Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe kutekeleza ahadi kazi: Mjane wa Mwangosi alia na Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimbunga, Oct 5, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kupitia uchambuzi wa magazeti kwamba Mjane wa Marehemu Daud Mwangosi analilia rambirambi alizoahidiwa na Dr. Slaa kwenye msiba wa mme wake. Anwalilia waandishi wamsaidie kupata hizo rambirambi toka kwa Dr. Slaa.

  Kumbe kutekeleza ahadi kazi kweli kweli!

  ============

  Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

  HabariLeo | Oktoba 05, 2012

  UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.

  Juzi, mjane wa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Aneti, alijikuta akiomba wanahabari wasaidie kufuatilia rambirambi iliyoahidiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutokana na kiongozi huyo, kukata mawasiliano baada ya msiba.

  "Nina mawasiliano na Profesa Mark Mwandosya ambaye pia aliahidi kumsomesha mtoto mmoja, yeye aliniambia nitakapokuwa tayari nimjulishe ili atume fedha kwenye akaunti ya shule, lakini sina mawasiliano na Dk Slaa," alisema Aneti.

  Mwangosi aliuawa Septemba 2 mwaka huu, kwa kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

  Aliuawa wakati Polisi ikizuia wafuasi na viongozi wa Chadema kufanya mikutano ya hadhara ambayo ilipigwa marufuku ili kuruhusu shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi, kufanyika bila kuingiliwa.

  Baada ya mauaji hayo, wakati wa maziko ya mwandishi huyo, Dk Slaa aliahidi kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwaye Nehemiah, ambaye yuko kidato cha nne katika Sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa.

  "Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake," alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

  Hata hivyo ahadi hiyo, mbali na ukweli kuwa haijatekelezwa, lakini pia hata mawasiliano kati yake na mjane wa Mwangosi hayapo mpaka mjane huyo kuamua kuomba waandishi wamfuatilie.

  Mwingine aliyeahidi kusaidia familia hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mwandosya, ambaye aliiwakilisha Serikali na katika salamu zake za rambimbambi msibani, alisema atabeba jukumu la kusomesha watoto wengine wa marehemu huyo.

  Aliahidi pia kufuatilia ahadi za watu wengine katika kuisaidia familia ya Mwangosi kwa kuwa ni ndugu yake na jirani. "Nitahakikisha familia hii inaishi maisha kama ambavyo angelikuwapo baba yao kwa kuhakikisha kila mtoto wa familia hiyo anasoma kwa kila hatua kwa kuzingatia kuwa hao ni sehemu ya familia yangu," alisema Mwandosya, ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM).

  Gazeti hili lilipompigia Dk Slaa simu kujua mipango yake ya kutekeleza ahadi hiyo, simu yake ilikuwa inaita mara zote bila kupokewa.

  Rambirambi zingine Wakati huo huo, wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Iringa, wametoa rambirambi zao kwa mjane huyo. Mhasibu Mkuu wa Tanroads Iringa, Alex Mgeta alikabidhi Sh 265,000 juzi katika nyumba yao iliyopo Kihesa Bwawani mjini hapa.

  "Nashukuru sana lakini pia nawaomba kwa kupitia michango ambayo nimeambiwa inaendelea kukusanywa mnisaidie nimalizie nyumba hii," alisema Aneti.

  Aneti alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne vya kulala haijakamilika na ikikamilika, atapangisha baadhi ili kiasi cha fedha atakachopata kitumike kuendesha familia yake.

  Septemba 30 katika harambee iliyofanyika Iringa kwa mujibu wa blogu ya Mjengwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto alijitolea kumchangia mjane huyo kwa kumlipia ada ya uanachama wa Bima ya Afya kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo.

  Alikaririwa akisema: "Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, naona ni muhimu akawa na uhakika wa huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya kwa miaka mitatu."

  Baadhi ya watu wengine maarufu waliojitokeza kumchangia mjane kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy-Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku na Mobhare Matinyi aliyepata kuwa Mhariri wa Majira.
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hivi Rambirambi ni deni? Mbona inakuwa kazi?
   
 3. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,509
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Ahadi kazi kweli kutekeleza..hata juzi kule Arusha kuna mjane wa marehemu aliyafariki kwenya vurugu za Arusha alililamika kwenye mkutano wa CUF kwamba ahadi alizoahidiwa na baadhi ya wanasiasa hazikutimizwa..sumu ya siasa ni ahadi za jazba!!!zinaweza zikakuvunjia heshmaa
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,424
  Likes Received: 19,747
  Trophy Points: 280
  duh nyie vijana wa kafu na ccm mna mbinu dhaifu kweli ..kajipangee.
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,535
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  Ahadi ni deni wampe rambirambi zake.!!
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa aliahidi kuwasomesha watoto! Sasa msiba umeisha juzi tu, leo ameanza kulia. Au alifikiri atapewa hela!? Huu ni uchuro!
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu mheshimiwa sana Kimbunga, imekuwaje mpaka unapost thread isiyo na mashiko? Hata msiba umekuwa siasa?
  Ungeelezea Dr. Slaa aliahidi nini, manake kama ni kumsomesha mtoto huwezi kukurupuka hivyo bana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Yule mjane alikiri kupokea 5mil kutoka kwa viongozi wa cdm iliyotolewa na Sabodo. Akasema viongozi wa cdm walimtafuta lakini alikuwa Tanga, hivyo hawakumpata. Tangu amerudi Arusha amekuwa akiwatafuta bila mafanikio sababu hajawakuta ofisini (labda wapo bize na m4c). Sasa hapo napo panahitaji lawama!? Huku ni kutumika kisiasa!
   
 9. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Uhuru na Habari leo? kama bado unayaita magazeti, Labda upo nje ya nchi.
   
 10. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiyo taarifa imeandikwa na Habari leo! Hakuna gazeti hata moja nyingine yenye habari hiyo, ukiweka post andika umesikia kwenye gazeti gani, hii kukurupuka na kuamini hadithi za HL sio busara!
   
 11. Ghiti Milimo

  Ghiti Milimo JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 60
  Kufa kufaana!
   
 12. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mkuu,leo hii umesahau sifa kemu kemu zilizomwaga kwa marehemu ikiwemo alikufa akifanya kazi ya chama na ukizingatia Dr hakuombwa na familia ya marehemu ni heri awe muungwana atimize kile alichoahidi.

   
 13. o

  obwato JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahadi ni deni na miongoni mwa mambo yanayomfanya mtu kuingia kwenye kundi la unafiki ni kutotimiza ahadi, kuaminiwa ukafanya hiana pamoja na kusema uongo, cdm wapo kwenye kipindi cha kujiimalisha na wapenda mabadiliko wengi wana imani kubwa juu yao hivyo wawe makini na mambo yanayogusa hisia za wapenda haki wengi..

  Nakumbuka chama kiliahidi laki 5 na kusomesha kijana mmoja kama hazijatekelezwa basi cdm itumie vizuri fursa hii ya ukumbusho kutekeleza hilo.
   
 14. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  AIBU aibu watu kupenda Makamera, maflash na kukaa nyuma ya vinasa sauti mradi uonekane mwenye uchungu kumbe Siasa tu
  Hakuna haja ya kutoa ahadi ww toa pole tutakuona
   
 15. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Kwani hao watoto/mtoto alikuwa anadaiwa ada ya shule wakati Marehemu yupo hai?
  Maana sielewi kwa nini alie badala ya kukaa chini na kumwombea Dr Slaa baraka.

  Kwani alimwambia lini atamsomesha? Huyo mtoto yupo nyumbani hana shule? Si amepokea pesa juzi kama kweli anadhamini na anahitaji mtoto aende shule si atumie hizo?

  Anataka apewe pesa then atie mfukoni pia? Dr Slaa labda anashughulikia plan ya kusaidiaje, labda kufungua acoount ya pesa zitoke humo direct kwenda shule hapo baadae.

  Ok nisaidieni kujua, huyo mtoto haendi shule now? Kwani ni makosa Dr kutaka saidia? Mie nilivyosomaga niliamini ni baadae labda from next year ndo atasaidia au baadae zaidi. Wewe mama hii inakuvunjia heshima as wengine watakimbia kukupa ahadi. Kama kuna mtu mwingine kasema atakusaidia basi usitumie kuharibia Chadema kuongoza.

  Umeshindwa kumtafuta simuni kama una shida?
   
 16. o

  obwato JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama kweli alikiri kupokea 5mil na kuwa alitafutwa hakupatikana kisha akaibukia kwenye magazeti na kuongea kauli tata basi ni mchache wa shukrani na atawakatisha tamaa wenye nia njema naye na kuwapa watoto wakati mgumu wa kusaidiwa. Asamehewe tu na kuelimishwa juu ya madhara ya kuongea kwa msukumo wa zawadi za kanga, Kapelo na skafu.
   
 17. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh kwahiyo hizo 5M toka kwa Sabodo, alishazipata huyu Mama au bado hazijamfikia?
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hadi sasa Ritz hajauona huu uzi!
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Marehemu alikuwa anafanya kazi ya ofisi aliyotumwa! Alikuwa ni mfanyakazi wa chanel ten na sio cdm! Acha kupotosha.
   
 20. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ahadi ya mtu mmoja anashindwa kuitimiza je ya watanzania millioni arobaini ataiweza?

   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...