Kumbe kelele za feki kutoka China ni za bure tena hazina maana mhh | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe kelele za feki kutoka China ni za bure tena hazina maana mhh

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Mar 22, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI wananchi wanalalamikia ubora wa betri za Tiger Head kuwa ni duni, Shirika la Viwango (TBS) limekamata shehena ya kontena 20 za betri hizo kutoka China kutokana na kutokidhi viwango vilivyowekwa na mamlaka hiyo.
  Betri hizo za Tiger Head ambazo ni miongoni mwa betri 41 zilizopigwa marufuku nchini Kenya, zimekuwa zinauzwa kwa wingi hapa nchini licha ya mamlaka zinazohusika kukiri kuwa nyingi hazina ubora unaotakiwa.
  Uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa betri hizo zimeliteka soko la hapa nchini kutokana na kuuzwa kwa bei ndogo ukilinganisha betri zinazotengenezwa hapa nchini.
  Betri hizo licha ya kuwa zinaagizwa nje ya nchi zinauzwa kwa Sh 350 kwa betri moja wakati betri zingine zenye ubora unaotakiwa zinazozalishwa nchini zinauzwa kati ya 450 hali inayowafanya Watanzania wengi kukimbilia betri za Tiger Head licha ya ubora wake kuwa na walakini.
  kwa habari zaidi nenda http://www.habarileo.co.tz
  SOURCE:Habarileo
   
 2. m

  major mkandala Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Betri hizo licha ya kuwa zinaagizwa nje ya nchi zinauzwa kwa Sh 350 kwa betri moja wakati betri zingine zenye ubora unaotakiwa zinazozalishwa nchini zinauzwa kati ya 450 hali inayowafanya Watanzania wengi kukimbilia betri za Tiger Head licha ya ubora wake kuwa na walakini.
  kwa habari zaidi nenda http://www.habarileo.co.tz

  ACHA KUWADANGANYA USIKIMBILIE BEI RAHISI NDUGU UTAUMIA KAMA UAMINI NENDA KARIAKOO KANUNUE BETRI ZA GARI ZA BEI RAHISI UONE HAW WACHINA WACHAFU WE WAACHE KAMA WALIVYO USIWATETE KABISA ........HAKUNA KITU WASICHOACHA KULETA WAMELETA HADI MISUMARI ,CEMENT.NA VIFAA VINGI VYA UJENZI FEKI..KAZI KWA WATANZANIA
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  kelele zinakuwa vp bure. serikali inatakiwa kuwa macho na udhibiti wa kutosha. pamoja na hayo, kikubwa ni kwa mtumiaji mwenyewe kuwa makini wakati wa kununua bidhaa za aina mballimbali, msipende vitu vya bei ya chini. Hata hao wachina wana bidhaa nzuri sana, lakini haiji kwa wingi katika soko la bongo kwa sababu wabongo wengi wanapenda vitu vya bei nafuu!!!!
   
 4. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Tatizo hili linanzia kwa waagizaji... wafanyabiashara wakiwa wanapiga mahesabu ya
  kutengeneza faida kubwa wanaenda China na kununua hizo bidhaa kwa bei bafuu za kutupa nao kwa ajili ya kujiongezea cha juu bila kuwekeza pesa nyingi... Huu ni wizi wa machomacho na ni ufisadi wa kibiashara.... TBS watupiemacho sana na wateketeze bidhaa zote feki ili wafanyabiashara hawa washikishwe adabu..Tena haitoshi wafunguliwe mashtaka ya kuhujumu uchumi.....
   
 5. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wandugu, Mchina ni noma kwa kila kitu.
  Umaskini wetu ndio unatuponza
   
 6. L

  Lukwangule Senior Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtu anayewatetea hapa labda tujifunze namna ya watuw anavyozungumza nimekuletea mpaka mahali pa kwenda kuona hiyo taarifa wka urefu ni shauri la kwanini wenzetu wakipiga marufuku sisi tunafungua tumekuwa jalala la maji machafu mbona hatuoni aibu?: Wapi bwana wee!FCC wanasema wao mhh TBS wanasema ahaa nini hii? Unadhani nilikuwa nawatetea nimewapasha habari watu watambhue Tiger Head WAZIOGOPE KAMA UKOMA kama wewe unadhani nimetetea you you yooo u wrong !take care
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu
  maelezo yako yapo wazi uwatetei bali kichwa cha habari ndio akijakaa vzuri kinaonyesha kuwatetea check it
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  tulivofungua milango yetu hadi mwisho wa bawaba si tulisema tumejiandaa? shirika la kuchek ubora ao TBS walitakiwa wawe wa kwanza kuwa wamejiandaa, haya ndio madhara, mao wakati anagoma kufungua milango ya china in 50's alisema ''when you open the window along with good weather come all kind of vermins'' hakua mjinga, ndio ii tunayoipata, kwa sasa serikali inachoweza wasaidia watu ni kwa kutoa elimu kwa watanzania vitu vingi hasa vya electronics na electrical watu wakanunue kwa dealers!
   
 9. L

  Lukwangule Senior Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thumb up Bona... nakupa nne hapana na nusu hapana nakupa mkono mzima yaani tano yaani ''when you open the window along with good weather come all kind of vermins'' ha ha ha ha that is true na kama hukujiandaa kukabiliana na huyo vemini hakika utalamba visivyolambika duh
   
 10. L

  Lukwangule Senior Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kabisa lakini hii ilikuwa kejeri.. Yaani tunapiga kelele kuhusu feki.. tuna madude sijui tbs na sijui fcc na sijui nini yailahi... lakini nini tunafanya.. kumbe kelel zetu ni za bure kabisa hazina maana kama kelele hizi zingelikuwa na maana basi tungelifanya samthing au vipi ndio maana namuunga mkono Bona tuna mushkeri si kawaida sori 4 misandastanding'
   
 11. m

  major mkandala Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  disregard roger
   
Loading...