Kumbe kuzuiliwa kwa shughuli za kisiasa zilichangia watu kutoajiriwa

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Wakuu, leo nimeona zimetoka ajira za madkatari Kwa wingi, juzi juzi tangazo la ajira kwa walimu lilitoka.

Nilichogundua kumbe hiii ya wanasiasa kupaza sauti ndio dawa ya Magufuli kumbe. Nimegundua kuwa kungekuwepo na shughuli za kisiasa miaka hiii yote, hili swala la kufuta ule utaratibu wa ajira za walimu na madaktari haungejitokeza, kumbe huyu mzeee alipata upenyo akakosa watu kama Tundu Lissu ndio maana akawa anatamba kwa jeuri.

Halafu kuanzia leo nitamuunga mkono mwanasiasa wa kweli kama Tundu Lissu kwa njia yoyote ile, maana kipindi hiki nimegundua kuwa wapo wanasiasa uchwara akina Lipumba na wanasiasa watetezi wa wanyonge, wanaosemea wanyonge, wanaotetea wanyonge, wanaopaza sauti kwa ajili ya wanyonge. Na kama kuna uwezekano tumuombe Lissu azungumzie sana lile swala la mifuko ya jamiii la kuchukua mafao baada ya mtu kufikisha miaka 60 na Uhakika na hilo linaweza pia kutolewa ufafanuzi na Magufuli.

Chadema ndio maana mnapendwa na Watanzania. Nyie ni zaid ya watetezi, ndani ya week tatu tu, mmesaidia wamachinga, walimu na sasa madaktari daaah MUNGU awabariki Sana chadema sasa Mtoto Wa Dada Yangu amepata ajira kwasababu ya Chadema.

Halafu kumbe week mbili nyuma watumishi wote waliokuwa wanadai mafao yao wameingiziwa mafao yote kwenye account zao? Tobaaa Lissu wa watu jamani tunashukuru MUNGU kukuokoa, pia walimu wote wamepandishwa madaraja yao waliokuwa wamenyimwa miaka yooote mitano. LISSU MUNGU AKUBARIKI.

Daaah imenitafakarisha sana, najiuliza hivi kuna Mtanzania atakaemnyima huyu mtu kura?

Barabara huko mikoani hela inatoka kwa kasi zinajengwa, nakumbuka walimu 13,000, madakatari 1,000 ,wamachinga wameambiwa vitambulisho sio lazima, mzeee anapiga simu kila siku barabarani daaaah huyu mtu ni wakupewa TUNZO yani mwenzi mmoja tu kayapigia kelele haya robo yameishafanyika papo kwa papo daaah!

Hivi yupo mtu anaeweza kupinga maneno ya huyu mtu? Jamani, awasemee na wale waliofukuzwa Kazi Kwa kusingiziwa vyeti feki, n auhakika nao watarejeshwa Mara na haki zao nina uhakika watapewa maaana kila analolisemea kesho yake linafanyiwa kazi utadhani yeye ndio rais, anatoa tu amri mzee anatekeleza ndio maaana mzee alijitetea juu ya uwanja wa Chato kuwa akifa hataondoka nao. Hahahhah!
 
Spana za Lissu si mchezo!! Si walikuwa wanapiga kelele eti maendeleo ya vitu!! Kiko wapi sasa??😂😂😂😂

Ndo mana tukisema Lissu ni mteule wa Mungu mataga inabidi wawe wanatuelewa saaana!

Ndani ya miezi mwezi mmoja tu wa kampeni za Lissu, wamachinga wameambiwa vitambulisho si lazima, ajira za walimu 13000 zimetoka, madaktari 1000 wameitwa kazini , watumishi wameanza kulipwa malimbikizo na kupandishwa madaraja na huko mikoani amri ya kujenga barabara zinatolewa.

Watanzania tuna kila sababu ya kumchagua Tundu Antiphas Lissu mwaka huu!!!

Ni yeye 🔥
 
Eee Mungu mwenye kiti cha enzi. Tumetawaliwa na chama kikuu na Kikongwe. Ni miongo imepita sasa sera zake ni chakavu hazitekelezeki.

Ni chama kimoja kilichokaa madarakani na kushika nafasi nyeti, wameifanya hii nchi ni mali yao. Ninakuomba Mungu tufanyie badiliko lililo bora.

Kura yangu inaweza kuibiwa, ila dua yangu kwako imefika. Amin
 
Eee Mungu mwenye kiti cha enzi. Tumetawaliwa na chama kikuu na Kikongwe. Ni miongo imepita sasa sera zake ni chakavu hazitekelezeki.

Ni chama kimoja kilichokaa madarakani na kushika nafasi nyeti, wameifanya hii nchi ni mali yao. Ninakuomba Mungu tufanyie badiliko lililo bora.

Kura yangu inaweza kuibiwa, ila dua yangu kwako imefika. Amin
Amina kwa Jina la Yesu
 
TAL alisema kinyago tulichokichonga wenyewe hutuwezi shindwa kukigeuza kiwe ukuni na kukitumia kama nishati ya kupikia chakula. Sasa ndiyo ule wakati muhimu wa kupata hiyo nishati.
 
Back
Top Bottom