Kumbe kuna 'Wanasiasa' Waandamizi wengine hawakuhudhuria Msiba Chato na leo ndiyo wameenda 'Kuhani' na 'Kuzuru' Kaburi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,482
2,000
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli wilayani Chato mkoani Geita kuangalia kaburi lake na kumjulia hali Mama yake Mzazi Suzana Magufuli.

Waziri Mkuu Majaliwa amefika nyumbani kwa Hayati Dkt. Magufuli akiwa safarini kuelekea mkoani Kigoma kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Wabunge katika majimbo ya Buhigwe na Mhambwe kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo katika uwanja wa ndege wa Chato alipokelewa na mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

Chanzo: tbc_online

Tafadhali ukitoka Kigoma katika Kampeni upitie pia na Butiama uzuru Kaburi la Hayati Mwalimu na usalimiane na Mjane Mama Maria.

Kisha ukitoka huko pita moja kwa moja hadi Kijijini Lupaso na ukazuru pia na Kaburi la Hayati Mkapa na pia utamkuta Kaka ( Mdogo ) wake utamsalimia pia.

Tanzania nzima Rais aliyefanya Makubwa na anayetakiwa Kukumbukwa na Kuenziwa vilivyo hakuwa huyu tu pekee na tujitahidi Kupunguza Unafiki.

Na Wengine tumeambiwa mlijifungia Vyumbani mwenu na Wake zenu mkifurahia 'Kutwaliwa' Kwake ghafla kwani alishawachokeni na alitaka hata Kutowarudisha tena hapo mlipo sasa sema tu 'Hirizi' zenu ziliwabeba.
 

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,853
2,000
Mkuu, wewe ni mzoefu wa jf, uwe unatulia basi unaandika vitu vya maana. Heading yako na content ni vitu viwili tofauti kabisa.
"Wanasiasa waandamizi" (wingi) - ni kina nani?
"Hawakuhudhuria mazishi" - PM alihudhuria mazishi!
Yani umejichanganya vibaya sana.
Au umeona nongwa PM kwenda kumjulia hali mama Suzana Magufuli ambaye amekuwa kitandani kwa zaidi ya miaka 2 kwa kuwa ni mama yake Mwendazake?
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,482
2,000
Mkuu, wewe ni mzoefu wa jf, uwe unatulia basi unaandika vitu vya maana. Heading yako na content ni vitu viwili tofauti kabisa.
"Wanasiasa waandamizi" (wingi) - ni kina nani?
"Hawakuhudhuria mazishi" - PM alihudhuria mazishi!
Yani umejichanganya vibaya sana.
Au umeona nongwa PM kwenda kumjulia hali mama Suzana Magufuli ambaye amekuwa kitandani kwa zaidi ya miaka 2 kwa kuwa ni mama yake Mwendazake?
Pumbavu huna Akili usinipotezee muda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom