Kumbe Lengo la Jumuia ya Afrika Mashariki ni ardhi yetu! Sitta aweka ngumu Kenya, wamnanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Lengo la Jumuia ya Afrika Mashariki ni ardhi yetu! Sitta aweka ngumu Kenya, wamnanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, May 31, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kenya na nchi nyingine za Jumuia ya Afrika Masharika hawana raha na Samuel Sitta na Tanzania kwa ujumla. Hii ni baada ya kuwawekea ngumu kuingiza suala la ardhi kwenye jumuia. Taarifa toka kwenye vyombo vya habari zimeonyesha chuki kiasi cha kuanza kutafuta pa kushika kuiadhiri Tanzania ionekane kama mnafiki. Maana kichwa cha habari kinasema kuwa Tanzania inahubiri maji na kunywa mvinyo. Tulishaonya kuwa hakuna mantiki ya kuwa na muungno wa Afrika Mashariki wakati nchi zote isipokuwa Tanzania hazina ardhi na zina idadi kubwa ya watu. Chukulia mfano Kenya ambayo ni chini ya nusu ya Tanzania ina idadi ya watu sawa na Tanzania. Kama ni kuungana heri tuungane na Msumbuji na Zambia lakini si nchi zisizo na raslimali wala ardhi. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Habari uliyoandika haiambatani na kwenye gazeti; na Kenya sio Nusu ya Tanzania; habari iliyoandikwa ni hii hapa chini
  Haikuzungumzia Jinsi Wakenya au East Africans wanavyoitaka Ardhi ya Tanzania; wanazungumzia Jinsi wananchi masikini wanavyodhulimiwa Ardhi Tanzania na Wajanja Investors na Sitta hawezi kuguarantee ardhi kwa hao wananchi wake

  The report says land disputes pitting poor villagers against powerful investors are now at more than 1,000 every year.

  According to the institute's executive director Yefred Myenzi, on average there are five land disputes daily in Tanzania and, three out of five involve powerful investors.

  In this context Mr Sitta's call should come in for closer scrutiny given the famously protective country cannot guarantee the interests of its locals.
   
 3. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ushauri wa Tanzania kuhakikisha watu wake wana ardhi ni mzuri ila ukilinganisha na tatizo kama hilo nchini Kenya kusema ukweli ni ile hali ya nyani haoni nonihino lake. Otherwise kichwa cha habari kwenye ile habari kinatosha kueleza kilichopo nyuma ya pazia. Hebu pigilia mstari maneno haya: Mr Sitta was quoted by the state-owned daily as saying that there were all sorts of "dirty tricks" being employed in order to drag the land issue into the EAC treaty.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  eatv imeshatuunganisha na inatosha.
   
 5. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni kweli tuungane ila aridh n ishu nyingine wajamen
   
 6. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mbona umechukua sehemu iliyokufurahisha tu au hii uliyoacha haina maana? Au wewe ni mkenya nini? Haya nimekurahisishia uisome tena, hasa paragraph ya mwisho..
  The prospect of "foreigners" (Read entrepreneurial Kenyans) owning land in the country due to the opening up of the region by treaties governing the bloc has been highly sensitive, and indeed Mr Sitta was quoted by the state-owned daily as saying that there were all sorts of "dirty tricks" being employed in order to drag the land issue into the EAC treaty.

  Speaking in Dar es Salaam at an induction seminar for newly-elected Tanzania members to the East African Legislative Assembly, Mr Sitta claimed land was a key target and urged the legislators to guard the national interests of their country.
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hili suala la ardhi tunatakiwa tukabiliane nalo kisayansi na kisheria zaidi kuliko kisiasa kama anavyo fanya waziri wetu, haitoi picha ya kimtazamo wa kimaendeleo.
  solution ya kwanza ni kuwaambia wenzetu kwa kuwa ardhi ni ya serikali , mtu akitaka ardhi kwa shughuli za kiuchumi basi aoitie mamlaka husika na kukodishwa hiyo ardhi kwa rent tutakayo mpa sisi , na ikihitajika majengo ya kudumu basi yatajengwa na serikali na huyo investor kazi yake ni ukodishaji, ya pili ni kuwaambia wenzetu kwamba kabla ya kwenda mbele tunahakiki ardhi kwani kuna watanzania wanaishi sehemu hizo hivyo kuna ardhi ya kijiji, ya kiukoo nk, na mwisho ni kurudisha jkt ambayo ilimiliki mashamba makubwa tu ,badala ya kuacha ardhi nyingi bila kutumika, hivyo wenzetu kutuona tuna choyo tu, hili la jkt litasaidia pia kuondoa hawa vijana wazururaji wa vijiweni kila kija asiye na kazi maalumu, basi sehemu yake ya maisha iwe huko jkt akazalishe, apate malazi na chakula na kujifunza jinsi ya kujitegemea akitoka huko. basi anaweza kuwa mkulima mzuri wa mazao mbali mbali pamoja mboga mboga . hivyo waziri husika apeleke hoja kwenye baraza la mawaziri kufanya hili ninalo pendekeza akishirikiana na wizara ya ardhi, sheria na kadhalika
   
 8. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,477
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Hata siku moja hatuwezi kukubali suala la aridhi likawa la EAC, bado tunaangaika na hawa wawekezaji wanaopewa aridhi yetu kinyemela tuongeze tena mzigo mwingine.
   
 9. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Wakati wakipigana kwa swala la ardhi, kuna wakenya na waburundi wengi wamehodhi ardhi yetu. Nilikuwa namtafutia mtoto wangu kindergaten, nikapata kindergaten moja nzuri na kubwa na hapo hapo nikaambiwa mmiliki anataka kujenga shule hapo pembeni ukiangalia eneo ni kama hekari 4 hadi tano. Sasa niulize eneo liko wapi, eneo liko karibu kabisa na ubungo external ila kwa ndani kidogo. Nikaambiwa mmiliki ni Mkenya jamani nilichoka nikasema hapa hatujaweka swala la ardhi kwenye muungano likiwepo ndo watachukua kila kitu. Serikali ya mafisadi yaani wanafanya uozo ndani ya nchi yetu. Ila ninauhakika CHADEMA wakishika dola na kwa kuwa wananchi wengi wanaridhika na hiki chama maana kinafanya kazi karibu sana na wananchi vitu kama hivi ni lazima tuviandikie report hata kama huna cheo popote na kuviwakilisha kwa baba yetu mpendwa Dr Slaa avifanyie kazi na chama chake. Peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
Loading...