Kumbe kugombana kwa wapendanao ndio kupatana

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,806
9,303
Nianze kwa kusema hivi tu mapenzi bwana!

Ndugu zangu wa MMU nawashauri msije mkaingilia kwenye migogoro ya wapendao, eti kujifanya unasuluhisha mambo, au kuwapatanisha usijaribu hata kidogo (don't try at home or any where)

Wapendanao kweli wakigombana kama na wewe unashuhudia mchezo live! utasema kimoyo moyo "hawa mapenzi ndo basi tena" na ukijifanya kutia umbea kwenye ligi yao itakutoke masikio sio pua.

Hapa kitaa kuna wapenzi flani walizingua mchana kweupe, wakamwaga kuku kwenye mchele mwingi, bwana wee kwa lile varangati wapambe na wajuzi wa mambo wakasema pale mapenzi kwisha.

Huwezi amini wale wapenzi hata siku tatu hawajamaliza mapenzi yamerudi mara elfu tano na mia tano themanini, halafu mapenzi mubasharaa! Wapambe kimya.

Wandugu, ni hayo tu!
Niseme mapenzi kitu cha ajabu sana!
 
Achana na wapendanao.....ukiwaona hata ndugu wawili wanagombana....WAHENGA walisema...WEWE CHUKUA/SHIKA JEMBE UKALIME...

Wanamaanisha ni bora utumie muda huo wa ugomvi wao UENDE KUJIONGEZEA KIPATO...!!
 
kuliko kuingilia mapenzi ya watu kama huna chakufanya kashike kalime
 
Umenikumbusha kitu
Kuna mdada na mkaka hapa wanapenda sana kugombana Kila mmoja analalamika juu ya mwenzio Si mdada si mkaka
Mi kazi yangu nasikiliza huyu namwambia haya nitaongea nae yule nae namwambia nitaongea naye. Halafu huyoo nakaa zangu kimyaa
Siku ya siku nashangaa tu haoo jion jion wameshikana viuno wanatoka out
Nacheeeka
 
wakigombana siku nyingine wewe inabidi uwe ndugu mtazamaji tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom