Cheef Baroka
JF-Expert Member
- Apr 28, 2019
- 491
- 1,000
Wakuu: Mimi ni miongoni mwa watu tunaopenda sana amani , napenda kuwa nafuraha muda mwingi, nafurahi zaidi mwingine anapofurahi au mambo yake yanapomuendea sawa.
Nimekuwa mtu nisie hifadhi chuki wala kuishi na vinyongo moyoni, nimekuwa nikipuuzia na kusamehe kila baya nalofanyiwa. Mimi ni mtu ambaye naweza kukwazika na mtu ila akija kunililia shida nikamsaidia nakusahau yote alonifanyia.
Mwaka 2010 kuna ndugu yangu (kaka) wa baba mmoja na mama mmoja matumbo mbalimbali, ye alikuwa anajishughulisha na biashara ya udongo (pemba) wanautoa kigoma kuja kuuza dsm. Binafsi sikupenda biashara ile coz nawaonaga wachafu muda wote, inatumia muda mwingi kukamilisha mzunguko (mana wananunua viroba vya udongo kutoka sehem panapoitwa Manyovu wanamwaga chini wanaponda na maji kama udongo wa tofali au kukandikia nyumba za tupe then wanafinyangisha, wanaanika , wanapakia kwenye mifuko then ndo wanasafirisha kuja dsm/ mlandizi ila sana ni DSM) , ni biashara yenye migogoro kwenye malipo, na sijaona mfano wa billionaire au hata millionaire alotokana au kupita kwenye hiyo biashara. So nikamuita tuyajenge, yeye akaniaminisha ile biashara inalipa sana kwamba pamoja na changamoto nilizoorodhesha but ina faida sana.
So siku moja nikapata vihela flani ivi kwa mbinde sana (mana me kipindi hicho sina mishe yyt bado npo school) nikaona kuliko kuhifadhi bank zikakaa tu ni bora niwekeze sehem pia nitapata na uzoefu wa biashara , ikabidi nikae chini na broo nikamkabidhi ile pesa aingize kwenye mzunguko wake azungushe ili nikuze mtaji mwisho wa siku nichukue pesa yangu ikiwa nyingi nikafanye ninachokipenda.
Brother akachukua ile pesa na kweli kazi ikaanza . Mwanzo nikashirikishwa kila hatua but soon nilipouliza faida ya mzunguko wa kwanza akanambia mdogo wangu me nina nia nikusaidie ko tufanye then nitakumegea fungu ukafanye yako. Baada ya hapo me nikawa bze na chuo nilipomaliza ikabidi nikaombe fungu sasa ili nianze harakati zangu duh! apo ndo picha likaanza broo akanambia Dogo mambo hayajakaa sawa ila suala lako linaniwazisha sana mana umekuwa unatakiwa kujitegemea ko nipe muda ,
Ikabidi nimuulizetu share yangu imefika sh ngap akasema nitakumegea kama m 4 nikamwambia broo 4 chache biashara imefanyika muda basi fanya 5 akasema powa ko ikabaki muda wa kukabidhiwa mtonyo. Basi ndugu yenu kichwa zaidi ya michoro ya KIPANYA nikajua matusua nikaweka plan kama zote ila wazo likanijia kuwa nikisema nimepata hiyo pesa nikafanye biashara ambayo sijawahi kufanya nitafeli so nikatufte mishe hata kwa kuajiliwa sehem ili hata pesa ikija inikute nina experience ya biashara apo ndipo nilipoanza kujichanganya kwenye mishe tofauti tofauti ikiwemo M-pesa, nafaka, viatu, nk huku nikijua pesa inakuja. Wakuu kiufupi ile pesa nikawa napigwa tarehe tu, ikaisha miaka miwili bado napigwa tarehe tu ,hadi naingia kwenye system bado pesa haijaja mwisho wa siku simu zikawa hazipokelewi wala sms hazijibiwi .
Haya: na broo mwingne tena (kaka yangu mkubwa) yeye alinipa kazi yakusimamia kazi yake ambayo walikuwa share na jamaa yake kiufupi malipo yake hata shilingi moja sijalipwa mpaka sasa na yeye simu hazipokelewi wala sms hazijibiwi. Nilipumuulza jamaa yake akanambia yeye alitoa pesa yote hadi ya usimamizi ko broo atakuwa kaila broo wangu. Wakuu inauma sana kutapeliwa na ndugu.
Nije kwenye point:
Ukweli ni kwamba kaka zangu hawa nafsi yangu imeshindwa KUWASAMEHE
najilazimisha sana lakini nashindwa. Najaribu kukumbuka zawadi walizonipa utotoni nakumbuka nikiwaomba vipesa vidogo vidogo wananipa, nguo,viatu na vitu kibao, Pia najaribu kuukumbuka msemo wa damu ni nzito kuliko maji ila pa1 na yote moyo unashindwa kusamehe hatimae unanikumbusha msoto nilopata kipindi natafuta ile pesa (kubeba, mawe, kubeba mizigo, kulima nk) nakumbuka msoto kipindi nasimamia kazi ya broo huyu mwingne (jinsi nilivyokuwa najitesa kufanya kwa ubora kama yangu, nalala masaa 3, natukanwa nk) nakumbuka muda nilopoteza nakumbuka walivyo nivurugia mipango yangu. Wakuu natamka haya kutoka Moyoni Wallahi nimeshindwa kuwasamehe.
Jamani nilikuwa nachukulia rahisi ila ndo nagundua "KUMBE KUSAMEHE NIKAZI HIVI " wakati mwanzo nilichukulia ni jambo simple sana.
Najiona nina kila sababu yakuwasamehe ila NIMESHINDWA KUSAMEHE.