hey people,

You caught me by surprise! Ninavoelewa mimi ni kuwa pale Mlimani kuna idara ... sijui faculty...kubwa ya ARTS (sikusoma mlimani) iliyo na madaktari na maprof wa ARTS, i do not know if you guys have the slightest idea the amount of harm mnayosababisha kwa waTz wenzetu hawa: dada zetu, kaka zetu, baba na mama zetu nk.

Utendaji mbovu wa mtu mmoja ni personal attribute na sidhan kama watu wote waliosoma/wanaosoma hiyo kozi wanastahili hizi kejeli au ndo "one bad apple spoils the barrel". Je, mnamaanisha idara hii ifungwe? Je, mnaelewa watu wanadai kuwa journalism ni kozi inayofanywa na watu waliofeli wakawa hawana pa kukimbilia?

Bwana acheni hizo, ni mambo ya kitoto na ukale kwamba: "nikikua nataka kuwa daktari", "mimi nataka kuwa mwanasheria", "mie rubani au injinia" ...... all stereotypes you know...wazee mnashikilia vitu hivi hadi utu uzima! duh basi ipo kazi....
 
salamu kwenu wana jf
Mwaka 1974 hadi 1977 Ndg.Edward Ngoyai
Lowassa alikua chuo kikuu cha Dar (UDSM)
akisomea kozi iitwayo Fine &Performing Art. Hii
ni kozi inayohusu usanii kwa mapana yake.
Ukihitimu kozi hii unakua msanii by professional.
Miongoni mwa areas of competence kwa mhitimu
wa kozi hii ni kuweza kuandaa na kucheza movie,
muziki, tamthilia, na futuhi. So hatuna sababu
kushangaa haya yanayoendelea maana Eddo
anatekeleza taaluma yake kwa vitendo.
Maigizo ya masheikh wa Bagomoyo, movie ya
wanafunzi wa UDOM na Futuhi ya wachungaji wa
kipentecoste hapo juzi na jana ilikuwa zamu ya bodaboda ni sehemu ya kuonesha
kuwa bwana Eddo alielewa vema kozi aliyoisomea
na hakupata degree yake bure. Hongera Eddo
kwa kutumia taaluma yako . Hakika wewe ni
Msanii by professional.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom