Kumbe kukeketa wasichana Wakikurya ni mradi wa wazee!

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
452
624
Nasikiliza hapa [HASHTAG]#SupaMix[/HASHTAG] [HASHTAG]#Zembwela[/HASHTAG] [HASHTAG]#Bishagagi[/HASHTAG] [HASHTAG]#Mwanne[/HASHTAG] na wengineo..

Wanadai kukeketa wasichana wa Wakikurya ni mradi wa kina mama na wazee wa Kikurya! Siku zote nilidhani wenzetu hizi mila zenye madhara ni jadi na Utamaduni wao, kumbe wazee wanaingiza hela ya kufa mtu kutokana na hizi mila zenye madhara.
Wanadai kuanzia faini kwa wasichana walioingiliwa, michango, misosi siku ya tukio wakeketaji wenyewe n.k. n.k.

Kama ni kweli, basi haina tofauti na Utumwa, kuuwa Albino na mauwaji mengi tunaowafanyia Binadamu wenzetu...

Karibuni..

RUSHWA YA NGONO, UKEKETAJI KUPATIWA DAWA 2018
Na JOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM -
WANAHARAKATI ngazi ya jamii kutoka Kituo cha Taarifa na Maarifa Kipunguni, Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, wamezindua kampeni ya kupinga rushwa ya ngono na ukeketaji kwa mwaka 2018.


Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo imefadhiliwa na Shirika la Women Fund Tanzania (WFT), Mwenyekiti wa Mtaa wa Amani, Dani Maragashimba, aliwataka wananchi katika mtaa wake kuhakikisha kila mmoja anasimama katika nafasi yake kukomesha vitendo vya ukeketaji na rushwa ya ngono.

Mbali na kutoa wito huo, alisema atasimama kidete pamoja na wanaharakati hao katika kupinga vitendo hivyo vya ukatili na ili kumfanya mtoto wa kike kupata furaha sawa na anayoipata mtoto wa kiume ikiwa ni pamoja na kupata elimu.

“Lengo ni hadi kufikia Desemba mwaka 2018, tusisikie kunaripotiwa vitendo vyovyote vya rushwa za ngono maofisini na mitaani ikiwa ni pamoja na ukeketaji watoto wa kike na udhalilishaji wa kijinsia,” alisema Maragashimba.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho, Seleman Bishagazi, alisema wameamua kuanzisha harakati hizo mapema kutokana na kwamba shughuli za ukeketaji hufanyika katika miaka inayogawanyika kwa mbili.

Alisema wanaamini kama wazazi na watoto watakuwa na uelewa wakutosha kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili wa kingono na ukeketaji, itasaidia kujua namna ya kukabiliana navyo pale vinapotokea kwenye jamii.


“Tunaamini mzazi akijua maana na madhara ya rushwa ya ngono, itakuwa rahisi kumwelimisha mwanawe na lengo letu ni kuona watoto wajue madhara ya jambo hili wakiwa wangali wadogo kwani hata wakienda shuleni, vyuoni na maofisini watakuwa wanajua namna ya kukabiliana na vitendo hivyo.

“Suala la ukeketaji sisi kama wanaharakati ngazi ya jamii tumekuwa tukifanya jitihada kubwa kupambana na suala hili hasa ukilinganisha kila mwaka unaogawanyika kwa mbili ndio watoto huwa wanakeketwa.

“Kesi ambazo tumekuwa tukikimbizana nazo kwa kuwakamata wazazi na mangariba wanaokeketa na kuwapeleka polisi mwisho wa siku zimekuwa zikiishia hewani kwa sababu zimekuwa zikikosa ushahidi kwani ni vigumu mtoto kwenda kuwatolea ushahidi familia yake,” alisema Bishagazi.

CHANZO : MTANZANIA

RUSHWA YA NGONO, UKEKETAJI KUPATIWA DAWA 2018 -http://mtanzania.co.tz/rushwa-ya-ngono-ukeketaji-kupatiwa-dawa-2018/ via @MtanzaniaNews
 
Bila kusahau bishara ya khanga, nguo, vinywaji, shughuli nzima kwa ujumla, wanaoumia na wasichana wakibakia na madonda, maumivu, mabaka, makovu na kupoteza sehemu ya mwili wao bila sababu, ukatili wa ujabu kabisa huu...
 
Ila bibi zetu, mama zetu, dada wetu na watoto wetu wa kike wanapitia maisha magumu na ya kikatili sana, yote haya ni kwa faida ya wengine, hasa kibiashara.
UKEKETAJI ni kesi ya uhaini, ni kesi ya mauaji, ni kesi ya kuhukumiwa kunyongwa kabisa..

Watoto 67 wakataliwa na familia zao baada ya kukataa kukeketwa Watoto 67 wakataliwa na familia zao baada ya kukataa kukeketwa via JamiiForums
Jinsi FGM imeathiri mfumo wa maisha yangu(psychologically),historia ya kweli. Jinsi FGM imeathiri mfumo wa maisha yangu(psychologically),historia ya kweli. via JamiiForums
Waliokeketwa hatarini zaidi kupata maambukizi ya UKIMWI Waliokeketwa hatarini zaidi kupata maambukizi ya UKIMWI via JamiiForums
Tatizo la nguvu za kiume lilikuepo tangu zaman Tatizo la nguvu za kiume lilikuepo tangu zaman via JamiiForums
Iceland kupiga marufuku tohara kwa wanaume Iceland kupiga marufuku tohara kwa wanaume via JamiiForums
Maandalizi na tendo la ndoa kwa mwanamke aliyekeketwa Maandalizi na tendo la ndoa kwa mwanamke aliyekeketwa via JamiiForums
Mafuta ya taa kwenye chakula, kuuwa Albino, ukeketaji, majini, hirizi, yote sisi Mafuta ya taa kwenye chakula, kuuwa Albino, ukeketaji, majini, hirizi, yote sisi via JamiiForums
Matokeo ya kutokufanyiwa Tohara: Mtoto wa kike miaka 12 nayeye anataka azalishwe! Matokeo ya kutokufanyiwa Tohara: Mtoto wa kike miaka 12 nayeye anataka azalishwe! via JamiiForums
Watoto wa kike nchini uingereza wanatamani kukeketwa na wengi wamekeketwa Watoto wa kike nchini uingereza wanatamani kukeketwa na wengi wamekeketwa via JamiiForums
Watoto wa kike nchini uingereza wanatamani kukeketwa na wengi wamekeketwa Watoto wa kike nchini uingereza wanatamani kukeketwa na wengi wamekeketwa via JamiiForums
Anahitaji kukeketwa kwa hiari yake. Je ni kosa kisheria? Anahitaji kukeketwa kwa hiari yake. Je ni kosa kisheria? via JamiiForums
Familia zimewakataa watoto wao kisa hawajakeketwa Familia zimewakataa watoto wao kisa hawajakeketwa via JamiiForums
Daktari ataka ukeketaji uhalalishwe Daktari ataka ukeketaji uhalalishwe via JamiiForums
Naibu Waziri alezea sababu 4 wanawake kupata UKIMWI zaidi ya wanaume Naibu Waziri alezea sababu 4 wanawake kupata UKIMWI zaidi ya wanaume via JamiiForums
Kuzuia ukeketaji Kuzuia ukeketaji via JamiiForums
 
Back
Top Bottom