Sijijui
JF-Expert Member
- Jan 14, 2018
- 7,879
- 8,800
Kwenye hizo rates wewe umegundua nini?Leo nimejipa mtihani mdogo kabisa kupitia katika bank tofauti na baadh baadhi ya bureau de change za hapa Tanzania,nilichokiona ni kwel kabisa mheshimiwa rais aliposema tunahujumiwa na baadhi ya watanzania wakishirikiana na makanjubah katika bureau de change zao na baadh ya bank ndogondogo ambazo nia ilikuwa ni kuharibu taswira ya uchumi wetu.
Labda nibak kwenye kwel uchumi wa Tanzania kiufup haupo sawa mana hili naliongea kama mtanzania ambae naishi katika jamii ambayo nashinda nayo na naishi nayo lakin wote tunajua kwann uchumi haupo sawa kama hapo nyuma ni kutokana na miradi mikubwa ambayo serikali inaiendesha kwa sasa lakin i hope ikishamalizika tutarud katika njia iliyokuwepo tuwe wavumilivu.
Turud katika point,hata kama uchumi wetu katika kipind hiki haujakaa sawa lakin tusitumie nafasi hiyo kuendelea kuihujumu nchi tujaribu kuwa wazalendo haiwezak dola ilitoka 2250 ghafla kwa miez michache ikafikia 2400 hiyo haipo hata uende nchini Libya ambako kila siku uchumi unaporomoka hawafikii kasi hii.Sasa ona baada ya kuwakaba mahafidhina wakubwa tulipo hii leo katika exchange rate in term of Dollar.
CRDB BANK(Buying 2265, Selling 2325).
NMB BANK (Buying 2270, Selling 2320).
NBC BANK (Buying 2270, Selling 2325).
BOT (Buying 2276, Selling 2299).
KCB BANK (Buying 2267, Selling 2300).
Bureau des change tofauti tofauti (Buying 2275, Selling 2325).