Kumbe kikombe cha babu kiliwasaidia wenye virusi vya ukimwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe kikombe cha babu kiliwasaidia wenye virusi vya ukimwi?

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Dec 1, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  <tbody>[TR]
  [TD="class: contentheading"]Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  <tbody>[TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 14 March 2011 21:40[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG]Mgonjwa wa kwanza kutibiwa na Mchungaji, akijulikana kwa jina la Wilia John Lnngume (30) anayedai kupona ukimwi baada ya kunywa dawa hiyo

  Mussa Juma, Loliondo na Deusdedit Moshi, Dodoma
  DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la 'Babu', huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi.Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Sonjo iliyoshirikisha mamia ya watu. Akizungumza katika ibada hiyo, Mchungaji Mwasapile alisema Lengume ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza kumtibu.

  Akizungumza na Mwananchi kanisani hapo, Lengume alisema baada ya mumewe, John Meneyi Lengume kufariki dunia mwaka 2002, aliamua kwenda kupima na kuonekana kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) lakini baada ya kutumia dawa hiyo alisema sasa hana tena virusi vya Ukimwi. Alisema kwa muda mrefu mama huyo alikuwa akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARV) katika Kituo cha Afya Didodigo wilayani Ngorongoro.
  Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kupona kwa mama huyo, Dk Mbosha alisema: “Hiki kitu kilituchanganya sana, nakumbuka mimi ndiye nilimpima mwaka jana... ikabidi niwaeleze watu wa maabara Hospitali ya Wasso ili wafuatilie aliyempima awali huyu mama na nilimweleza aache kutumia dawa kwani hana HIV,” alisema Dk Mbosha.
  Dk Mbosha alisema alihamishiwa katika kituo hicho cha Afya cha Digodigo zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alimkuta mama huyo akiendelea kuhudhuria kliniki na kupata ARV pamoja na ushauri wa kulinda afya yake lakini alianza kuona mabadiliko makubwa ya afya yake na ndipo alipoamua kumpima tena.

  Aliamua kumpima mwaka jana baada ya kuona 'CD4' (kinga za mwili) zake zinaimarika kiasi cha kutohitaji kuendelea kutumia dawa hizo za kupunguza makali.Aliamua kumhoji kujua siri iliyokuwa imejificha katika mabadiliko hayo ambayo alisema yalikuwa ya haraka haraka mno na ndipo alipomweleza kwamba alipata tiba kutoka kwa Mchungaji Mwasapile.
  Lengume alisema licha ya mumewe kufariki, mtoto wao mmoja pia alifariki dunia lakini baada ya kutumia dawa ya Mchungaji Mwasapile, maisha yake ni mazuri na ana mtoto mwingine mchanga anayeitwa Evelyn ... “Namshukuru Mungu na Mchungaji Mwasapile sasa nimepona na ninaishi maisha mazuri tu.”Alisema baada ya kuanza kuugua, mchungaji huyo, ndiye aliyemfuata na kumuomba amtibu akimthibitishia kwamba atapona maradhi yaliyokuwa yakimsibu.Hata hivyo, kitalaamu bado haijathibitika kupatikana kwa tiba wala chanjo ya Ukimwi.

  Ushuhuda wa Mzee Mtaki
  Mwingine aliyejitangaza kupata ahueni kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsibu baada ya kupata tiba ya mchungaji huyo ni aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mzee Ali Said Mtaki.Mzee Mtaki (81) ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mpwapwa katika miaka ya 1980, Mkuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida kwa nyakati tofauti, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mbunge wa Afrika Mashariki na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Usharika Mkoa wa Dodoma, alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kutetemeka kiasi cha kushindwa kutembea na kuzungumza vizuri.

  Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Mtaa wa Nyerere Mjini Dodoma, Mzee Mtaki alisema tangu anywe dawa ya mchungaji huyo Jumanne ya wiki iliyopita huko Loliondo, sasa anaendelea kupata nafuu siku hadi siku.
  Akiongea kwa kujiamini alisema sasa anajiona kama amepona na anaweza kuendelea na shughuli zake ikiwamo ya uwakala wa bima... "Si unaona nilikuwa natembea kwa shida, kuzungumza kwa taabu, sasa hali yangu ni nzuri nafanya kila kitu bila kusaidiwa.”Akielezea safari yake ya siku mbili ambayo ilimfikisha kijijini Samunge, Loliondo anasema alifuatana na mkewe, Amina Mtaki ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na mgongo. Anasema naye pia amepona.

  Anasema safari ya kutoka Dodoma hadi Samunge iliwagharimu Sh60,000 kila mmoja na baada ya kufika huko walikuta umati mkubwa wa watu ukisubiri kupata tiba hiyo. Anasema aliwakuta watu wa mataifa mbalimbali, Waafrika, Wahindi, Wazungu na Waarabu... "Watu walikuwa wengi na kila mtu na matatizo yake lakini Mchungaji alikuwa akiwasisitizia kwamba habagui watu na haangalii dini au uwezo wa mtu."
  “Katika mkusanyiko huo nilibahatika kukutana na Askofu Thomas Laizer wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati akiwa amefuatana na mama wa kizungu. Nilikaa karibu na mama yule wa kizungu ambaye sikumbuki jina lake. Nilimshika Askofu Laizer mkono tukasalimiana na kuongozana naye kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile."

  "Tulipofika kwa Mchungaji, Askofu Laizer akamwambia mchungaji kwamba ana wageni wake, hivyo mama yule wa kizungu akapewa dawa na mimi pia nikapewa na mke wangu akapewa pamoja na kijana wangu japo yeye hakuwa na tatizo lolote la kiafya."[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]

  chanzo: DAKTARI: MGONJWA LOLIONDO AMEPONA UKIMWI - Global Publishers

  [​IMG]
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mrema atoa ushuhuda wa 'kikombe cha loliondo

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Walioenda kwa imani wamepona....
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  sielewi kwa nini wengi walikufa
   
 5. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Moto wa mabuwa auhivishi maji!
   
 6. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hata makaa ya mawe hayaivishi maji..........maji hayaivi!
   
 7. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,337
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Walioenda kwa imani wamepona....<!-- google_ad_section_end -->

  Namwogopa mungu, mimi nilikwenda nikiwa na tatizo la moyo LV na kwa kweli nilikuwa na maumivi mara kwa mara sehemu ya kifua.Nimepona anayetaka ushahidi ani pm nimpe contacts na ushahidi.
   
 8. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tunatia aibu kwa kweli.
   
 9. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Daaah.....huyu mama mbona m'tata' hivi! Mumewe alifariki kwa HIV/AIDS tangu 2002, naye akapima akawa na maambukizi, na akatumia dawa. Na hapo ana mtoto mchanga....ina maana aliendelea 'kugawa' bila kinga wakati akijijua ana maambukizi!? Na hao waliogawiwa hawakujua kama mama mgonjwa!? Hii vita dhidi ya UKIMWI ngumu sana..
   
 10. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii story inatia aibu, hamna kitu kama hicho.
  Kuna ugonjwa gani wa virusi unaotibika?.....
  Sana sana ni vaccination, na suppression.
   
 11. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  watu wanasema eti walioenda kwa BABU walikufa!! hivi hao waliokufa ni wa wapi?
  Maana mimi nawafahamu watu kibao ambao walienda mpaka sasa wanadunda mitaani.
  Au wamekufa wakiwa hai?
  Tupeni sample jamani sisi wengine ktk mikoa tunaishi wako hai na kama kuna walioondoka in my view coz sio kikombe cha BABU, na hata sasa safari za kwenda huko bado zipo.

  Tupeni takwimu hivyo vifo vimetokea sana kyk mkoa gani? tujulisheni tujue
   
 12. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Sikumbuki kama imeshaongelewa kuwa 'walioenda kupata kikombe cha babu walikufa', na kwa walikufa kutokana na kikombe cha babu. Wizara ya Afya ilipeleka watafiti kuchunguza kama ni dawa salama (mind you...sio kama inatibu, bali salama), na ripoti yao ilionyesha ni dawa salama haina athari zozote (mind you...hawakuwahi kusema iantibu, bali salama).

  Wagonjwa walioongelewa kufa hawakuuawa na kikombe cha babu...bali walikufa kwa magonjwa yao waliyokuwa wanaumwa yakasababisha waende kwa babu (presha, kansa, kisukari, VVU/Ukimwi etc), na hii ni kwa sababu wengi waliacha tiba zao za hospitali (data za waliokufa zipo kwenye hospitali nyingi tu, na hili liliongelewa sana kwenye vyombo vya habari...tafuta utaona).
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Naona Mzizimkavu leo amekuja na staili ya kumpromoti tena babu wa Loliondo baada ya kupoteza umaarufu.
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu Watu wanapenda sana Mambo ngono Sio hapo kwetu duniani kote huku nilipo mpaka mashoga wa kumwaga (home Sexual) na mwisho wa ngono ni kupata Ukimwi Mwenyeezi Mungu atuepushe na hilo balaa la ngono Mkuu.
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
 16. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mimi nipo ngangari..asante kwa info lakini. Nikiona mtu mwenye uhitaji nitamdirect kwako. Lakin mbona zipo expensive sana? USD 300 kwa mbongo wa kawaida kuzipata ni ishu!
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa, utatanishi mtupu.
   
 18. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,231
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180

  WEWE unatia aibu!!! sio wote kama uliamini its up to you,
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,087
  Likes Received: 6,553
  Trophy Points: 280
  no comments.
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kutokana na Gharama za huku nilipo kwa ufupi dawa hazipo Tanzania zipo huku nilipo nje ya Tanzania Ughaibuni ukituma hizo pesa ninakutumia kwa njia ya ndege zitakufikia within 7 Day. dawa zenyewe zinauzwa dola 250 na gharama ya usafiri ni dollar 50 jumla ni Dola300 mkuu upo pamoja na mimi . chupa 3 kila chupa ina vidonge 60 kila siku unatumia vidonge 2 kimoja Asubuhi kimoja usiku kwa muda wa miezi 3 kwisha utakuwa na nguvu kama za chuma cha pua magoli ya kumwaga utayafunga ukiwepo kiwanjani.
   
Loading...