Kumbe Kuongoza Migomo ni Sifa na Kigezo!

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Nimefuatilia malumbano na majibizano kwenye mitandao ya kijamii kuhusu katibu mkuu mpya wa chadema..

Katika harakati za kumtambulisha dr. mashinji jana kwenye viwanja vya furahisha,mwenyekiti mbowe alimsifia katibu mteule kuwa alishawahi kuendesha migomo ya madaktari pale muhimbili..

Siku ya leo pia, ndugu kigwangala ameshika headlines kwa kudai yeye ndiye aliyeshiriki kikamilifu kuendesha migomo hiyo na akimtuhumu dr mashinji kuwa hana misimimo hata ikatokea wakamtenga!

Sasa nini tafsiri ya haya yote maana wote kwa sasa wameshika nafasi kubwa katika vyama na serikali!

Katika hali ya kugoma ni mengi hutokea,kuna athari hasi huweza kujitokeza ukiacha mbali maslahi ya hao madaktari wanayoyagomea..Kama tunakumbuka vizuri,migomo hiyo iliweza kuleta athari kubwa sana kwenye uhai wa binadamu na wengine walipata taabu sana kwenye hicho kipindi!wagonjwa wengi walinyayasika na wengine kupoteza maisha kabisa kwa madaktari kupigania usawa wa maslahi yao..

Cha kushangaza wote hao leo wanaona kuwa ni sifa na wengine kutumia kama sehemu ya kumnadi mteule..Sasa tukirejea tena kwenye kugoma kwao je kumesaidia kuboresha huduma za afya au mtu wa chini mpaka leo au ilikuwa ni maslahi binafsi na kutaka sifa?

Watanzania tulio wengi tuna machungu na ile migomo kwani kuna baadhi tulipoteza ndugu zetu!Kwa wazalendo kama sisi hatujafurahishwa na kujitapa kwenu kuwa mmendesha migomo ambayo mpaka sasa haijaleta tija kwa mgonjwa mwenyewe na hata kwa madaktari wenyewe..huduma bado ni mbovu vilevile,maslahi ya madaktari bado ni mabaya ila mmkeaa kutafuta sifa kwa kuanzisha migomo ili baadae muitumie kama advantage kisiasa..hamna lolote zaidi ya misifa!

Na mkome kabisa siku nyingine kujitapa kuwa mlianzisha migomo..Bado tuna uchungu na ndugu zetu waliopoteza maisha kwa kugoma kwenu!
 
Back
Top Bottom