Kumbe kina Invisible tuko wengi.......!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
houseparty.jpg


Peter wa Gloucestershire huko Uingereza alipatwa na jambo lenye kushangaza sana mwaka 1987. Akiwa katikati ya sherehe ya jamaa yake mmoja alishikwa na haja ndogo. Aliamua kwenda kujisaidia maliwatoni. Nyuma yake kulikuwa na mwanamke aliyekuwa anelekea huko huko maliwatoni {kumbuka sherehe ilikuwa nyumbani ambapo vyoo havikutengwa vya wanawake na wanaume}

Peter alijisaidia haraka na kutoka ili huyo bibie naye akajisaidie. Alimsalimia wakati anatoka chooni baada ya kujisaidia, lakini yule mwanamke hakuitikia. Kwa Peter halikuwa ni jambo la maana sana na hakulitilia manani. Alienda zake sebuleni ambako muziki na vinywaji vilikuwa vikiendelea. Alipofika hapo alienda kukaa kwenye meza ambapo rafiki zake walikuwepo.Alipokaa alichukua kinywaji chake na kuanza kuzungumza na hao rafiki zake. Lakini hao rafiki zake walionekana kumpuuzia. Kila aliposema wao hawakumjibu wala kumtazama, waliendelea tu na mazungumzo yao. Peter alijua wameamua kumfanyia mzaha, hivyo aliamua kunyamaza ili kujua lengo la ule mzaha wao.

Kwa kuwa alikuwa ameshikwa na hamu ya sigara, aliamua kuinuka na kumfuata bibi yake ili ampatie moto awashe sigara yake. Ajabu ni kwamba, alipofika pale kwa bibi yake na kumnyooshea mkono ili ampatie sigara aliyokuwa anavuta ili awashe yake, bibi yake hakuonekana kujali. Peter alinyoosha mkono karibu na bibi yake huyo, lakini bibie aliendelea kucheza bila dalili kwamba mbele yake alikuwa akiona mtu. Peter kuona hivyo alikasirika. Ni mzaha gani wakijinga, aliwaza! Rafiki zake pale mezani wamempuuzia na bibi yake tena anampuuzia, kwa nini? Aliamua kurudi chooni ili ajikague vema, huenda kuna kitu hawataki kumwambia kwamba amechemsha, hasa mavazi.

Peter anasimulia: Nikarudi chooni, kufika namkuta yule mwanamke bado anasubiri pale mlangoni labda akiamini kwamba, labda sijatoka humo. Nilipomuona bado anasubiri, nilikumbuka kwamba, nilipotoka nilimsalimu na hakuitikia. ‘Yule mwanamke aligeuka na kuniona. Aliponiona alishtuka sana,' ‘kumbe umeshatoka wala sikukuona, ningejikojolea nikiwa hapa hapa,' yule mwanamke alisema kwa mshangao'

Peter alisema alipoenda tena sebuleni rafiki zake na bibi yake walimuuliza alipokuwa muda wote huo. ‘chooni ndio ukae mwaka mzima?' Walimwambia. Anasema, alipowauliza kama ni kweli hawakumwona, walimwambia, hawakumwona. Aliwaeleza kilichotokea na wakabaki wameshangaa.

Je, wewe imeshakutokea hali kama hiyo? Kama bado au kama hujawahi kuisikia , haina maana kama haipo. Hiyo ni hali yenye kuwatokea watu kwa idadi ya kutosha. Tofauti iko kwenye kiwango tu. Wengine huwatokea kwa muda mfupi sana, kama sekunde tano au kumi na wengine hata dakika tano au zaidi, kama ilivyotokea kwa Peter.

Ni hali ambayo mtu anapoteza uwezo wake wa kuonwa na wengine. Mtu anaamini kwamba wengine wanamuona kama kawaida, wakati wala hawamuoni. Hawamuoni mwili na wala hawasikii sauti yake. Hali hii ambayo kitaalamu hufahamika kama invisibility, huwatokea wengi pengine hata ukiwemo wewe, bali inakuwa vigumu kung'amua kwa sababu unaweza kutafsiri kama dharau. Kwa mfano, kuna siku nilikuwa ninampa kondakta wa basi la daladala nauli, nikaona hapokei, bali anapokea za wengine tu. Kuona hivyo nilikasirika sana, na kuacha kumpa. Nilishuka kituo kinachofuata nikiwa nimenyoosha mkono ili achukue pesa zake, lakini wala hakunitazama, alikuwa anawadai wengine tu.

Kwa sababu naijua hii hali ya invisibility, sikushangaa sana, nilitabasamu. Kwa asiyeijua ataitafsiri kwa njia mbali mbali na hivyo hatajua ukweli. Kuna wakati mtu anakwenda hotelini, halafu anakuta wahudumu wote wanampita tu , hadi baada ya dakika fulani, kama vile wahudumu wanatoka usingizini ndio wanamwona na kumfuata. Mwingine anaweza hata kufoka, lakini wahudumu wanaonekana hawamjali , kumbe hawamwoni.

Hivi ni kitu gani kinatokea hadi mtu haonekani? Hilo ni swali ambalo bado halijapatiwa jibu. Lakini, huenda Wajapani watatoa jibu hivi karibuni, kwani wamegundua tayari.
 
mimi ikintokea najua ni dharau za wabongo so mimi naendelea na mambo yangu wala sijali. kama ndo nauli wala siwazi kabisa. mia
 
Umenifungua macho kuhusu Deja vu, this happens several times to me ila huwa nadhani labda ni hivi viroba tunavyokunywa!? kuna jamaa aliwahi ibiwa pesa bwenini tukiwa form five, zilitafutwa kila kona hazikupatikana, usiku nilivyolala it came to me like a dream nikawa namuona jamaa alivyoiba pesa na mtu aliyempa exactly asubuhi nikaamka na confidence kama what i saw was real nikawaambia jamaa wambane mshikaji niliyemuota na huyo mwingine aliyempa na kweli baada ya kumbana jamaa ali confess exactly kama nilivyoona, hadi tunamaliza shule jamaa wakawa wananiogopa, this happens to me so many times kwa kweli.
 
Duh hii ishu ya Invisibility mkuu Mtambuzi nilikua siifahamu.
Lakini binafsi nafahamu kitu kinaitwa Deja Vu na Limbo. Mara nyingi sana nimesha-experience effect ya deja vu katika maisha yangu.

hiyo deja vu ndo nini ielezee basi,haya mazingaombwe kwa kweli,tuseme unakua umeitwa na Mungu au,Mtambuzi elaborate mo pls
 
Mtambuzi ndugu yangu natamani sana hali hii ya "invisibility" iwe inanikuta mara nyingi sana hususani ninapokuwa kwenye mazingira haya:

1. Wezi wameingia nyumbani kwangu na mimi niko kwenye "invisible mode" - Nitawapiga mpaka basi!
2. Kuna vurugu mbalimbali na mimi niko eneo la vurugu eg. Uamsho na askari! - Itanisaidia kuwasambazia taarifa JF
3. Jamaa awe anamtokea mamsap, lol! (ingawa sipendi kumchunguza sana bata, unaweza kushindwa kumla!!!)
4. Niko vitani - na wanaonitafuta hawanioni!
5 ....
6 ....

Nafahamu ni kitu gani huwapelekea watu waingie ktk hii hali, hili nitawajuza next week ili kwa sasa nisichakachue uzi wa Mtambuzi, Lol!:becky:
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi ndugu yangu natamani sana hali hii ya "invisibility" iwe inanikuta mara nyingi sana hususani ninapokuwa kwenye mazingira haya:

1. Wezi wameingia nyumbani kwangu na mimi niko kwenye "invisible mode" - Nitawapiga mpaka basi!
2. Kuna vurugu mbalimbali na mimi niko eneo la vurugu eg. Uamsho na askari! - Itanisaidia kuwasambazia taarifa JF
3. Jamaa awe anamtokea mamsap, lol! (ingawa sipendi kumchunguza sana bata, unaweza kushindwa kumla!!!)
4. Niko vitani - na wanaonitafuta hawanioni!
5 ....
6 ....

Nafahamu ni kitu gani huwapelekea watu waingie ktk hii hali, hili nitawajuza next week ili kwa sasa nisichakachue uzi wa Mtambuzi, Lol!:becky:

Umenivunja mbavu mkuu HorsePower ,hasa hiyo ya majambazi hayakuoni afu unagawa kibano, wataenda kusimulia kuwa nyumba ile ina mashetani
 
Last edited by a moderator:
Weka Picha.


Kiukweli siamini hayo makitu wabongo wana dharau sana hasa kwenye migahawa nawashauri ma-managers waweke wahudumu wenye sura za mbuzi ili wasiwe na mashauzi.
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom